Hii imekaaje, Mimi na kaka yangu hatuna ukaribu wa hata kujuliana hali lakini kwenye matatizo tunasaidiana sana kuliko marafiki tuliozoeana sana.

Hii imekaaje, Mimi na kaka yangu hatuna ukaribu wa hata kujuliana hali lakini kwenye matatizo tunasaidiana sana kuliko marafiki tuliozoeana sana.

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
nina kaka yangu alienizidi miaka 8, kiukweli hatujazoeana sana nadhani hii imesababishwa sana kwa yeye kunionea utotoni maana nimekula sana vipigo vyake, hii hali ilinifanya nimchukie na ikapelekea mpaka mawasiliano yetu kuharibika hadi sasa maisha ya ukubwani... nipo karibu na dada yangu.

Yani hata ile kuchati tu whatsapp ni nadra sana, sana sana ni kuangaliziana status za whatsapp, hata kutembeleana majumbani kwetu labda kuwe na ishu muhimu sana.

Ila licha ya hivyo tuna ukaribu sana kwenye kunasuana kwenye matatizo, matatizo ambayo hata rafiki zetu mabesti mengi wanatukimbia.

-nikiwa nimemaliza chuo niliwahi kufungua biashara, haikufika hata wiki 2 nikaibiwa,, ni kaka yangu ndie alienipa pesa ya kugharamia vitu vyote nilivyoibiwa na ilizidi,

-kuna kipindi kaka nae aliingia kwenye matatzo, marafiki walimkimbia, mimi ndie nilihangaika kumtoa kituo cha polisi.

-gari yangu iliwahi kugongwa maeneo ya ofisi ya kaka, nakumbuka kaka yangu ndie alishughulikia mpaka kumlipisha aliegonga atoe hela ya matengenezo.

- kaka yangu kuna kipindi aliumwa sana, mimi ndie niiemuuguza kwa wiki 2 hivi japo nilimuuguza kikauzu na alivyoanza kupata nafuu nikasepa.

- habari za kaka yangu huwa nazipata kwa wife wake, akiwa na matatizo basi mke wake ndio hunijulisha.

-Mimi na kaka yangu kama hatujuani vile na ni nadra sana kupeana misaada ya pesa mara ya mwisho mwaka juzi, ila ikitokea huwa ni simu moja tu muamala umesoma,
 
Kawaida Sana hio ! Mm kidoogo sister zangu ndo ukaribu upo, yupo mmoja tu ndo tunamawasiliano ya karb mambo/mipango yetu mingi tunashirikishana !!

Nnao Kaka wa3, Yani hata miez 3 inapita bila mawasiliano! Ishu za msingi za kifamilia tunashirikishana fresh tu,,,, !!! nampigia/kumtext namwabia nn bila ishu ya msingi ? Big no !! Wao pia ivo ivo hawanicheki bila ishu ya msingi
 
Mimi na kaka yangu alienizidi miaka 8, kiukweli hatujazoeana sana na hata zamani alikuwa ni mbabe sana kwangu, hali hii ilinifanya nimuogope sana kwa hio nilikuwa nipo karibu na dada yangu ambae anafata baada ya kaka.

Kusema kweli mawasiliano yetu ni madogo sana, yani hata ile kuchati tu whatsapp ni nadra sana, hata kutembeleana majumbani kwetu labda kuwe na ishu muhimu sana.

Ila licha ya hivyo tuna ukaribu sana kwenye kunasuana kwenye matatizo...
Ila licha ya hivyo tuna ukaribu sana kwenye kunasuana kwenye matatizo...[emoji1541]
Hilo ndio muhimu kuliko yote
 
Mimi almost wote tunaweza piga hata miaka miwili bila simu wala nini connection bi mkubwa ukimpigia ndo anakwambia na wenzio hawajambo tunakutanaga kwa ishu za msingi tu.
 
