Friday Malafyale
JF-Expert Member
- Jan 18, 2017
- 1,811
- 2,916
Mi nina kaka yangu ambaye tumeshare baba, ila mama tofauti mwanzo tulikuwa fresh tu kimawasiliano tokanipo school hadi chuo kikuu. Basi miaka kadhaa nyuma niliibiwa kiasi kikubwa cha fedha ofisini kwangu, mengine siyasemi maana nahisi yumo akijua key tu za post atanijuwa ni mimi. Basi nikaomba msaada niinuke nikaona amekuwa mzito, viswahili vingi 3 months kila ukimpigia mara naumwa, niko busy nikapiga chini mawasiliano na kufuta namba zake zote voda, tigo, Halotel na Airtel anazomiliki. Nikaishi fresh tu miaka kama mitano kila mmoja busy na yake na hatujawahi onana. Mwaka fulan akaenda home kusalimia akaanza kulalamika kwa dingi na maza kwamba dogo simuelewi nahisi hatuelewani. Mi nna maisha yangu nae kivyake sinaga muda kupigia magoti hata uwe mkubwa kwangu ganzi kwa kwenda mbereee bhita ni bhita muraa