Hii inatokea na inawezekana tu Tanzania, hivyo acheni wenye Akili watucheke na watudharau kwani tumejitakia na tunastahili

Je kuna article inayoeleza nini awamu na awamu moja ni muda gani? Kwa kumbukumbu zangu nakumbuka mzee ruhsa alipokuwa rais wa zanzibar ndie alieanza kutumia neno awamu ndani ya serikali akiashiria kipindi chake cha utawala, sikumbuki kabisa kama katika katiba ya Tanzania kuna neno awamu na kama limebainishwa muda gani ni awamu moja.
Niko radhi kukosolewa.
 
Katiba inazungumzia awamu kama kipindi cha miaka 5 ambapo inasema Rais atakuwa na vipindi viwili vya miaka 10 pia katiba inazungumzia Rais wa kuchaguliwa yani electoral President pia katiba ibara ya 35 kifungu cha 5 inazungumzia Rais kama Ofisi si mtu so makamu atakuchukua madaraka ya Rais kumalizia kipindi cha kilichobaki ambacho kikatiba ni miaka 5
 
Nguzo kuu ya nchi ni kuamini katika ujinga na mjinga mkuu ni mwanasiasa.Sielewi kwanini bado wanang'ang'ania kuifanya iwe awamu ya sita!? wakati katiba ipo wazi!
 
Labda umeshindwa kufahamu ninachokiuliza, ninachokiuliza hapa ni kuwa neno "awamu" lipo katika katiba?
 
Muktadha wa neno awamu katika uongozi wa nchi yetu limejengwa katika kuuesabu vichwa vya Marais walioliongoza taifa letu.

Ni ile hesabu ya kawaida kabisa moja ,mbili nk.
Hivyo tumahesabu Nyerere (1),Mwinyi (2),Mkapa (3),Kikwete (4 ) Magufuri (5) na Samia (6).

Uchaguzi mkuu hauna kitu chochote cha ku-influence neno awamu.Hata Magufuri angegombea vipindi vitano ingebaki kuwa awamu moja tu ya tano.
 
Hivi katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana 2020, kama TL angemshinda JPM na kuwa Rais, angekuwa ni Rais wa awamu ya 5 au 6? Kwa nini?

Binafsi naamini awamu ni kipindi cha urais. Ni regime. Katika hilo swali langu kama TL angeshinda basi ingekuwa ni awamu ya 6 na sio ya 5. Nyerere aliongoza Tanzania kama Rais kutoka 1964 mpaka 1985....awamu ya kwanza. Magufuli kaongoza miaka 5 na miezi kadhaa, awamu yake (utawala wake) ukakoma alipofariki. Sasa tuna Rais mwingine, ni Urais (awamu ya..) wa Samia. Tupo awamu ya sita.

Hatupo chini ya utawala (awamu ya..) wa JPM kwa sasa. Ameshakufa, tumeanza awamu nyingine mpya. Rais ni mpya, kaapa upya.

Kazi iendelee!
 
100%
 
We bwana hauchokagi kutwa nzima unashinda JF kupoteza ushenzi?
 
1)neno awamu lipo katika katiba?

3)na kama lipo limefafanuliwaje?

4)na kama halipo,hyo tafsiri yenu mmeitoa wapi!

5)je nyerere aliongoza awamu ngapi katika miaka yake 23?
 
Hili siyo bunge la awamu ya tano ni bunge la 12 na huu ni mkutano wa tatu.
 
Labda umeshindwa kufahamu ninachokiuliza, ninachokiuliza hapa ni kuwa neno "awamu" lipo katika katiba?
Kifungu cha 42 na 43 vinazungumzia Terms of office of President kwa maana ya (mihula) ambapo ni miwili na isizidi miaka 10 swala la Awamu (phase)lipo kwenye tafsiri tu ya Kiswahili ambapo kila mtu anaweza kuja na tafsiri yake mwenyewe.
 
Utakufa ww msukuma
 
Wamwache mama yetu apige kazi, hakika ni chaguo sahihi la watanzania walio wengi.
 
Awamu haihesabiw kwa Miaka inahesabiwa kila anapoingia rais Mpya. Kwa maana hiyo hakuna wabunge wa awam ya tano.
 
Tunawakaribisha katika Kutuua Watu wa Mitandaoni ili tuache kuwa Wakweli, Wakosoaji wa Mantiki na tusiotaka Uwongo wala Kujikomba Kwao ili wabakie na Wapumbavu wao wengi wanaowamudu na kuwalelekesha watakavyo.

Mathayo 10:28
Msiwaogope wauao mwili(Binadamu), wasiweze kuiua na roho; afadhali muogopeni yule(MUNGU wa Mbinguni-JEHOVA) awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanamu.
 
Tunawakaribisha katika Kutuua Watu wa Mitandaoni ili tuache kuwa Wakweli, Wakosoaji wa Mantiki na tusiotaka Uwongo wala Kujikomba Kwao ili wabakie na Wapumbavu wao wengi wanaowamudu na kuwalelekesha watakavyo.
Haa has a ukitoka kwenu aga kabisa mana uhakika wa kurudi Tena mdogo....
 
Nani ameleta habari za kumchukia?? Umelewa sio???

Upumbavu wenu na kosoa kosoa zenu zisizo na msingi hazina nafasi AWAMU hii.

Mheshimiwa rais Mama Samia hana muda wa kusikiliza kosoa kosoa za kipumbavu. Muda wake ameutenga kutumikia Watanzania
Hivyo ndivyo mulivyokuwa mnamsifia hayati lkn kumbe alikuwa mwendazake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…