PakavuNateleza
JF-Expert Member
- Sep 9, 2009
- 1,106
- 1,297
chuo gani hicho ukikutwa na cm darasani unapelekwa kwa principal?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[/LIST]
Ukiona mtu anahamahama shule ujue kuna tatizo.....aidha la kinidhamu au la walezi/wazazi........halafu hii haina qualifications za kuitwa CV........imekaa kama ukle wasifu wakati wa mazishi ya mtu!
huyu hapa Juliana Shonza ila najua hapend kumtetea ila ni NJAA t
u.
Kakosea, Butimba TTC haina A-Level. Kama ni Butimba basi labda alikuwa anamaanisha kuwa mwaka 1998 - 2000 Nape alikuwa gereza la Butimba!Butimba Alevel?
BUTIMBA TTC ni chuo cha ualimu lakini ni center ya kufanyia mitihani kwa wanafunzi ambao hawako mashuleni.,na hili ni kwa sababu Mheshimiwa Nape hakuwa ameendelea na sekondari kwa mtindo wa Boarding School.,kwa kuwa hakupenda kuendelea kukaa boardingi hivyo aliyasoma masomo yake ya high level akiwa nyumbani na kisha kwenda chuoni hapo kufanya mtihani wa form six.
Aisee! hapa umenifanya niange kicheko!
sasa hapo kwa nini asingeandika alikuwa "private candidate" kama sivyo basi aweke jina la shule aliyo enroll, iliyomruhusu ajisomee mwenyewe nyumbani na sio jina la kituo cha kufanyia mtihani, hata UDM inweza kuwa kituo vile, sasa mtu akisema kamaliza form six UDM si atakuwa anachekesha walionuna?
Nimeamua kueleza ukweli huu baada ya kuona upotoshaji wa makusudi unaoendelea humu.
Kuna mtu kajitokeza kujibu elimu ya Nape wengi wakahoji kwani Nape yuko wapi asijitokeze mwenyewe kujibu kama alivyofanya Mnyika?
Naomba mfahamu aliyejibu ni Nape mwenyewe kwa kutumia ID ya bandia, lakini amekuwa mno too radical hadi watu wakamshtukia.
Lakini hoja sio kuwa radical, au kutumia ID bandia, hoja ni kuwa amefanya upotoshaji wa makusudi uliotuacha mdomnd wazi wale tunaomfahamu. Sasa ukweli kuhusu elimu ya Nape huu hapa.
Mwaka 1993 alifeli darasa la saba. Wakati ule jina halali la Nape akiitwa Nahum Nnauye. Waliosoma nae wanakumbuka. Bt akafanyiwa mpango na kupewa jina la Nape Mkumbo Nyagicha mtoto masikini wa Kinyiramba, aliyefaulu lakini familia yake haikuwa na uwezo wa kumsomesha.
Mwaka 1994 Nahum Nnauye akajiunga na shule ya sekondari ya kutwa Ndugu wilayani Kwimba akiwa na jina kaiba jina jipya la Nape. Mwaka 1995 akahamishiwa shule ya Sekondari Nsumba kwa kutumia title ya baba yake Mzee Moses Nnauye.
Mwal 1997 akafeli form four kwa kupata division four ya point 29 akiwa na D 4, c 1 na F 5. Akareseat mara 2 bila mafanikio pale Butimc TTC ambacho ni kituo cha watahiniwa binafsi. Mwaka 1999 na mwaka 2000.
Akakata tamaa na hatimaye mwaka 2001 akaamua kwenda kusoma cheti cha Uhazili (cert of secretarial services) katika chuo cha Kivukoni. So kabla sijaendelea naomba ieleweke kuwa Nahum Moses Nnauye (Nape) hajawahi kusoma form 5 shule yoyote duniani. Kama anabisha aje hapa tumuulize maswali ya Geography 1 au Ecomics 2 uone atakavyochanganyikiwa. Kwanza hajui kama kuna paper 1 na 2 A.level, atasemaje amesoma A.level?
So uhazili mwaka akatumia cheti chake cha uhazili kuomba diploma pale chuo cha Diplomasia kurasini. akapata na akaanza kusoma. Mwaka mwaka 2002 akafeli kuendelea na 2nd year baada ya kupata suplimentary 4 ktk masomo 6 aliyokuwa akisoma. So kwa kifupi akadsco. Hivyo naomba ieleweke kuwa huyu jamaa anayejiita Nape hajawahi kutunukiwa diplmoma yoyote kutoka Chuo cha Diplomasia Kurasini. Kwanza asikidhalilishe chuo maana pale hakuna Diploma ya mwaka mmoja. kama anabisha aupoad picha yoyote hapa alipokuwa anatunukiwa hiyo diploma.
Grace Mwasonge unamkumbuka Nape vzr maana alikuwa classmate wako wakati huo. So najua uko humu japo kwa ID tofauti naomba ujitokeze kudhibitisha ili isionekane nafanya defamation.
Mwaka 2004 akatumia cheti chake form four kuomba degree India kwa kusaidiwa na mwandishi mmoja mashuhuri nchini kwa kuwatafutia vyuo vya nje watu waliofeli.
