Hii CV inaonekana ni ya kulazimisha, hakuna ubishi!! Najua Nape kakutuma na sipendi kushindana na wewe ila kuna walakini kwenye maelezo yako!
Mfano, kati ya 1987 na 1989 Nape alianza drs la kwanza. Kwanini usiweke "exactly" mwaka alioanza hilo darasa??
Pili Butimba ni chuo cha ualimu, alisoma cheti au diploma? Kwa muda ulionyesha wa mwaka mmoja pale Butimba, jamaa atakua amesoma cheti na kwa mantiki hiyo matokeo yake ya form six hayakumruhusu kusoma diploma!!
Tatu, umesema alisoma diploma ya diplomasia pale Dar kuanzia 2002-2003, je kuna diploma ya mwaka mmoja?? (lazima amesoma certificate kwa kutumia matokeo ya form four)
My take:
Kwa maelezo yako, Nape ana elimu ya vyeti ila hajaelimika popote, na ndio maana uwezo wake upo chini sana! Nape kafika hapo alipo kutokana na kubebana kulikopo chani ya CCM. Wapo wengi tu kwenye idara nyeti za serikali ambao ni vilaza zaidi ya Nape.!
Kwa kuwa Nape ndie alieanzisha mjadala wa kuchokonoa elimu za watu; angetakiwa aje hapa jukwaani mwenyewe sio kukutuma wewe.
Hili linadhirisha jinsi alivyo kihiyo. Angemjibu Mnyika kwa hoja ingependeza sana! Nape hawezi kushindana na Mnyika hata kwa dawa!! To me Mnyika is the next level before Moses Nape. Huwezi kuwalinganisha hata kidogo. Simshabikii Mnyika, ila nimewa-evaluate wote ndo maana nikaja na hiyo observation.