Fantastic Beast
Member
- Feb 18, 2019
- 53
- 539
Hii kesi ya ugaidi inatumika kupiga ndege wawili kwa jiwe moja, ila mmoja ndiyo analengwa zaidi, kwa bahati mbaya mshika manati ndiyo anapoteza zaidi.
Nakumbuka miaka ya 2000 kuja 2005 ilikuwa ukipita mitaani chama kilichokuwa kwenye headlines ni CCM. Ndicho chama kilichokuwa kinatrend sana, Rais Mkapa kila mwisho wa mwezi alikuwa na utaratibu wa kuhutubia taifa kila mwisho wa mwezi, zile hotuba asikuambie mtu zilikuwa zinawakusanya watu vibandani na wakitoka hapo mwezi mzima ni stori mtaani.
Mawaziri wa enzi hizo pia walikuwa si watu wa mchezo mchezo, walikuwa wanatengeza headlines haswaa. Akina Kikwete,Magufuli,Mramba,Sumaye,Lowasa nk. Kwa kifupi CCM ilikuwa na watu wazito haswaa ambao walikuwa ni talk of the town.
Kuanzia 2005 mpaka 2015 CHADEMA ndipo walipoanza kuimarika na kuwa na viongozi ambao walivuta attention za watu pindi waposimama. Hiki kipindi ndicho siasa za Tanzania za kistaarabu zilikuwa kwenye the highest peak. Wanasiasa walishindana kwa hoja haswaa. CCM & CHADEMA mikutano yao ilikuwa inajaza watu 50/50, hoja zilirindima, shangwe zikapigwa na nyomi la raia, raia wakazifurahia siasa haswaa.
2015 CCM wakafanya kosa la karne, kosa ambalo kama bado hawajazinduka usingizini ndilo linalowatafuna mpaka leo na litawapeleka kaburini. Kosa lenyewe ni kitendo cha kukubali chama kugawanyika. Siasa ni watu, na watu hufuata mtu wanayemuona anawafaa kwa kipindi hiko regardless ya chama alichopo. Ndiyo maana CCM walipoparanganyika na Mr White Hair akahamia CHADEMA aliondoka na lundo la watu wake wote bila kujali anahamia chama gani.
Hapo ndipo CCM walipigwa na ganzi kwani hata mikutano yao ikawa haijazi watu kama CHADEMA. CCM wakapagawa ikabidi waanze kutumia njia mbadala kujaza majukwaa yao. Wakashinda kwa mbinde sana, uzuri walikuwa na mgombea anayenadika kirahisi.
Baada ya ushindi wakaunda serikali. Katika process za kuunda serikali CCM wakapigwa na ganzi waliyokuwa hawaitegemei pale chifu walomsimika alipowaambia waziwazi SIPANGIWI. Huyu chifu alisahau uchifu una muda maalumu na kuna maisha baada ya uchifu. Hapo ndipo walipojua waliruka mkojo na sasa wametua juu ya nnya.
Huyu chifu akasahau yupo hapo kwa sababu ya siasa na siasa ni watu na hao watu wanapatikana kwa ushawishi wa hoja, hivyo inabidi a-balance kati ya uchifu na siasa. Wakati CCM wamepigwa na ganzi ndani mwao, CHADEMA wakaendeleza moto uleule wa enzi na enzi. Chifu akaanza kulalama kwanini watu wa chama chake wameacha kuwasha moto kama wenzao wa CHADEMA? Ikafika mpaka mahali akawachana waziwazi kambi yake ya vijana kwamba wamezidiwa na wenzao wa CHADEMA.
Chifu alipoona chama chake hawawezi tena kuwasha moto kama zamani ikabidi sasa aanze kuzima moto wa CDM. NA HILO NDILO KOSA LA KARNE.
Toka wakati huo CCM wanahangaika kuzima moto wa CHADEMA, na tukumbuke siku zote moto ukiwaka kinachomake headlines ni ukubwa wa moto na si wazima moto. Hivyo watakaoendelea kuwa juu ya vichwa vya habari ni CDM na si CCM wanaouzima huo moto. Wanaweza wakatumia nguvu kubwa sana kuwazima CHADEMA lakini hawataweza na hii ina faida kubwa zaidi kwa CHADEMA maana wanazidi kumake headlines na ndio wanaozidi kusikika huko mitaani.
Chifu Hangaya alianza vizuri sana kwa kujaribu kurudisha ile status quo ya enzi zile, na CCM walianza kumake headlines zinazokijenga chama kama zamani. Yule kiongozi wa vijana alianza vizuri sana kwa kuomba msamaha kwa yale mabaya waliyoyatenda kipindi cha nyuma, japo ilikuwa ni ajabu lakini kwa watu waungwana kile kilikuwa ni kitendo cha kiuungwana na kiliwapa credit sana.
Vyama vingine navyo vilianza kupumua kwa kufanya mikutano ya hadhara kama kawaida, raia nao tulishaanza kuyafurahia maisha yale ya kisiasa tuliyoyazoea toka zamani.
LAKINI GHAFLA, YANI ILE GHAFLAA, LIKATOKEA KUBWA KULIKO, KIONGOZI MKUU WA UPINZANI AKAPEWA KESI YA UGAIDI.
Kiongozi mkuu kabisa ambaye ni icon wa siasa za kidemokrasia na kiuungwana akakamatwa kwa tuhuma za UGAIDI. Mikutano ya hadhara na ya ndani ya vyama vya kisiasa nayo kimya kimya ikapigwa marufuku.
Kifupi ni kwamba tumerudi kule tulipotoka. Tena tumerudi nyuma mara 1000 zaidi...
Sasa chifu wa sasa kama bado hajashituka basi ajue aliye/waliomshauri wanamlenga yeye zaidi, na CHADEMA kama nyongeza tuu. Ila ambacho hajui huyo mshika manati ni kwamba yeye ndiyo anapoteza zaidi maana anazidi kuwaweka CHADEMA kwenye ramani huku akiifuta kabisa vichwani mwa watu CCM.
Kama wana CCM na wenyewe hawalioni hili basi wajiulize tangu uchaguzi wa mwaka 2020 ukamilike chama chao kimefanya nini ambacho kimewapa credit toka kwa wananchi. Wajiulize pia kati ya CCM na CHADEMA ni nani mtaani anaongelewa zaidi na nani ambaye anaheshimika zaidi.
CCM endeleeni kuhangaika kuuzima moto wa CHADEMA, lakini kaeni mkijua siku zote moto ndio unaomake headlines na sio wazima moto.