Na akapata kwa masharti ya kusoma miaka minne. Ikumbukwe India ni nchi yenye vyuo vya hovyo sana duniani, na ni miongoni mwa nchi ambazo hata kama una zero unaweza kusoma Bachelor bila matatizo yoyote hadi ukahitimu. Reffer kesi ya Mr.Andekisye, Lecturer aliyefukuzwa kazi Arusha University kwa kusoma elimu feki India. Andekisye aliajiriwa kama mhadhiri wa Marketing na Business Mathematics akidai ana MBA kutoka India. Bt ilipofuatiliwa ikagundulika ni kweli ana Masters bt hajawahi kusoma Bachelor. Alichomoka na Diploma yake ya Ualimu (Mathematics & Physics) kutoka Monduli TTC akaaply Masters India akapata akaenda kujoin. Sasa imagine mtu anatoka Diploma anakwenda Masters sembuse Nape kusoma bachelor?
So akapata degree yake fake ya psychology ambayo ndiyo aliyoitumia kuomba masters mzumbe. Na mzumbe hakukabidhi cheti zaidi ya kile cha degree yake ya India.
Kama anabisha aweke vyeti vyake vya o.lel na a.level hapa.
Huyo ndiye Nahum Moses Nnauye anayejiita Nape. Katibu mwenzezi wa Chama cha Mapinduzi CCM na mgombe ubunge ubungo mwaka 2010, wakati ule akijaribu kushindana na genious aliyepata A 9 O.Level yeye akiwa na D 4 tu.
1998 -2000 alisomaje 'A' level na wakati huoo kuhitimu butimba TTC? Laa kaunga unga lakini poa tu haijalishi mradi kapenya na hadi masters. Kila akiongea mnaona pumba kwa kua ni kazi ngumu kuitetea CCM.Kumekuwepo na habari ambayo inavumishwa katika mitandao ya kijamii hasa hapa Jamiiforums kuhusu Elimu ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikati na Uenezi, Ndugu Nape Moses Nnauye. Taarifa hiyo kwa kiasi kikubwa inapotosha na kueleza yale ambayo si sahihi kuhusiana na CV ya Kiongozi huyo wa Chama cha Mapinduzi; Kutokana na Hilo, nimeona ni jambo la busara kuwasaidia wanajamvi kwa kuwapa CV iliyo sahihi ya Nape Moses Nnauye kama ifuatavyo;
NB: Ndugu Nape Nnauye akiwa Kivukoni aliandika thesis iliyohusu ; VIKWAZO VINAVYOZUIA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA SIASA. Na pia akiwa Mzumbe University aliandika kuhusu ; SABABU ZINAZOCHANGIA USHIRIKI WA WAPIGAKURA (ni ipi sababu ya kutojitokeza wapigakura siku ya Kura)
- Kati ya mwaka 1987-1989 alianza elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Mwanga-iliyopo Iramba Singida (ambapo alianza darasa la 1 mpaka 3)
- Mwaka 1989-1993 aliendelea na kumalizia elimu ya msingi katika shule ya Bukumbi iliyopo misungwi Mwanza.(ambako alikuwa ni kati ya wanafunzi watatu 3 kati ya 120 waliochaguliwa sekondari.
- Mwaka 1994-1995 alianza elimu ya Sekondari katika shule ya kutwa ya Ngudu Sekondari.(ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha pili)
- Mwaka 1995-1997 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Bweni ya Sekondari Nsumba iliyopo Mwanza (ambapo aliendelea kidato cha pili mpaka cha nne)
- Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC
- Mwaka 2001-2002 alisoma Diploma ya sayansi ya jamii katika Chuo Cha sayansi ya Jamii-Kivukoni.
- Mwaka 2002-2003 alisomea Diploma ya Diplomasia na uhusiano wa Kimataifa Chuo cha Diplomasia Dar es salaam.
- Mwaka 2005-2008 alisomea digrii ya Saikolojia, Lugha na Habari katika Chuo Kikuu cha Bangalore-India
- Mwaka 2009-2010 alisoma digrii ya pili ya utawala (Masters in Public Administration-MPA) katika chuo cha Mzumbe
Hii ni serious kuliko unavyodhani.
Ukosefu wa maelezo ya namna Nape alivyovuka kikwazo cha kutokuwa na credit za kufanya mtihani wa Form VI unampa doa Nape. Vile vile kukosekana maelezo ya kuridhisha ya elimu yake ya Form VI ni fumbo jingine kubwa. Tunapata hisia za uwezekano wa kughushi vyeti au udanganyifu mwingine. Integrity ya Nape inahojiwa hapa.
Ni serious kuliko unavyodhani, na haitaishia hapa JF, mpaka habari za uhakika zimepatikana
hapo kwenye red....butimba ttc si chuo cha ualimu jaman...au tuseme butimba ttc secondary school?..
Kajipange upya urudi tena na kiwango cha ufaulu kwa kila level hasa hasa sekondari
Ha ha haa.......elimu ya Nape? Kwani kaelimika.huyu?Elimu ya Nape haina mashaka wala maswali,elimu ya Mnyika pamoja na mbwembwe zote kaishia njiani.Lawama nyingi kwa serikali kwenye kujibu tuhuma kuwa hana degree.