Kila weekend yaani jumamosi jumapili wanafunzi wote wananafasi ya kupiga simu kwa wazazi ndugu na jamaa kupitia simu za waalimu wote wanapewa namna hiyo ya mawasiliano bado wanapaswa wawe chini ya uangalizi wa waalimu
Yani mwanafunzi wa form six kwa nini atumie simu ya mwalimu kuwasiliana na wazazi wake.
Form six anauelewa wa kutosha.
Hili liangaliwe vizuri. Wapewe ruhusa ya kuwa na vitochi sio smartphone.
Haya mambo yanatatiza mana Kuna kilio kikubwa cha watoto kulawitiwa au kubakwa na walimu .
Hii ni kutokana na vitisho na kificho .
Mtoto anapewa simu ya mwalimu anapiga simu amesimamiwa na mwalimu hivyo anashindwa kueleza kwa wazi unyanyasaji anaoupitia.
Matokeo yake inakuja kubainika too late.
Dunia imebadilika ,tuliosoma boarding school zamani tulikua na uhuru wa kuandika barua Moja kwa Moja kwenda kwa wazazi ,ndugu,marafiki mpaka nje ya nchi. Zilikua zinapitia posta na zinaletwa kila siku . Ukiwa na shida unawasiliana na jamaa Yako Moja kwa moja.
Barua za urafiki ,mapenzi ya ujana zilikua nyingi sana kama njia ya kurefresh akili tu.
Leo wanafunzi wananyimwa njia ya kuwasiliana na wazazi wao kwa uhuru lakini vitoto vidogo vinapelekwa beach kukaa uchi vikitazama vibabu na vibibi vya kizungu vikiwa uchi ufukweni. Wakirudi wanakua na picha za hovyo kichwani kwa muda mrefu.
Wanatunzi wanajengewa woga mkubwa sana mashuleni na baadhi ya walimu kutumia mwanya huo kuwafanyia vitendo vya kikatili ikiwemo kulawitiwa .
Hili liangaliwe kwa undani zaidi.
Miaka ya nyuma ilikua vigumu sana kusikia mwalimu amemlawiti mwanafunzi.
Kwanza angepokea kichaoo kikubwa sana na mgomo mkubwa ungefuata.
Tunajenga kiizazi laini lkama kuku wa kisasa.
Ndio maana siku hizi wakifika vyuo vikuu wanasumbuka sana na masuala ya mahusiano na hata kujiua . Wanakua kama wametoka gerezani.
Vijana wa kidato Cha sita wanapaswa kujitambua zaidi kuliko kujengewa hofu.
Wanatakiwa wapewe ruhusa ya kuwa na visimu vidogo vya mawasiliano tu . Na muda wa mawasiliano utengwe.
Wanaoridheshwa majina ya wale wenye simu . Zinakusanywa kila Jumatatu asubuhi kupewa Kila Jumamosi asubuhi ili wawasiliane Kwa uhuru na jamaa zao.