Nina huyo Dada yangu, hajawahi kunisifia.
Kila atakaponiona ataniambia sijapendeza, nimenenepeana sana nimekuwa kama kiroba.
Unazeeka, umekua mbovu. Na hata tukiongozana barabarani hunifananisha na watu, hunionyesha mtu....yaaani umemuona yuleeee Ndo yupo kama wewe
Hii imenifanya nitumie muda mwingi kujitizama kwenye kioo
Jana nimekutana naye tena, ameniona nikiwa na simu nyingine hii siyo mpya nimepewa tu na boyfriend wangu.
Kwakuwa simu yangu haikufaa iliharibika sana,
Basi akaniambia heee umenunua simu, umejitahidi, NIKAMWAMBIA sijanunua nimepewa na boyfriend wangu
Akaanza, heee mwanamke mzima unapewa simu mbovu?
Mwanaume anakupaje simu mbovu kama hiyo, loooh haoni aibu.
Haikushika simu, aliiyona tu ikiwa kwangu...nilishangaa ubovu kaona wapi? Mbona mimi naiona ni nzima na nzuri na inafaa ni samsungA70 sijuh
Sasa huyu ni Dada yangu nampenda sana.....mbaya zaidi kamwambia mtoto wake WA kiume asiwe anawasiliana na mimi kwasababu mimi siyo mtu mwema.
Huyu mtoto wake, alinitafuta na kunieleza vile mama yake kamwambia.
Jaman huyu ni Dada yangu yupo around 43 years na mimi ni mkubwa ila ni mdogo sana kwake,
Mimi nampenda sana, naumia kuyaona haya....
Nachagua kujitenga naye, najua hili litamuuza sana mama........
Huyu ni Dada yangu ila hatujashare chochote,
Mama yake amenilea mimi kwasababu ni mama yangu yaani ni mke WA baba yangu.
Nampenda sana huyu mama yake kwasababu amenipenda sanaaa mimi amenilea mimi tangu nipo mchanga mpaka leo nimekua Dada.
Naweza kumtenga huyu Dada yangu???
Sasa nitaishi mwenyewe kama mkiwa daah
Wakinieleza tatizo nawasaidia...huwa natoa hata kile cha mwisho nilichobakiwa nacho....
Niliuza kitu changu ili ipatikane pesa kwaajili ya (kuhonga) kumpa mtu ili amuunganishe na kazi huyu mtoto wake na ilifanikiwa....
Ni vingi nimefanyaaaaa, basi hata aone nampenda kumjali mama natumia pesa ninazozipata kwa taabu kumfanya mama afurahie hatakama Sina.....