Hii inatokea na inawezekana tu Tanzania, hivyo acheni wenye Akili watucheke na watudharau kwani tumejitakia na tunastahili

Ungetambua maana ya awamu za urais zinavyotambulika na mnyumbuliko wa namba za kibunge katika utambuzi wala usingebabaishwa kwa kuweka kapu moja vitu vyeny mnyumbuliko tofauti.

Ulitaka aseme yy ni rais wa awamu ya tano B?

Awamu za urais hutambuliwa kwa Personality ya Rais husika sio uchaguzi wala muda wa kukaa madarakani. Awamu ya kwanza ilikuwa na miaka 24 kwa sababu ilikuwa na mtu mmoja tu. Awamu ya 5 ilikuwa ya miaka mitano na kiezi mitatu kwa sabab Rais wa awamu hyo alifariki akiwa ofisini. Kwa sasa Tupo awamu ya Sita ya Rais mpya wala haijalishi amepatikanaje iwe kwa kupigiwa kura au kukwea nafsi kikatiba.

Bunge la sasa halitambuliwi kuw an bunge awamu fulani( Awamu huambatana na Urais) Bunge lina mnyumbukiko wa namba zake katka utambuzi. Hili sasa n Bunge la Kumi na mbili(12) chini ya Spika Job Ndugai.
 
Rais Mama Samia Suluhu Hassan ameendelea 'Kuchemka' kwa Kujiita ni Rais wa Awamu ya Sita ila amesahau kuwa Leo amehutubia Wabunge waliochaguliwa katika Awamu ya Tano.

Nao Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo muda mwingi walikuwa wakimfurahia, wakimpigia Makofi, wengine hadi kupiga Sarakasi katika Viti vyao na Kumuimbia Rais wa Awamu ya Sita Mama Samia Suluhu Hassan huku wao wakijitambua kuwa ni Wabunge wa Awamu ya Tano.

Huenda Mimi Generalist na baadhi ya Watanzania wenzangu wachache sana Wanaojitambua ( Werevu ) hatujui kuwa kumbe baada tu ya Kifo cha Hayati Rais Dkt. Magufuli tarehe 17 Machi, 2021 Kesho yake kulifanyika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ambapo Rais Samia akaibuka Mshindi wa Kura pamoja na Wabunge na kuwa rasmi ni Rais wa Awamu ya Sita pamoja na hao Wabunge na Madiwani.

Leo Watu wa Mitandaoni tumetishiwa na kuambiwa kuwa kumbe tunajulikana na wakikutaka basi muda wowote ule watatupata.

Nawapongeza kwa hilo ila Rais Mama Samia nae akae akijua kuwa wengine hata ikitokea tumekufa kwa Kulazimishwa ( Kuuawa ) kwa kuwa Wakosoaji wenye Mantiki humu Mitandaoni dhidi ya Utawala wake huwa tunafurahi kwani kwa Mwenyezi Mungu atatupokea kama Mashujaa wa kuwa Wakweli, siyo Waongo na kutopenda Unafiki wala Kujipendekeza Kwake.

Msimamo wangu Generalist ni ule ule tu kuwa Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Sita ndani ya ( katika ) Awamu ya Tano iliyo katika Muhula wake wa Pili ( wa mwisho )

Sipo katika Kundi la 'Vichwa Maji' wengi.
Bunge la awamu ya Tano[emoji16][emoji16][emoji16]

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kuwa na akili sana Ila zikusaidie

Kwan katiba ya nchi inasemaje kuhusu makamu wa rais?

Tupunguze stress
 
Mama mjanja kweli manake anajua akijiita raisi wa awamu ya 5, basi 2025 ndani ya CCM kutakuwa na mchuano wa kumteua mpeperusha bendera kiti cha uraisi...
Ila akisema yy ni wa awamu ya 6...basi 2025 CCM watasema wafate utamaduni apewe awamu ya pili apeperushe bendera ya kiti cha urais uchaguzi mkuu bila pingamizi kutoka chamani
 
Rais Mama Samia Suluhu Hassan ameendelea 'Kuchemka' kwa Kujiita ni Rais wa Awamu ya Sita ila amesahau kuwa Leo amehutubia Wabunge waliochaguliwa katika Awamu ya Tano.

