Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Hebu wakuu nanyi muicheki tuone kama bado inalipa. Hii iliandikwa kipindi kile cha mwaka 2015 wakati TAL anagombea urais. Katika uzi mmoja nikasema kama wakivuka salama hawa wakuu na FAM akawa mkiti, basi maridhiano yawe kwamba TAL apambane tena na SSH
Ee Mungu Baba kwa namna ya pekee utuvushie mtu huyu kwa salama ili naye atuvushe kutokea sasa na hata baadae ili akiingia kuwa kiongozi wa nchi, basi aiweke misingi ya kiutawala kwa namna ambayo hata akija kiongozi mwingine isiwe tabu kwake kuongoza. Baba ujue tunahitaji taasisi imara na si watu imara. Watu imara wawe ni kwa ajili ya kuongoza na kusimamia taasisi imara na sio mawazo binafsi.

- Mbeba maono - Tuvushe
- Mbobezi wa sheria - Tuvushe
- Mkwepa mauti - Tuvushe
- Kiboko ya wajuaji - Tuvushe
- Kipenzi cha wengi - Tuvushe
- Jabali la hoja - Tuvushe
- Ngome ya ushindi - Tuvushe
- Ngao ya haki - Tuvushe
- Mussa ajaye - Tuvushe
- Kiongozi jasiri - Tuvushe
- Mfuasi wa haki - Tuvushe
- Kimbilio la wanyonge - Tuvushe
- Kiongozi makini - Tuvushe
- Chungu cha maarifa - Tuvushe
- Msaliti wa hujuma - Tuvushe
- Mfano wa mchungaji - Tuvushe
- Haiba ya uongozi - Tuvushe
- Kitanzi cha dhuluma - Tuvushe
- Shubiri ya wapenda madaraka - Tuvushe
- Mwanazuoni - Tuvushe
- Kiama cha mahasidi - Tuvushe
- Mkweli na muwazi - Tuvushe
- Heshima ya Taifa - Tuvushe
- Tunu ya thamani - Tuvushe
- Amiri Jeshi ajaye - Tuvushe