Jamani kuna vitu hutokea katika maisha ambavyo hata nyie mukiulizana hampati jibu.
Kama ulivyosema hawa hawakugombana. Kuachana kwao ilikuwaje. Walipotezana? Mawasiliano hayakuwepo. Mimi namfahamu jamaa mmoja alikuwa na GF wake tangu wakiwa form 1 wakapotezana walipomaliza form 4. Siku moja jamaa anakatiza mitaa ya DSM wakati wa likizo akakutana na wake wa zamani wakarudiana tena. Miaka ikakatika mara wakatenganishwa na jeshi, bibie songea braza bulombora. Kumaliza JKT tu wakakutana wakijiandaa na vyuo. Kiutani wakaleta kiumbe duniani. Ikabidi mvulana atangulie chuo maana bibie analea mimba. Kapata chuo urusi. Miezi tisa kwisha wakawa na mtoto wa kike. Jamaa huko urusi anasikia kuwa mwana kaja! Miaka ikakatika bibie naye kaenda pale mlimani. Man si unajua tena mambo ya Russia tena miaka 7 sio mchezo. Kurudi kakuta demu keshaokomea kwa met pale mlimani. Haikuwa taabu wala hawakukasirikiana. Bahati mbaya sana yule jamaa wa mlimani aliyechukua demu jumla hakumpenda yule binti wa jamaa. Wakamtafuta wakampa mtoto wake. Jamaa aliyeenda kusoma Urusi hakuoa kamwe. Kwa kuwa hakuwa na mke ikabidi ampeleke mtoto boarding school. Miaka kadhaa baadae muoaji kapata ajali na kufariki. Bibie ana watoto 3 wa kiume. Muda ukapita! Mara akaamtafuta jamaa na kufanikiwa kumpata huko Katesh- Babati. Jamaa mkulima lakini maisha yake bomba sana. Sasa mama wa yule binti akawa anamtembelea kwa kigezo cha kumuona mtoto. Siku hazigandi, historia ikajirudia wkakuta wanalala kitanda kimoja na safari hii kapata mtoto wa kiume. Makubaliano yakafikiwa! Bibie aliporudi Dar akafungasha mpaka watoto wa marehemu mumewe wakahamia Katesh. Amini usiamini HUWEZI HATA KUJUA YUPI NI MTOTO WAKE NA YUPI SI WA KWAKE. Wanaishi kwa raha mno.
Hakuna kitu kama matapishi hapa ila pia MAVI YA KALE HAYANUKI!