Nao Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo muda mwingi walikuwa wakimfurahia, wakimpigia Makofi, wengine hadi kupiga Sarakasi katika Viti vyao na Kumuimbia Rais wa Awamu ya Sita Mama Samia Suluhu Hassan huku wao wakijitambua kuwa ni Wabunge wa Awamu ya Tano.

Huenda Mimi Generalist na baadhi ya Watanzania wenzangu wachache sana Wanaojitambua ( Werevu ) hatujui kuwa kumbe baada tu ya Kifo cha Hayati Rais Dkt. Magufuli tarehe 17 Machi, 2021 Kesho yake kulifanyika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ambapo Rais Samia akaibuka Mshindi wa Kura pamoja na Wabunge na kuwa rasmi ni Rais wa Awamu ya Sita pamoja na hao Wabunge na Madiwani.

Leo Watu wa Mitandaoni tumetishiwa na kuambiwa kuwa kumbe tunajulikana na wakikutaka basi muda wowote ule watatupata.

Nawapongeza kwa hilo ila Rais Mama Samia nae akae akijua kuwa wengine hata ikitokea tumekufa kwa Kulazimishwa ( Kuuawa ) kwa kuwa Wakosoaji wenye Mantiki humu Mitandaoni dhidi ya Utawala wake huwa tunafurahi kwani kwa Mwenyezi Mungu atatupokea kama Mashujaa wa kuwa Wakweli, siyo Waongo na kutopenda Unafiki wala Kujipendekeza Kwake.

Msimamo wangu Generalist ni ule ule tu kuwa Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Sita ndani ya ( katika ) Awamu ya Tano iliyo katika Muhula wake wa Pili ( wa mwisho )

Sipo katika Kundi la 'Vichwa Maji' wengi.
Iko hivyo. Yaani tunaweza SEMA hivi, awamu ya tano: JPM/SSH. Awamu ya tano muhula wa mwisho. Kama footbal inavipi do viwili vya dk 45.
 
Nafikiri Kwanza tujue maana ya neno lenyewe " Awamu" Kimaana neno hili haliendi kinyume na neno "Zamu" , "Zama" ama kipindi" au "nyakati" . kila " Awamu" katika serikali huwa na "mkuu" wake yaani Rais. Kwa muda wote atakaokaa madarakani huunda awamu yake moja (kiutawala) . Kwa mujibu wa katiba Rais mmoja anaweza kuwa "mkuu" wa serikali Kwa "awamu" mbili lakini Kimantiki huwa ni awamu moja iliyogawika katika vipindi yaani A na B , hivi vipindi viwili Kama mechi moja ya mpira wa miguu. ambapo kila "kipindi A na B" kina miaka mitano Kama dakika 45 za soka ( na hapa ndipo wengi pamewachanganya) . Awamu ya Kwanza " mkuu" wa serikali alikuwa JK Nyerere aliyeongoza "awamu" moja yenye jumla ya miaka 23. Nyerere alipostaafu " awamu" , "Zama" ama wakati wake ukaishia hapo, ikaja "awamu " ama "Zama" za Alhaji Mwinyi ambayo ilidumu Kwa miaka "10" awamu ya Mwinyi iliisha Kwa yeye kumaliza mda uliowekwa kikatiba, ikaja awamu ya tatu na ya nne zilizoisha Kwa namna Kama ya Mwinyi. Ikaja awamu ya tano iliyoongozwa na JPM ambapo awamu yake imedumu Kwa takribani miaka sita , awamu ya JPM imeisha Kwa yeye kufariki (R.I.P) kabla haijakamilika miaka iliyowekwa kikatiba Kwa awamu moja . Rais akifarik na "Zama" , wakati wake wa kutawala huishia hapo . Kifo kimekatisha awamu ya utawala wa JPM na kutulazimisha kuingia awamu ya "sita" ya Rais Samia Suluhu Hassan. Awamu za uongoz hazibadiliki Kwa uchaguzi pekee Kama wengi walivyokariri bali zinaweza kubadilika Kwa Rais wa awamu husika kujiuzulu "kung'atuka" , kumaliza kipindi chake kikatiba na Hata Rai's kufariki.

