Hii kesi mdogo wangu ana haki au hana?

Hii kesi mdogo wangu ana haki au hana?

Mimi ni mwalimu kiuhalisia hakuna sheria za wizara au za nchi zinazozuia mwanafunzi kumiliki simu,ni utashi na sheria uchwara za walimu na shule

Mimi nimemiliki smu kwa kificho nilipokuwa kidato cha tano na sita na asilimia 99.9 ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita walikuwa na simu japo sheria za shule zilikuwa zinakataza.

Ni wajibu waserikali kutoa tamko/mwongozo wa kuwaongoza walimu na wanafunzi juu ya matumizi sahihi ya simu kwa dunia ya leo ,huku ni kubinya uhuru wa wanafunzi hasa huyu wa kidato cha tano na sita ambaye ni mtu mzima,wengi wao ni miaka 18/19/20 sasa huyu unazuiaje? Wakati huo mwenzake aliyeenda vyuo vya kati mfano diploma au certifivate level akiruhusiwa kumiliki simu
Big up mkuu.
Akili kubwa 👍👍👍
 
nna mdogo wangu alikua shule moja mkoa wa Dodoma, akakamatwa na simu shuleni na mkuu wa shule akiwa form 6 siku chache kabla ya mtihani.mkuu akakaa na simu hiyo na mdogo wangu alipomaliza shule akadai simu yake lakini mkuu wa shule amegoma kumrudishia na anadai simu imeharibiwa.Ni kweli sheria ya shule hiyo simu ikikamatwa inataifishwa lakini je sheria za nchi zinasemaje,shule inatumia sheria gani kutaifisha mali ya mtu?
Nakumbuka simu yangu ilikamatwa na head master na akawa anaitumia yeye na sikumdai mpaka naondoka
 
Back
Top Bottom