Mkuu naomba twende taratibu na kwa hoja.
Kwani Madereva wanagoma kwa sababu ya kutaka uhuru wa kuvunja sheria za Barabarani?
Tuongelee hasa barabara za mikoani.
Hakuna ambaye hajui kuwa madereva wanaonewa.
Hakuna ambaye hajui kuwa hata kama Huna Kosa. Traffick anakuambia naomba hela ya maji.
Hasa hasa Mikoani.
Kwakuwa magari Makubwa yanaingiza hela. Traffick na wenyewe wanaona ndio sehem ya Kuishi nao.
Hizi 5k na 10k zinaachwa sana njiani.
Na hapo sio kwamba ni over speed.
Ila labda umetanua sehem ambayo ina hard line.
mfano unaenda Karagwe. Umekutana na Lori Chalinze.
linaenda taratibu. Mko kwenye hard line. Dereva anaona kuna usalama kutanua.
Unafikiri ataacha kutanua?.
Hata mm ningetanua.
Kumbe kuna kijamaa kimekaa kinapiga picha na kutuma kwa traffick wa mbele.
Ukishikwa unakatwa point kwenye leseni.
Leseni ina Point ni 15 . Kwa miaka 5.
Ila kosa moja ni point 3.
Hapo ni makosa matano tu. Unafutiwa leseni.
mfano wa kosa hapo juu Dereva wa Dar-karagwe anaweza fanya hata mara 10+ kwa safari moja. Kwa maana hiyo safar moja tu inatosha kufutiwa Leseni.
Na ukikataa kukatwa point.
Basi wanataka mpunga mrefu. Maana wanajua wamekushika pabaya.
Hawa Mapolisi wetu wasipewe kuamua ishu kubwa namna hii. Hapa tu wanatuonea. Sasa wakipewa madaraka zaidi itakuwaje?.