Mama Samia ni Rai's wa awamu ya sita.
 
Mama anasisitiza kuwa hii ni awamu ya 6.
Nchi hii ilipata mapinduzi matukufu na muungano.
Kusanyo la kodi kwa sasa ni 1.9trillion kwa mwezi
Industrial park ni lazima
Kodi sio shuruti wala kutumia nguvu
Expatriates wapewe vibali bila kuadhiri wazawa
Usajili wa wawekezaji uharakishwe
Maongezi ya miaka 6 yanaenda kukamilishwa kwa vyovyote vile.
Waliosema Magu katangulizwa atawatafuta, ila wanaosema ni korona wako free ingawa yeye kasema ni moyo.

Kazi iendelee.
Mimi nadhani habari ya Kifo Cha mtangulizi wake na tetesi za mitandaoni kuhusu Kifo hicho angeachana navyo, hasiviongee publically, maana kuendelea kuongelea issue hii inatufikrisha Sana.
 
Nguzo kuu ya nchi ni kuamini katika ujinga na mjinga mkuu ni mwanasiasa.Sielewi kwanini bado wanang'ang'ania kuifanya iwe awamu ya sita!? wakati katiba ipo wazi!
Pengine sababu yaweza kuwa kuna mambo yasiyokuwaopo kwenye ilani yanataka kuchomekwa na mengine kuondolewa, pasipo kuwaandaa watu ki saikolojia kwa misemo (slogans) ni ngumu kuwatoa kwenye Magu mode waliyomo .Hivyo ndo maana hadi Mungu mpya jamHuri naye kawa introduced nika kama kwa jina la Osiris wa Misri ya kale
 
Mimi nadhani habari ya Kifo Cha mtangulizi wake na tetesi za mitandaoni kuhusu Kifo hicho angeachana navyo, hasiviongee publically, maana kuendelea kuongelea issue hii inatufikrisha Sana.
Ni kweli aachane na mambo ya mtandaoni na inawafanya hata ambao hawakuwa wamesikia hizi tetesi ambao ni wengi kuliko mtandaoni waanze kuzijadili pia mbeleni inaweza leta shida kwenye nchi ya watu wanotafuta mchawi mtu wao anapokufa kawaida tu kwa kudhani kalogwa suala la sumu ni kubwa mno kwao hasa ukichukulia mwendazake kwenye moja ya hotuba zake aliwahi sema kutendewa hivyo..achape kazi tu
 
Mama anasisitiza kuwa hii ni awamu ya 6.
Nchi hii ilipata mapinduzi matukufu na muungano.
Kusanyo la kodi kwa sasa ni 1.9trillion kwa mwezi
Industrial park ni lazima
Kodi sio shuruti wala kutumia nguvu
Expatriates wapewe vibali bila kuadhiri wazawa
Usajili wa wawekezaji uharakishwe
Maongezi ya miaka 6 yanaenda kukamilishwa kwa vyovyote vile.
Waliosema Magu katangulizwa atawatafuta, ila wanaosema ni korona wako free ingawa yeye kasema ni moyo.

Kazi iendelee.
Haya majadiliano ya miaka 6 ni ya nini
 
Katiba inazungumzia awamu kama kipindi cha miaka 5 ambapo inasema Rais atakuwa na vipindi viwili vya miaka 10 pia katiba inazungumzia Rais wa kuchaguliwa yani electoral President pia katiba ibara ya 35 kifungu cha 5 inazungumzia Rais kama Ofisi si mtu so makamu atakuchukua madaraka ya Rais kumalizia kipindi cha kilichobaki ambacho kikatiba ni miaka 5
Mkuu unalazimisha sana, acha kuteseka!
 
Nakubaliana kabisa na wewe.

Samia Suluhu ni Rais wa sita lakini aliye wa awamu ya tano.

Siombei wala sitaki iwe hivyo, ila kwa mfano ikitokea Samia anakufa, basi Philip Mpango atakuwa Rais wa saba katika awamu ya tano.

Hatokuwa Rais wa awamu ya saba!

Kwangu mimi awamu zinaendana uchaguzi baada ya muhula wa Rais kuisha.

Muhula wa pili ya Rais Magufuli haujaisha. Yeye Magufuli kafariki. Na ilivyo kikatiba, makamu wake ndo amekuwa rais.

