Kishimbe wa Kishimbe
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 7,835
- 8,703
BOMU LINAHESABU KINYUMENYUME!
Wakoloni wetu walituacha wamepandikiza mabomu ambayo, walijua au hawakujua, kuna muda yatalipuka! ... Rwanda walikuwa na dini moja lakini wakagawanywa kwa koo zao na baada ya muda wakalipuka!
.... TANZANIA!
Tumejitahidi sana, tokea tunapata uhuru, kusahau tofauti za makabila na koo zetu ili kutunza amani na utulivu wetu, na, kwa bahati, kwakuwa koo na makabila ni mengi sana, TUMEFANIKIWA!
JINAMIZI la Tanzania linataka kuibukia tusipotarajia kabisa, yaani kulekule tulipoweka matumaini yetu kuwa kuna viongozi wetu wa kiroho wanaojali usalama wetu kama taifa sasa ndiko moto unapotaka kulipukia! SABABU NDIPO ULIPO MGAWANYIKO WETU UNAOTUGAWA KIRAHISI SANA NA KUUNDA MAPANDE MAWILI TU HASIMU!
Tanzania tumerithi dini mbili kuu, UISLAM NA UKRISTO!
Dini ya kiislam kutoka kwa waarab, imekuwa ikiendeshwa na waislam ikiwa na utawala wa kati, BAKWATA, ambao makao makuu yake ni hapahapa Tanzania, japo kwa waislam kwa ujumla, kila msikiti ni kama taasisi inayojitegemea na sio kila muislam au msikiti upo chini ya BAKWATA kiviile!
Ukristo una madhehebu mengi, lakini kubwa na lenye ushawishi mkubwa ni dhehebu la wakatoliki lenye makao makuu Vatican kwa Papa! ... Vatican imeulea ukatoliki Tanzania kwa muda mrefu na kuujengea nguvu za kuichumi katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya na Elimu. Hili ni zuri sana maana wote tunanufaika na huduma hizi!
Tukienda mbele kidogo, sasa Vatican imeacha wakatoliki wa kila nchi wajiendeshe! Na hapo ndipo linapotaka kupasukia BOMU, maana kuendesha hiyo taasisi ni sawa na kuendesha nchi ndani ya nchi, na ndio maana mikwaruzano ya kanisa na serikali sasa inazidi kukua!
Hivi mikwaruzano hii ya ukatoliki na serikali haiwezi kuamsha chuki baina ya wakatoliki na waislam ambao uendeshaji wa dini yao, kiuchumi, hautegemeani sana na sera za kiuchumi za serikali? Hili ni bomu jamani.
TUJADILI KISAYANSI!