Huyo ndo ndugu yako sasa,au unataka mtu wa kutaniana nae?,acha mambo yako kama mnasidiana vya kutosha basi ji jambo zuri zaidi
 
All in all kaka ni kaka tu. Hakuna mtu atakaewez kukusaidia kama si familia yako tu ukipatwa na matatizo.. note this guys!
 
nachojilaumu ni kwamba sikuwahi kumdindia aache uonezi wake, laiti ningelifanya hilo basi leo hii tungekuwa karibu sana.... nimeona watu kama wawili waliwahi kufanya hii kitu iliwafanya wazoeane sana na kaka zao
Ha ha pengine si sababu ya kuelewana kistori ama kwa namna nyingine lakini Ni Kwamba katika familia Ni kawaida kabisa wengine kuelewana vyema kabisa na wengine no.
Licha ya hivyo Hili Lisisabishe chuki hata tushindwe kusaidiana matatizoni

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
nina kaka yangu alienizidi miaka 8, kiukweli hatujazoeana sana nadhani hii imesababishwa sana kwa yeye kunionea utotoni maana nimekula sana vipigo vyake, hii hali ilinifanya nimchukie na ikapelekea mpaka mawasiliano yetu kuharibika hadi sasa maisha ya ukubwani... nipo karibu na dada yangu.

Yani hata ile kuchati tu whatsapp ni nadra sana, sana sana ni kuangaliziana status za whatsapp, hata kutembeleana majumbani kwetu labda kuwe na ishu muhimu sana.

Ila licha ya hivyo tuna ukaribu sana kwenye kunasuana kwenye matatizo...

-nikiwa nimemaliza chuo niliwahi kufungua biashara, haikufika hata wiki 2 nikaibiwa,, ni kaka yangu ndie alienipa pesa ya kugharamia vitu vyote nilivyoibiwa na ilizidi,

-kuna kipindi kaka nae aliingia kwenye matatzo, marafiki walimkimbia, mimi ndie nilihangaika kumtoa kituo cha polisi.

-gari yangu iliwahi kugongwa maeneo ya ofisi ya kaka, nakubuka kaka yangu ndie alishughulikia mpaka aieigonga akatoa kama laki 2 hivi za matengenezo.

- kaka yangu kuna kipindi aliumwa sana, mimi ndie niiemuuguza kwa wiki 2 hivi japo nilimuuguza kikauzu na alivyoanza kupata nafuu nikasepa.

- habari za kaka yangu huwa nazipata kwa wife wake, akiwa na matatizo basi mke wake ndio hunijulisha

-Mtu ambae anagombana na kaka yangu ni wajibu wake ajue huo ugomvi utanihusu mimi pia.
Huo ndio upendo wa ndugu, ukaribu gani unautaka zaidi? Wakati mpo pamoja kwenye mambo yote muhimu, kwenye shida na raha.
 
Kama mi na chalii angu, pia mi na mabroo zangu wote hatunaga story mingi simu inaezapita hata miezi kadhaa, ila kwenye shida au maswala ya msingi tunaunganisha wallet kiroho safi tu
 
Wanaume wengi ni wagumu kwenye suala la mawasiliano. Zaidi kwa sababu ya mihangaiko ya maisha.

Ni wachache wanaowasiliana na hao utakuta kwa sababu ya kusukumwa na wenza wao.

Wanawake ndio tuna hayo mambo ya kupigiana simu na kutia story za hapa na pale. Bila kusahau kupeana ubuyu [emoji23]
 
Mimi na mdogo wangu tumetenganishwa na barabara kubwa tu ya Tabata Seregea, lakini huwa kwa miezi minne au sita tunaweza tukawa tumewasiliana mara moja tu na hapo hadi mimi kaka mtu nimpigie simu au akiwa na shida na muamala. Yote kwa yote sioni tatizo lolote naona fresha tu. Hata watoto wangu na wake hawajuani kabisa
 
Back
Top Bottom