Hii ndio (CV) Wasifu ya Nape Moses Nnauye

[/LIST]

Ukiona mtu anahamahama shule ujue kuna tatizo.....aidha la kinidhamu au la walezi/wazazi........halafu hii haina qualifications za kuitwa CV........imekaa kama ukle wasifu wakati wa mazishi ya mtu!

acha wivu. mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. mbona mnyika amekiri kuwa hana degree!? afadhali huyu an masters
 
Uzuri hapa jf huwezi danganya!cv ya kutnka f4 hadi chuo(TTC) bila Hata ya uwazi wa ufaulu!kuna mdau mmoja ameanika matokeo yake ya f4 akimlinganisha na mnyika!ni aibu tupu!!
 
.....CV ndo nini .. hapa kazi tu ... hebu tuwekeeni CV za akina Livingstone Lusinde, MHe. Arfi, Mhe. Stephen Ngonyani (Prof. Maji Marefu), Mhe. Lukuvi tulinganishe linganishe angalau...kinachotakiwa ni kufanya kazi na kazi unayoifanya iwe inaeleweka na si vinginevyo....
 

Aisee! hapa umenifanya niange kicheko!
sasa hapo kwa nini asingeandika alikuwa "private candidate" kama sivyo basi aweke jina la shule aliyo enroll, iliyomruhusu ajisomee mwenyewe nyumbani na sio jina la kituo cha kufanyia mtihani, hata UDSM inaweza kuwa kituo vile, sasa mtu akisema kamaliza form six UDSM si atakuwa anachekesha walionuna?
 
Mwaka 1993 alifeli darasa la saba. Wakati ule jina halali la Nape akiitwa Nahum Nnauye. Waliosoma nae wanakumbuka. Bt akafanyiwa mpango na kupewa jina la Nape Mkumbo Nyagicha mtoto masikini wa Kinyiramba, aliyefaulu lakini familia yake haikuwa na uwezo wa kumsomesha.

Mwaka 1994 Nahum Nnauye akajiunga na shule ya sekondari ya kutwa Ngudu wilayani Kwimba akiwa na jina jipya la Nape. Mwaka 1995 akahamishiwa shule ya Sekondari Nsumba kwa kutumia title ya baba yake Mzee Moses Nnauye.

Mwal 1997 akafeli form four kwa kupata division four ya point 29 akiwa na D 4, c 1 na F 5. Akareseat mara 2 bila mafanikio pale Butimc TTC ambacho ni kituo cha watahiniwa binafsi. Mwaka 1999 na mwaka 2000.

Akakata tamaa na hatimaye mwaka 2001 akaamua kwenda kusoma cheti cha Uhazili (cert of secretarial services) katika chuo cha Kivukoni. So kabla sijaendelea naomba ieleweke kuwa Nahum Moses Nnauye (Nape) hajawahi kusoma form 5 shule yoyote duniani. Kama anabisha aje hapa tumuulize maswali ya Geography 1 au Ecomics 2 uone atakavyochanganyikiwa. Kwanza hajui kama kuna paper 1 na 2 A.level, atasemaje amesoma A.level?

So akatumia cheti chake cha uhazili kuomba diploma pale chuo cha Diplomasia kurasini. akapata na akaanza kusoma. Mwaka mwaka 2002 akafeli kuendelea na 2nd year baada ya kupata suplimentary 4 ktk masomo 6 aliyokuwa akisoma. So kwa kifupi akadsco. Hivyo naomba ieleweke kuwa huyu jamaa anayejiita Nape hajawahi kutunukiwa diploma yoyote kutoka Chuo cha Diplomasia Kurasini. Kwanza asikidhalilishe chuo maana pale hakuna Diploma ya mwaka mmoja. kama anabisha aupoad picha yoyote hapa alipokuwa anatunukiwa hiyo diploma.

Mwaka 2004 akatumia cheti chake cha form four kuomba degree India kwa kusaidiwa na mwandishi mmoja mashuhuri nchini kwa kuwatafutia vyuo vya nje watu waliofeli.

Na akapata kwa masharti ya kusoma miaka minne. Ikumbukwe India ni nchi yenye vyuo vya hovyo sana duniani, na ni miongoni mwa nchi ambazo hata kama una zero unaweza kusoma Bachelor bila matatizo yoyote hadi ukahitimu. Reffer kesi ya Mr.Andekisye, Lecturer aliyefukuzwa kazi Arusha University kwa kusoma elimu feki India. Andekisye aliajiriwa kama mhadhiri wa Marketing na Business Mathematics akidai ana MBA kutoka India.

