Hii imekaaje wapendwa


Atakuwa alifichwa huyo bidada, wanawake na sie tuna viherehere wewe bday ya mume wa mwenzio unaivalia njuga namna hiyo.basi atakuwa mke hajui. mwisho wake iliisha salama?
 
Pia tukumbuke pamoja na kugombana kama wapenzi maisha bado yanaendelea, ipo siku mtakutana. Hakuna haja ya kuwekeana visasi mpaka mnavuana na c***i mlizopeana zawadi wakati mkiwa kwenye good terms

inategemana sana mliachanaje....wengine hatutaki hata kupishana nao rodini coz cku nzima itakuwa imeshaharibika.
 
Hilo hata mimi nimeliona maana unakumbushwa na mtu wa more than 10yrs? Aibu ningekuwa mimi nisihudhuria kabisa


kuna kupitiwa jamani, yeye ni binadamu kama wengine labda alijisahau, kuna mambo mengi humu ndani ya nyumba so kwa kusaidiana tunaweza kukumbushana pia sio mbaya na huyu x kukumbuka bday ya huyo kaka haimaanishi kwamba ndio alimpenda/walipendana kwa dhati...mbona hawakuishi pa1?.....Dena mie wala nicngejuta ningeeenda na ningeshukuru kuondoka bila kujua nani kaandaa hiyo party coz ningejua yangekuwa mengine.
 
Lol huyo mke kazubaa sana hivi nafikiri mie nifanyiwe bday na x wangu niende n a mume wangu hivi inakujaje hapo. atleast wangejifanyia wenyewe mchana kuliko kuwachoresha wenzao

kwa ujumla huyu x ana kiherehere....
 

Nyamayao mpenzi umepotea hivyo kuna ni jamani tumekumiss lol. Umeona ee hata mimi ningeenda kabisa kama alimpenda si angemwoa ila ni vizuri kama ulivyosema bora uondoke usijue ni nani alieandaa hiyo party
 
kwa ujumla huyu x ana kiherehere....


Tena kiherehere haswa unaingia migharama kumuandalia mume wa mwenzio party wakati una mumeo na familia inayokutegema akitoka hapo kwa mkewe wewe kuonana mpaka adanganye kwake lakini upo tu kujiingiza magharama makubwa hivyo.
 
maisha fulani ambayo ni kawaida sana huko mashariki ya mbali kwa kina Nyani Ngabu! Kwa hapa kwetu ngumu sana hii... I wish DA utuletee mrejesho nyuma baada ya mwenye mali kurejea.
 
Na huyo mke aliendaje kwenye shughuli asiyojua mwandazi? Nadhani hajui wajibu wake ndo maana wenzie wanamsaidia.


Buke tunaambiwaga ofc imejitolea kunifanyia party...hii kitu imenigusa sana coz friday na mie niliambiwa utumbo huu huu nikaenda kwenye bday party iliyoandaliwa na wafanyakazi wenzake...
 
hii ya kuwa marafiki na ex mwenzenu ilinishinda kabisa, ni drama tu mda wowote mnamegana, hasa kama uliachwa bado unapenda ni ngumu kushinda majaribu

sitaki kusikia habari ya ex kwenye mahusiano yangu kabisa, huyo mama anaibiwa

Hizo point nzito sana aisee
 
Buke tunaambiwaga ofc imejitolea kunifanyia party...hii kitu imenigusa sana coz friday na mie niliambiwa utumbo huu huu nikaenda kwenye bday party iliyoandaliwa na wafanyakazi wenzake...

Duh pole sama mwaya inawezekana nae huyo kachomekea wafanyakazi wenzake kumbe humo ndani kuna ex aahh siombe hiyo iwe hivyo
 
 

kuna watu mpo sensitive sana...mie bday yangu mwaka jana alisahau/pitiwa ckujali kabisa zaidi kwenye mida ya saa 12 mchana ndio nikamtumia sms kumkmumbusha, alisema samahani mambo yakaendelea, sio big deal kwangu na sio lazima akumbuke na hii miparangano ya maisha kuna kupitiwa jamani, mamangu mzazi anasahau kaniazaa lini nije nimshikike mtoto wa watu bastola kwa kupitiwa kukumbuka?....huyu mwanamke ana kimbembele chake, hapo inaonyesha bado anampenda huyo bwana....
 
Hizo point nzito sana aisee


Dena ndo hivyo katika kuachana sio kwamba wote wawili mnakuwa mmechokana, mmoja wapo atakuwa bado anapenda na anatamani warudiane, sasa mtu kama huyu akiombwa gemu hawezi kubisha lazima atoe tu, huku akiamini labda watarudiana,

Mimi urafiki na ex big NO labda tukutane njiani nitamsalimia
 

Kwa kweli hapa nakuunga mkono kwa hili hata mie huwa sipendi maana saa nyingine naona kama karoho kanauma vile
 
Nyamayao mpenzi umepotea hivyo kuna ni jamani tumekumiss lol. Umeona ee hata mimi ningeenda kabisa kama alimpenda si angemwoa ila ni vizuri kama ulivyosema bora uondoke usijue ni nani alieandaa hiyo party



nipo dearest, mambo yalikuwa yamebana sana....hope ni mzima wa afya!....Maty kwangu mie ni bora nicjue kabisa coz hii ishu ingewahusu wote mr/x...wewe umemwandalia kama nani/wewe umenileta huku umeandaliwa na x wako kuja kunichoresha ama....hii hotuba ingehitimishwa pasaka walaahh.
 
Hao ma-EXs wote hakuna hata mmoja aliye serious na ndoa yake na si ajabu "nyuma ya pazia" wakawa na mahusiano ya unyumba kama kawaida.
 

DA, hebu nijibu kwanza haya maswali.

1. Samaki wako umeenda mtoni/ziwani (tena Vicoria au Lweru) ukamvua na tayari yuko kwenye kikaango, unaweza kumlisha tena chambo kama wewe siyo chizi?

2. Una soda yako iko kwenye friji (tena yako, siyo kwa kaka au shemeji), unaweza kutoa pesa ukainunua tena?

Nitakuja baadaye tuendelee na mada!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…