Mkuu naomba twende taratibu na kwa hoja.Nchi hii ngumu sana, karibu kila kona watu hua wanalalamika bajaji na pikipiki zibanwe, leo kibano kibataka kuanza kwa maderva magari. Watu wanakataa
econonist jana nimetaja katiba ukadhani napiga majungu katiba,
Mimi nauliza tunapotaka uwajibikaji kwa viongozi sisi hatuhusiki?
Dereva yupo radhi afanye makosa ila asisimamishwe kazi kwa muda kwa sababu "anasomesha" "anafamilia"
Uwiano huu wewe unauafiki?
Aisee noma sana Mkuu.Imezoeleka kila siku asubuh kuwa wanaoenda mjini huwa wanatanua.
Na ni traffick wenyewe ndio wanakuita utanue njia.
Na jion inakuwa vice versa.
Sasa siku hiyo Dokta katanua kama kawaida. Maana ni mazoea kutanua njia mida hiyo .na hakuwa mwenyewe. Kuna magar mbele yake na nyuma yake. Yote yametanua.
Ila traffick akawa ameamua kusitisha utanuaji. Akawa anawafuata madereva na kuwambia wasitanue tena.
Akafika kwa Dokta akamwambia usitanue, na kwann unatanua?.
Dokta kamwambia hata jana mida hii nimetanua. Tumezoea.
traffick akawa mkali. Wakajibizana ,na traffick akamtukana dokta "kulalamamaake" na kuchomoa funguo.
Dokta kisukari kikampanda akashuka na ndio wakaanza U-john Cena.
Nimesikia story kutoka kwa mmoja wa mashuhuda.
Miongoni mwao ni hilo, nimesikia jana madereva wakisema hawawezi kucontril gari kwenye 80 inawafanya muda mwingi waangalie dashboard hivyo wanapoteza umakiniMkuu naomba twende taratibu na kwa hoja.
Kwani Madereva wanagoma kwa sababu ya kutaka uhuru wa kuvunja sheria za Barabarani?
Mkuu naomba twende taratibu na kwa hoja.
Kwani Madereva wanagoma kwa sababu ya kutaka uhuru wa kuvunja sheria za Barabarani?
Sheria lazima zifuatwe kama zilivyo wekwa kwa upande wa madereva.Miongoni mwao ni hilo, nimesikia jana madereva wakisema hawawezi kucontril gari kwenye 80 inawafanya muda mwingi waangalie dashboard hivyo wanapoteza umakini
Ufafanuzi wako mzuri sana mkuu.Tuongelee hasa barabara za mikoani.
Hakuna ambaye hajui kuwa madereva wanaonewa.
Hakuna ambaye hajui kuwa hata kama Huna Kosa. Traffick anakuambia naomba hela ya maji.
Hasa hasa Mikoani.
Kwakuwa magari Makubwa yanaingiza hela. Traffick na wenyewe wanaona ndio sehem ya Kuishi nao.
Hizi 5k na 10k zinaachwa sana njiani.
Na hapo sio kwamba ni over speed.
Ila labda umetanua sehem ambayo ina hard line.
mfano unaenda Karagwe. Umekutana na Lori Chalinze.
linaenda taratibu. Mko kwenye hard line. Dereva anaona kuna usalama kutanua.
Unafikiri ataacha kutanua?.
Hata mm ningetanua.
Kumbe kuna kijamaa kimekaa kinapiga picha na kutuma kwa traffick wa mbele.
Ukishikwa unakatwa point kwenye leseni.
Leseni ina Point ni 15 . Kwa miaka 5.
Ila kosa moja ni point 3.
Hapo ni makosa matano tu. Unafutiwa leseni.
mfano wa kosa hapo juu Dereva wa Dar-karagwe anaweza fanya hata mara 10+ kwa safari moja. Kwa maana hiyo safar moja tu inatosha kufutiwa Leseni.
Na ukikataa kukatwa point.
Basi wanataka mpunga mrefu. Maana wanajua wamekushika pabaya.
Hawa Mapolisi wetu wasipewe kuamua ishu kubwa namna hii. Hapa tu wanatuonea. Sasa wakipewa madaraka zaidi itakuwaje?.
Ninyi watu wa JF ni watata sana aisee.Hili swali ulilouliza unataka kujibiwa kwa mujibu wa sheria au kwa maoni tu ya watu na kwa jinsi watakavyo ona wao?