Not a big deal. But it’s as simple as 1,2,3.
kwahiyo kwa mujibu huo wamaelezo yako akimaliza anagombea aongoze kwa mihula miwili sio[emoji848]au anagombea amalizie mi5 iliyo baki
 
Nafikiri Kwanza tujue maana ya neno lenyewe " Awamu" Kimaana neno hili haliendi kinyume na neno "Zamu" , "Zama" ama kipindi" au "nyakati" . kila " Awamu" katika serikali huwa na "mkuu" wake yaani Rais. Kwa muda wote atakaokaa madarakani huunda awamu yake moja (kiutawala) . Kwa mujibu wa katiba Rais mmoja anaweza kuwa "mkuu" wa serikali Kwa "awamu" mbili lakini Kimantiki huwa ni awamu moja iliyogawika katika vipindi yaani A na B , hivi vipindi viwili Kama mechi moja ya mpira wa miguu. ambapo kila "kipindi A na B" kina miaka mitano Kama dakika 45 za soka ( na hapa ndipo wengi pamewachanganya) . Awamu ya Kwanza " mkuu" wa serikali alikuwa JK Nyerere aliyeongoza "awamu" moja yenye jumla ya miaka 23. Nyerere alipostaafu " awamu" , "Zama" ama wakati wake ukaishia hapo, ikaja "awamu " ama "Zama" za Alhaji Mwinyi ambayo ilidumu Kwa miaka "10" awamu ya Mwinyi iliisha Kwa yeye kumaliza mda uliowekwa kikatiba, ikaja awamu ya tatu na ya nne zilizoisha Kwa namna Kama ya Mwinyi. Ikaja awamu ya tano iliyoongozwa na JPM ambapo awamu yake imedumu Kwa takribani miaka sita , awamu ya JPM imeisha Kwa yeye kufariki (R.I.P) kabla haijakamilika miaka iliyowekwa kikatiba Kwa awamu moja . Rais akifarik na "Zama" , wakati wake wa kutawala huishia hapo . Kifo kimekatisha awamu ya utawala wa JPM na kutulazimisha kuingia awamu ya "sita" ya Rais Samia Suluhu Hassan. Awamu za uongoz hazibadiliki Kwa uchaguzi pekee Kama wengi walivyokariri bali zinaweza kubadilika Kwa Rais wa awamu husika kujiuzulu "kung'atuka" , kumaliza kipindi chake kikatiba na Hata Rai's kufariki.

Mama Samia ni Rai's wa awamu ya sita.
Kama unaandika Barua ndefu hivi na unashindwa tu hata kuweka Paragraph ili ueleweke Kiuandishi hizi Hoja zako za Kipunbavu zitaweza Kueleweka kweli?
 
Mkuu say thumb up kwa mama,OK umejitahidi kichanganua lakini ulichokosea kuchanganya bunge mhimili tofauti kabisa na mhimili.alikuwepo Mama samia,pia rais siyo lazima apatikane kupitia uchaguzi mkuu,na ndo maana hata katiba yetu ibalitambua hilo

Hivyo SSH ni rais Wa sita katika awamu ya sita,
 
Katiba inaweka limits ya vipindi vya uongozi lkn haikatazi Rais wa kipindi kimoja! Kama ingetokea Jiwe kukaa ama kuwekwa pembeni na Chama chake October 2020, na CCM wakatuletea Mgombea mwengine... na akashinda.. angekuwa Rais wa awamu ya ngapi?
Nakubaliana kabisa na wewe.

Samia Suluhu ni Rais wa sita lakini aliye wa awamu ya tano.

Siombei wala sitaki iwe hivyo, ila kwa mfano ikitokea Samia anakufa, basi Philip Mpango atakuwa Rais wa saba katika awamu ya tano.

Hatokuwa Rais wa awamu ya saba!

Kwangu mimi awamu zinaendana uchaguzi baada ya muhula wa Rais kuisha.

Muhula wa pili ya Rais Magufuli haujaisha. Yeye Magufuli kafariki. Na ilivyo kikatiba, makamu wake ndo amekuwa rais.

Not a big deal. But it’s as simple as 1,2,3.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom