Hii michango ya harusi laki moja mnayoweka kwenye kadi tena bila option ya kuchagua ya size yako tutaonana wabaya aisee

PROFOUND NOTION

Senior Member
Joined
Nov 3, 2022
Posts
138
Reaction score
374
MLianza na 20, 30, ikaja 50, ikaja 80, sasa hivi 100k

Laki moja imekuwa sasa kama trend.

Tena hamjali hata hali ya mtu kisa tu ni rafiki au ndugu

Hivi haya yootee ya nini, jamani,

Si mchukuane mpelekane nyumbani hivyo hivyo kwani lazima mrushe watu roho mjini humu na matarumbeta?
 
Aisee kama ulikuwepo kwenye Akili yangu,Kuna jamaa yangu eti single laki na 50, double Laki na 70!Hata kupokea simu, sipokei.
 
Waomba michango wawajielewi na wachangiaji pia hawajielewi. kumekuwa na tabia ya watu kulalamikaaa weeeeee lakini bado wanachanga na kuendekeza watu wajiombee tu michango kiholela. Kama ni lazima sana uchangie hiyo harusi changa ulichonacho bila kujali utaalikwa au laaa.... yaani ujikaze kutoa laki na nusu kwa sahani ya pilau na huku inakuuma!! eti uonekane ulichanga na ulihudhuria... huu ni utumwa. Changia pale unapoweza na unapohitajika. na usikubali mtu akukoromeee na masimu ya kila dakika akikukumbusha mchango wa harusi.
 
Sasa ivi tupo kwenye dunia ya kuacha huu ujinga,kama hutaki kitu unamwambia mtu direct tena ukiwa umenyooka kabisa,asilimia kubwa ya Watu tunaowaonea aibu hawana mchango wowote kwenye maisha yetu
 
Ubaya ubwela,... wake zao ni wake zetu
 
Mkuu,

Hivi ukiwaambia sina inakuwaje?
 
Shughuli za maendeleo ziwe kipaumbele kwenye michango yenu.

Inuaneni kiuchumi, jengeni miundombinu ya kutolea huduma kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.

Msiache kushirikiana na kushirukisha walio ndani ya jamii zenu na nje pia.
 
Mkuu ulikubali kupokea kadi ya nini?. Mimi atakayeniletea Kadi ya sherehe lazima anione mbaya!. Uchumi wa nchi hii siyo wa kufanya anasa anasa za ajabu!
 
Ukiletewa kadi inasoma single 100,000 kama hauwiwi kutoa/hauna mpatie 30/50 ya zawadi mambo yasiwe mengi….Akilaumu atajijua mwenyewe.
 
Reactions: Nus
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…