Hii ndio (CV) Wasifu ya Nape Moses Nnauye

Hii ndio (CV) Wasifu ya Nape Moses Nnauye

Mzee wa goli La mkono
na mzima bunge live, aliyesadikika kugeuka shujaa
 
Kumekuwepo na habari ambayo inavumishwa katika mitandao ya kijamii hasa hapa Jamiiforums kuhusu Elimu ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikati na Uenezi, Ndugu Nape Moses Nnauye. Taarifa hiyo kwa kiasi kikubwa inapotosha na kueleza yale ambayo si sahihi kuhusiana na CV ya Kiongozi huyo wa Chama cha Mapinduzi; Kutokana na Hilo, nimeona ni jambo la busara kuwasaidia wanajamvi kwa kuwapa CV iliyo sahihi ya Nape Moses Nnauye kama ifuatavyo;


  • Kati ya mwaka 1987-1989 alianza elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Mwanga-iliyopo Iramba Singida (ambapo alianza darasa la 1 mpaka 3)
  • Mwaka 1989-1993 aliendelea na kumalizia elimu ya msingi katika shule ya Bukumbi iliyopo misungwi Mwanza.(ambako alikuwa ni kati ya wanafunzi watatu "3" kati ya 120 waliochaguliwa sekondari.
  • Mwaka 1994-1995 alianza elimu ya Sekondari katika shule ya kutwa ya Ngudu Sekondari.(ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha pili)
  • Mwaka 1995-1997 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Bweni ya Sekondari Nsumba iliyopo Mwanza (ambapo aliendelea kidato cha pili mpaka cha nne)
  • Mwaka 1998-2000 alisoma elimu ya juu ya sekondari (advanced level), mchepuo wa EGM na kuhitimu Butimba TTC
  • Mwaka 2001-2002 alisoma Diploma ya sayansi ya jamii katika Chuo Cha sayansi ya Jamii-Kivukoni.
  • Mwaka 2002-2003 alisomea Diploma ya Diplomasia na uhusiano wa Kimataifa &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG];Chuo cha Diplomasia Dar es salaam.
  • Mwaka 2005-2008 alisomea digrii ya Saikolojia, Lugha na Habari katika Chuo Kikuu cha Bangalore-India
  • Mwaka 2009-2010 alisoma digrii ya pili ya utawala (Masters in Public Administration-MPA) katika chuo cha Mzumbe.
NB: Ndugu Nape Nnauye akiwa Kivukoni aliandika "thesis" iliyohusu ; VIKWAZO VINAVYOZUIA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA SIASA. Na pia akiwa Mzumbe University aliandika kuhusu ; SABABU ZINAZOCHANGIA USHIRIKI WA WAPIGAKURA (ni ipi sababu ya kutojitokeza wapigakura siku ya Kura)
Tuwekee na ya Daudi Albert Bashite.
 
HAPO KWENYE RED....BUTIMBA TTC SI CHUO CHA UALIMU JAMAN...AU TUSEME BUTIMBA TTC SECONDARY SCHOOL?..
kajipange upya urudi tena na kiwango cha ufaulu kwa kila level hasa hasa sekondari

Diploma mwaka mmoja then INDIA..hakuna mtu anafeli india elimu inauzwa kama samaki
 
Mbona hivyo kwa nape ambaye hakupata zero yaani fa fa fa fa fa fa fa fa fa, mwambie bashite aweke vyeti kwanza acheni hiizooooo
 
Wangekuwa wauza kama maziwa mngekuwa mnapeleka viongozi was nchi kutibiwa , inawezekana we bashite mamba tatu, diploma mwaka moja niutaratibu mbona digirii ilikuwa miaka 4 sasa mitatu kwa baadhi ya digrii, bashite atupie vyetiiiiii..,............
 
Takataka tupu diploma hata hazieleweki mwaka mmoja mmoja!!
Ndalichako pitia huku uone
Na hapo ndio utamu wa siasa ulipo, unaweza kukutana na ukweli mwingine unaoumiza hapa matokeo yake ukaongeza mapigo! Hivi Koromije si inapatikana jirani na maeneo ya Misungwi pia!?
 
Back
Top Bottom