Mwizukulu mgikuru
JF-Expert Member
- Oct 21, 2021
- 6,788
- 16,227
Mara nyingi ukihoji kuhusu utendaji kazi wa serikali huwa wanatokea wazarendo uchwara na wapigaji wakubwa, utasikia anakuambia "unataka serikali ikuletee maendeleo mlangoni kwako?" Wengi wao ukiwatizama huwa ni watu ambao huwa wamegawanyika kwenye makundi mawili, kundi la kwanza ni watu flani ambao wamejikatia tamaa kundi hili huwa limejaa wajinga wengi na watu wenye kipato Cha chini sana yaani wasioweza kuwa hata na uhakika wa kupata Milo mitatu. Kundi hili ndilo lilikuwa ni wafuasi hasa wa magufuri 😁, na mara nyingi kundi hili huwa hawaamini kwenye kupata utajiri mkubwa utasikia mfano msanii Diamond 💎 ni freemason 😂😂. Kundi la pili ni kundi lililopata mafanikio kwa njia ya kubebwa almaarufu" connection" kundi hili huwa ni wabinafsi sana na huamini yeyote yule anaeibeza au kuhoji kuhusu serikali iliyopo basi anataka kuharibu ugali wao kwa hiyo hutumia njia zote kumdhibiti ikiwezekana hata kumuuwa kabisa. Watu wengi huwa wanashindwa kutambua kuwa ili yapatikane mafanikio ya mtu mmoja mmoja basi inatakiwa serikali itoe support katika nyanja zote za kiuchumi na pasina kupendelea kundi flani katika nchi.