Hii ndio (CV) Wasifu ya Nape Moses Nnauye

Ilikuwepo Butimba sekondari form 1 - 4 kwenye majengo hayo hayo ya chuo but kumbukumbu zangu hazinipi kama kulikuwa na A-Level pale

MMh, Butimba TTC ilikuwa na high school? Hakikuwa chuo cha ualimu kile??
Anyway, hata uwe na Phd kama hamnazo za maisha hazimo tu.
 

Hapo kwenye red na nilipobold sio kweli hata kidogo, Nape kasoma Journalism and Mass Communication Acharya College which is affiliated to Bangalore University, na sio SOCIOLOGY kama unavotuambia. note lilichoandika ndio degree yake inavoitwa...sasa kama hapa tu unapindisha, je taarifa zako zinaaminika kweli?
 
Nape aliweza kurudia baadhi ya masomo na kusafisha cheti ndipo vyuo husika vikampokea; tumpe pongezi kwa uthubutu wa kutokata tamaa

Yamekuwa hayo tena? Lakini kwa nini asije mwenyewe kutueleza kwa nini nyie mmsemee wakati yeye ni hodari wa kubwabwaja?
 
jamani mbona nape mwenyewe yupo? Alete results zake za o'level na A'level ndo tutaelewa. By then kwn kipind cha miaka yake walikuwa wakisoma diploma kwa mwaka 1? Km cy basi alisoma certfct asituzingue. Lakn ni kawaida kwa watoto wa wakubwa kuonekana walifaulu kila level ila wakiambiwa wapresent issue utaona wanavojing'ata, tena ndo ikiwa kwa kingereza ndo kabisaaa.
 
naomba kuuliza tu hivi katika diploma huwa wanaadika THESIS???? au DISSERTATION?
cHUO CHA ualimu wana michepuo ya EGM?
kama alipata F FORM 4 aliwezaje kusoma huo mchepuo?
mtoa mada ili mada yako iweze kuwa na mshiko ambatanaisha TRANSCRIPT YA nape.

Anza na transcript ya Mnyika kabla ya kuhoji ya Nape. Usilete double standards hapa kama huna cha kuandika kaa chini usome. Mbona Mnyika kabwabwaja na O-level yake ya A-tisa, lakini hajathubutu kueleza form six alipata A??..
 
ndio matatizo ya.kulikoroga afu unashindwa kulinywa. ss tunaomba atoe ufaulu wake f4 na f6. mbona mnyika amefanya hivyo!?
 

Mkuu usitutoea kwenye hoja ya Msingi...anzisha Thread nyingine ya hicho unachokisema.Hapa ni Nape vs Mnyika
 
Kwani NAPE mwenyewe yuko wapi ? mbona hoja nyingine anakuwaga kimbelembele kujitokeza kama busha lisivyopenda kufichwa..aje hapa ajieleze,haya mambo si yalianzishwa na yeye mwenyewe kwa kuhoji elimu ya Mnyika? sasa ngoma imerudi kwake!! Nyie vibaraka wake kwa nini mnahangaika kumjibia si mumuite atoke huko mafichoni aje ajibu mwenyewe? :behindsofa:
 

Anza na transcript ya Mnyika kabla ya kuhoji ya Nape. Usilete double standards hapa kama huna cha kuandika kaa chini usome. Mbona Mnyika kabwabwaja na O-level yake ya A-tisa, lakini hajathubutu kueleza form six alipata A??..

Mkuu jielekeze kwenye Hoja ya msingi...BUTIMBA kuna EGM?Ilikuwaje EGM kwa matokeo ya D na F?
 

Anza na transcript ya Mnyika kabla ya kuhoji ya Nape. Usilete double standards hapa kama huna cha kuandika kaa chini usome. Mbona Mnyika kabwabwaja na O-level yake ya A-tisa, lakini hajathubutu kueleza form six alipata A??..
Kuna thread ya Mnyika bado iko open. Peleka ombi kule.

Hapa ni Nape Nnauye.
 
Ushauri kwa vijana,

Hii mijadala ya elimu ya Nape na Mnyika ina mafundisho mengi sana kwa vijana kama mnataka kujifunza. Wekeni siasa pembeni na jifunzeni jinsi maisha yanavyobadilika na jinsi ambavyo kushindwa jambo moja sio mwisho wa mafanikio.

Hapa inaonyesha wazi Mnyika alikuwa na uwezo mkubwa sana shuleni na bado ana uwezo mkubwa maana hata hoja zake nyingi zina mshiko. Lakini inakuwaje kwa miaka yote hiyo kashindwa kumalizia hako kadegree ambako kwa uwezo wa Mnyika ni kadogo sana? Sidhani kama muda ndio tatizo pekee, labda hata hakuona umuhimu, kitu ambacho mimi nakielewa maana hata akina BIll Gates, Jobs hawakuona umuhimu wa kubaki vyuoni wakati tayari kichwani walikuwa na uwezo wa kufanya yale waliyotaka kufanya baada ya vyuo.

