Hii ina maana gani kwenye mahusiano?

Hii ina maana gani kwenye mahusiano?

Salam wadau,

Mwezi wa pili mwanzoni kuna binti niliona bora tu ahamie getoni kwangu tuishi kama mke na mume japokuwa bado sijajitambulisha kwao lakini wazazi wake wananifahamu!!!

Lengo langu nilipanga mwezi wa kumi nikajitambulishe na ikiwezekana nimalize kila kitu hasa mahali awe mke rasmi!!

Utata upo hapa, kwa kawaida sina mazoea ya kuota ndoto lkn nashangaa kuna ndoto inajirudia, leo ni mara ya tatu naota kuna ndege anajenga kiota kwenye mti uliokauka ambao ushaanza kuoza imenifikirisha sana je hii ina maana gani? Na kwa kawaida ndege huwa hawaweki viota kwenye miti iliyokauka?!

Je ina maana naweka mipango ya ndoa kwa mtu asiye sahihi??

Mwenye uelewa anisaidie tafadhari!
Huyo sio wako, mtu uliooza ni huyo binti na ndege ni wewe, unafanya makao kwenye kitu kilichooza au kufa ambacho hakina mchango kwako zaidi ya kuporomoka. Utakapo muoa jua kwamba huwezi kupiga hatua mambo yako yotee yataporomoka, mti uliokauka hauna faida kwako. Muombe Mungu sana
 
Back
Top Bottom