Lushoto ilitakiwa iwe ni Switzerland 🇨🇭 ya Tanzania,nilibahatika kufika kule last December,Mwenyezi Mungu kawapa super wilaya ila wale wabunge wake 3 ni zeros kabisa,yaani hawawezi kujenga hata ile barabara ya mombo to mlalo,yaani barabara ipo vile vile alivyoiacha mjerumani,ilitakiwa ile pass ilambwe vema,jenga cable cars kutoka kule milimani hadi barabara kuu ya Moshi,jenga virukio vya maparachuti,yaani hizi ni vyanzo vya usd tu,vijana wake wamekua vibarua na maisha yao wamejikatia tamaa
EEEeeenHEEEeee. Mkuu 'Nkanini', ni kweli Lushoto ina mandhari ya Kiswiss kama ulivyo eleza; lakini kwa vitu hivyo ulivyotaja hapo, nadhani utakuwa unawaonea bure hao wabunge (siwatetei). Miradi ya namna hiyo ni ya serikali kuu, wizara husika na utalii kwa mfano.
Labda tuseme wabunge hawakuwa wabunifu wa mambo kama hayo uliyoyasema, na kuwa wafuatiliaji wa karibu kuhakikisha serikali inafanya jambo juu yake.
Lakini pia turudi nyuma kidogo. Kila wilaya nchi hii inayo mambo ya kipekee sana ambayo kama yangefuatiliwa wilaya hiyo ingepata manufaa makubwa, na kwa hiyo nchi nzima ingefaidika. Chukulia mfano wa wilaya kama ya Ukerewe.
Hawa wangejikita katika uvuvi wa samaki, na kufuga samaki kisasa, wilaya ile ingekuwa inasambaza samaki wake nchi nzima na hata kuuza nchi za nje. Wabunge wa wilaya ile wangekuwa na nafasi zao za kuhimiza na kusimamia maendeleo hayo ya wananchi wao; lakini mbali na hilo, uwezo wa kuwekeza kwenye shughuli hiyo ingepaswa iiangukie wizara husika.
Hali ni hivyo hivyo kote nchini.
Sasa labda tuseme, maendeleo ni hatua kwa hatua. Lushoto isingekuwa na hao ma'cable' car wakati hata huko kutoka Mombo hadi Mlalo bado ni tatizo.
Nisiandike sana. Hivi mambo kama haya nayo huwekwa kwenye mipango ya maendeleo ya nchi na kupewa muda maalum wa kuyatekleza?
Nakuunga mkono. Lushoto imekaa vizuri sana kwa utalii, na ndiyo maana kule wazungu hawakomi kwenda huko.
Makamba? siyo mtu sahihi wa kuyafanya hayo. Unakumbuka alivyowachomea utambi watangulizi wake?