Tukija kwa Nape ni wazi uwezo wake ulikuwa mdogo, hakuwa na credits za kuingia A-level. Lakini kijana Nape hakulala chini na kuanza kulia au kulalamika, badala yake aliamua kujiendeleza kwa kuunga uunga elimu. Mwisho wa siku amesoma mpaka sasa ana masters yake kwenye Public Administration. Hili ni fundisho hata kwa vijana wote waliofeli mwaka huu, tumieni elimu hiyo ya Nape kama hamasa ya kwamba kama Nape ameweza kwanini na nyie msiweze? Bila kujali umepata sifuri au division four. Elimu ya karne ya 21 bado kijana una nafasi ya kuweza kusoma, kujiendeleza na mpaka hata kuwa profesa ukitaka. Uamuzi ni wako, kuamua kupambana au kuishia kucheka wengine. Ukipata F si unarudia?

Sisi sote tuliosoma zamani tunawajua watu wengi sana ambao form six walipata zero hata ya F zote lakini wengine sasa ni maprofesa, madaktari, wachumi nk. Kama mtu anabisha, awaangalie watu waliokuwa wanasoma PCB miaka ya 80. Utawakuta wengi pamoja na kufeli form six lakini leo wako mbali sana. Walichofanya, walijiendeleza na kufeli form six haikuwa sababu ya kuwakwamisha. Kuna jamaa mmoja juzi juzi akaniambia utani akimsema msomi mmoja maarufu wa sheria TZ kwamba alipata division zero PCB Tabora. Nilishutuka sana, sikuamini. Lakini ukweli ndio huo, kupata four au zero sio mwisho wa elimu.

Binafsi kuna vijana nimewahi kuwasaidia ambao form four walitoka na points kama hizo za Nape. Through kuwashauri na kuwasaidia, leo hii wamemaliza degree zao na wana mafanikio kwenye kazi zao.

Sawa tutumie siasa kuchekana kama kujifurahisha, lakini kwenye mioyo yetu tutambue hili ni somo tosha. Kufeli jambo mara moja sio mwisho wa dunia. Badala yake amka, jipukute na anza safari tena kwa speed hata kubwa kuliko mara ya kwanza.

Wakati wewe unacheka na kupoteza muda, wenzako wanasonga mbele.
 
Unasema kuna mchepuo wa EGM pale Butimba TTC?! Na Nape ndio alipita hapo?! Ilianza lini hiyo?!
 
Ambatanisha na ufaulu wake kwa kila ngazi ya elimu
Good point, Mnyika alileta na grades zake alizopata kwenye kila level. Na Nape atupe grades zake. O-level, A-level, diploma, degree ya kwanza, degree ya pili. Atuambie ana class gani au alikuwa anapita kwa pass halafu hela za babake ndiyo zinampull kwenda mbele?
Lakini hebu nikumbusheni wadau, Butimba TTC in A-level? Nakumbuka pale palikuwa na shule ya mazoezi ya O-level, au CV imekosewa?
 

Mafilili Ni Maagizo ya Maandiko matakatifu kuwa tupendane sisi kwa sisi!cyo kosa la chadema.Issue hapa siyo kuwa na shahada ni mchakato wa kuipata mwisho wa huu uzi kama mods wasipouondoka utamwaacha mtu uchi wa mnyama!
 


Hiyo imekaaje kaka, Butimba TTC ni Chuo Cha Ualimu, huwa wanafundisha na EGM, n.k? i had no idea about that
 

Mkuu,hao ndio ma pro-chadema,wakimpenda mtu hadi matapishi yake huwa wanaita siagi. By the way Chadema ni watu wa shortcut at any cost. Ndio maana Mnyika alijibu ataenda kusoma apate degree Chadema itakaposhika dola,atakavyopata..connect. Lakini pia Mnyika ataenda shule kwa msukumo wa nani ikiwa viongozi wake wa juu elimu zao za kuunga kwa gundi. Mbowe_form IV,na degree za kwenye mitandao,Slaa_certificate za theology na PhD bila Barchelor wala Masters degree,Lema_form four,udalali wa madini kule Arusha.
 
Hiyo miaka iliyotajwa hakukuwa na A-Level Butima sec, labda kama imeanza miaka ya hivi karibuni.Na butimba ttc ni kituo cha privite candidates labda kama alifanya mtihani kama PC

Mkuu jielekeze kwenye Hoja ya msingi...BUTIMBA kuna EGM?Ilikuwaje EGM kwa matokeo ya D na F?
 
Swali bado linabaki:

1. Nape alifanyaje kukabiliana na kikwazo cha kukosa credit za kusoma A'level kwa Division IV points 29 ya Form IV?

2. A' level alisoma lini na wapi na alifauluje?

3. Kuna uwezekano wa kununua au kughushi cheti?

Suala ni uwazi tu. Kwenye siasa hata shule ya msingi ni qualification. Lakini tunataka ukweli na uwazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…