Bt ilipofuatiliwa ikagundulika ni kweli ana Masters ya MBA bt hajawahi kusoma Bachelor. Alichomoka na Diploma yake ya Ualimu (Mathematics & Physics) kutoka Monduli TTC akaaply Masters India akapata akaenda kujoin. Sasa imagine mtu anatoka Diploma anakwenda Masters sembuse Nape kusoma bachelor?

Nape akapata degree yake fake ya psychology ambayo ndiyo aliyoitumia kuomba masters mzumbe. Na mzumbe hakukabidhi cheti zaidi ya kile cha degree yake ya India.
Kama anabisha aweke vyeti vyake vya o.lel na a.level hapa.

Huyo ndiye Nahum Moses Nnauye anayejiita Nape. Katibu mwenzezi wa Chama cha Mapinduzi CCM na mgombe ubunge ubungo mwaka 2010, wakati ule akijaribu kushindana na Genious John Mnyika aliyepata A 9 O.Level yeye akiwa na D 4 tu.
 

kweli ai. elimu ya nape imekaa kama msukule.
 

huyu anamfahamu sana ndg Nape Nnauye kama Nehum Nnauye,hivyo ndg anayefahamika km Nape Nnauye hana tofauti na Lameck Mkumbo Madelu aka Mwigulu mchemba au Saidi Bagaile aka Hamisi Kigwangala wote wana sifa kuu moja inayowaunganisha wote achilia mbali kuwa wanachama wa CCM.
 
1998 -2000 alisomaje 'A' level na wakati huoo kuhitimu butimba TTC? Laa kaunga unga lakini poa tu haijalishi mradi kapenya na hadi masters. Kila akiongea mnaona pumba kwa kua ni kazi ngumu kuitetea CCM.
 
duh kumbe hii 61% inaweza enda india ikarudi na degree.
nahum hebu saidia hawa vilaza wenzio.
 
Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC? ni diploma au advance level?
 
Butimba hakujawai kua shule na A-level ipo O-level pekeake na wanafunzi wa kwanzi ni sisi mwaka 1999 zaidi ya apo kunachuo cha ualimu kaka mbona tunadanganyana mchana kweupe.
 
A-level wanasoma miaka mitatu? (1998-2000). huyu dogo alirudia form two ndo maana hesabu hazikai sawa. alifeli ikabidi aende kurudia form two mwanza. 1994 alianza form one, 1995 form two akafeli, akarudia 1996. 1998 akamaliza form four na 99 akaenda A-level sijui ndo wapi akamaliza 2000. (butimba ni chuo cha uwalimu). labda akarekebishe alipo soma A-level halafu tuendelee. mia
 

Kweli, this is serious! ni kosa la jinai kughushi vyeti kwa namna yoyote, ndio maana mwaka 2008 wale wafanya kazi wa Benki kuu waliodaiwa wameghushi vyeti walipelekwa mahakamani...
 
Anyway, sio yeye mwenyewe Nape aliyeweka hii cv, labda tatizo ni source ya mtoa mada.
 
Elimu ya Nape haina mashaka wala maswali,elimu ya Mnyika pamoja na mbwembwe zote kaishia njiani.Lawama nyingi kwa serikali kwenye kujibu tuhuma kuwa hana degree.
 
hapo kwenye red....butimba ttc si chuo cha ualimu jaman...au tuseme butimba ttc secondary school?..
Kajipange upya urudi tena na kiwango cha ufaulu kwa kila level hasa hasa sekondari

matokeo ya nape ya o-level kwa maana ya form four mwaka 1997 alipata div three point 24

akajiunga na ziwani sekondari inayosimamiwa na butimba ttc kwa masomo ya a-level na alipata div four point 18.

Akarist tena matokeo hayakuwa mazuri pia, akaamua kujiunga na chuo cha siasa ya jamii pale kivukon kwa kuanza kusoma certificate na kisha akasoma diploma hapohapo ya masuara ya siasa, kwingine alikoendelea sikujua kwani tulipotezana naye.
Hata asemeje habari ndo hiyo, NA NDO UKWELI WAKE ANACHOONA AIBU KUJITOKEZA HAPA NI MATOKEO YAKE YA O-LEVAL NA A-LEVEL WANAJAMVI
ALIKUWA KIJANA WA KILOKOLE ASIYEPENDA KUDANGANYA HATA KIDOGO HAPO NYUMA LAKINI SASA HIVI KAHARIBIKA, HATA KWENYE SHEREHE ZA UKWATA NA CASFETA HAONEKANI.
 
Elimu ya Nape haina mashaka wala maswali,elimu ya Mnyika pamoja na mbwembwe zote kaishia njiani.Lawama nyingi kwa serikali kwenye kujibu tuhuma kuwa hana degree.
Ha ha haa.......elimu ya Nape? Kwani kaelimika.huyu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…