Hapa tatizo linalojitokeza ni kuanza miradi mipya kabla ya kumaliza Ile ya zamani. Miradi inarundikana hata haijulikani upi ni upi. Mawaziri husika hudaganywa kuwa kazi inaendelea na wafanyapo ziara Wakandarasi huwekwa vifaa vyao kazini ila wakiondika vinarudishwa camp. Kibaya zaidi ni kutoa taarifa za uongo kwamba mradi umefikia asilimia 95 ilhali hata kwa macho hizo 20 hazifiki. Hali hii inatisha na si salama kwa maendeleo ya Taifa.