Hii midoli ya fasheni kwenye maduka inayovalishwa nguo za ndani inavunja maadili

Hii midoli ya fasheni kwenye maduka inayovalishwa nguo za ndani inavunja maadili

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Wakuu,

Hivi karibuni kumekuwa na matumizi ya midoli kwa wenye maduka ya nguo kuwavalisha mavazi yanayopatikana kwenye maduka yao

Sasa utakutana na mdoli wa kike umevalishwa sidiria na nguo ya ndani mchana kweupe na umewekwa nje kwa maonesho

Binafsi naona hata kama ni maendeleo ila sio sawa

Au mnasemaje wadau
 
Halafu kuna wengine unakuta hawajalivalisha, liko tu wazi.

Nafikiri kuna namna hapa inabidi ifanyike, siyo powa kimaadili.

Kuwe na haki za midoli.
Haha,

On a serious note mkuu,

Ile ni mfano wa binadamu kwahiyo ni kinyume Cha haki za binadamu kuweka mfano wake uchi mchana kabisa aisee tena nje.
 
Upo sahihi, kuna mmoja niliukuta uchi kabisa duka fulani
 
ukiwa peke yako ni fresh, ubaya ni pale unapokua na mama bibi au mtu mzima wa kike lazima ujibalaguze kwa aibu,
huku na wewe ukibadilisha sight
 
Back
Top Bottom