Hii ndio hali ya Bumbuli ambayo Mbunge wake ni Waziri wa Mambo ya nje ya Nchi

Ni kwa ushahidi upi unaothibitisha picha hiyo ya magari na barabara ni ya Bumbuli na ni ya mwaka huu? Kwani mara ngapi wewe tumekuona na kushuhudia ukibandika picha za zamani na zenye lengo la kudhalilisha watu?
 
yuko busy kumsafirisha raisi nje kwa waislamu for his own selfish interest, western countries hatakiwi na wala haalikwi popote, angalau wakati wa Mulamula walikuwa wanaalikwa western countries sasa lkn sasa hivi ni mwendo wa uturuki au irani …
 
Kati ya Viongozi ambao, Watu hawajui au wamechelewa kujua alivyombabaishaji basi Ni Makamba Jr..
Huyu jamaa kipindi watu wanamtukuza, watu wa Bumbuli hata wazee waliojichokea, huwezi mwambia kuhusu huyu jamaa wakakuelewa, Kiufupi hamna mzigo, hakuna alichofanya kule kwaoo,

Kule hua watu wanajiulizaga, huyu ana nini huko kitaifa kinamfanya akubalikee?, kwa sababu hawana experience yoyote ya maendeleo aliyowaletea ya kujivunia, atasubiri Uchaguzi, aende Maweni pale akamwage Pesa..

Na Bado hamjamjua Makamba Vzr, waulizeni watu wa Bumbuli.
 
πŸ€”Β°Β°Β°Β°Β°Β°Β°Β°Β°Β°Β°Β°Β°Β°Ο€(CHADEMA)* (Mwakala wa Mabeberu)=😌

Siku zote Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe.
 
Ni kwa ushahidi upi unaothibitisha picha hiyo ya magari na barabara ni ya Bumbuli na ni ya mwaka huu? Kwani mara ngapi wewe tumekuona na kushuhudia ukibandika picha za zamani na zenye lengo la kudhalilisha watu?
Dawa ni wewe kutuwekea mkeka wa lami Bumbuli ili tunyamaze na tufunge mdomo , halafu kingine ni hiki , taarifa za Bumbuli siyo mali ya January wala si mali ya ccm na wala siyo mali yako wewe

Uliandika kuhusu Lissu kuhama Chadema huku ukijua umezusha tena bila hata kielelezo , uliona tukipayuka ? tulikupuuza mara moja kwa sababu tunajua wewe ni mjinga
 
Acha porojo .weka ushahidi kuwa hiyo ni barabara ya Bumbuli.maana wewe kwa uongo na kubandika picha za kuokoteza unapenda sana .
 
Tukisema tuandamane Jimbo la Bumbuli, tunapitia wapi sasa,

Ukute kipara anafanya kusudi Ili asifikiwe na nguvu ya mabadiliko πŸ˜€
Ameandamana Mbowe jana, ukafika wakati wa kuuza sera, akaanza kuwachonganisha Watanzania na Wachina-Kwa sababu ya barabara kama hiyo ya Bumbuli?

Kaongea Sifuri nyingi sana hata Kompyuta zisiweze kutarakilisha! Noma sana

...labda, CHADEMA wajenge Barabara zao 2050 ndio CCM waje waandamane.
 
CCM haijawahi kumiliki ofisi,imepora,

Itawezaje kujenga barabara kweli?
 
Kwanza hizo mvua zinazo watandikeni huo kuanza kutupiana lawama za ubovu wa barabara itakuwa ni kuamua kuwa wachawi kwa hiari
 
Kuanzia kazungula, pandamatenga, ngwasha, nata, francis town, palapye, mahalapye, Gaborone, A3 ni super road, kwakweli, Namibia kupitia katima mulilo boda, ni super. Na ni landlocked countries. Sijui tumelogwa wapi Watanzania. Dah inauma sana.
 
Kuanzia kazungula, pandamatenga, ngwasha, nata, francis town, palapye, mahalapye, Gaborone, A3 ni super road, kwakweli, Namibia kupitia katima mulilo boda, ni super. Na ni landlocked countries. Sijui tumelogwa wapi Watanzania. Dah inauma sana.
Ni shida mkuu,na barabara hiyo kuanzia kazungula OSBP hadi Nata ni national park (more than 300km)hukuti matuta ya ajabu,kwetu pale mikumi national park (50km ni vurugu tupu na kwa sasa magari kibao yanapata pacha kwenye like handaki)siku V8 ya wateule itakapoumia pale ndio watakurupuka kuitengeneza
 
Hao wakazi ndio wanaojenga Barabara? Au Serikali huweka miundombinu ili kuchochea maendeleo?
 
Mkuu you are missing the point, si wajibu au jukumu la mbunge kujenga barabara au kupeleka maendeleo jimboni kwake.

Kukukumbusha tu, mbunge huwakilisha maoni ya wanajimbo lake bungeni, kujadili na kupitisha bajeti ya serikali, kutunga sheria na kuisimamia serikali.

Ni kazi ya serikali kupeleka maendeleo majimboni maana ndio wanaokusanya kodi. Kimsingi wakuulizwa ni Mkuu wa wa wilaya, Mkurugenzi, Mkuu wa mkoa, katibu mkuu, Waziri na raisi.
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…