Hii ndio hali ya Bumbuli ambayo Mbunge wake ni Waziri wa Mambo ya nje ya Nchi

Yule ni mbunge na waziri,

Unaamini anajielewa Kweli na kutimiza ipasavyo majukumu yake?
 
Tuache blah blah mkuu,tuongee facts hapa,mbunge anapofanya kampeni za kuwa mbunge na kuahidi atajenga zahanati hapo Mlalo,means anaongopa!na mtu mwongo ni zaidi ya shetani,mkuu labda nikupe historia ndogo,ukitembelea Magomeni na kinondoni A kuna nyumba zilijengwa kwa sheria za mipango miji chini ya yule mbunge mzungu Bryaston na mpaka leo heshima ile bado ipo kwake,wakaingia hawa wabunge waliojaa uongo na ufisadi waka fa....c...up kila kitu pale,ufipa street,wibu street etc etc mitaa ile inajifunga yenyewe kwa uchafu,pale studio kuna kenge mmoja kaweka kituo cha mafuta kwenye zone ya makazi na wapumbavu wote kimyaa,kule mikocheni wakafeli kisa wanaishi royal families!,with my respect kwako mkuu ninaijua Tanzania na nimebahatika kufika sehemu nyingi tu,wabunge ni waongo
 

Attachments

  • IMG_20240420_081417_680.jpg
    2.3 MB · Views: 4
Aiseeee !!!
 
EEEeeenHEEEeee. Mkuu 'Nkanini', ni kweli Lushoto ina mandhari ya Kiswiss kama ulivyo eleza; lakini kwa vitu hivyo ulivyotaja hapo, nadhani utakuwa unawaonea bure hao wabunge (siwatetei). Miradi ya namna hiyo ni ya serikali kuu, wizara husika na utalii kwa mfano.

Labda tuseme wabunge hawakuwa wabunifu wa mambo kama hayo uliyoyasema, na kuwa wafuatiliaji wa karibu kuhakikisha serikali inafanya jambo juu yake.

Lakini pia turudi nyuma kidogo. Kila wilaya nchi hii inayo mambo ya kipekee sana ambayo kama yangefuatiliwa wilaya hiyo ingepata manufaa makubwa, na kwa hiyo nchi nzima ingefaidika. Chukulia mfano wa wilaya kama ya Ukerewe.

Hawa wangejikita katika uvuvi wa samaki, na kufuga samaki kisasa, wilaya ile ingekuwa inasambaza samaki wake nchi nzima na hata kuuza nchi za nje. Wabunge wa wilaya ile wangekuwa na nafasi zao za kuhimiza na kusimamia maendeleo hayo ya wananchi wao; lakini mbali na hilo, uwezo wa kuwekeza kwenye shughuli hiyo ingepaswa iiangukie wizara husika.

Hali ni hivyo hivyo kote nchini.

Sasa labda tuseme, maendeleo ni hatua kwa hatua. Lushoto isingekuwa na hao ma'cable' car wakati hata huko kutoka Mombo hadi Mlalo bado ni tatizo.
Nisiandike sana. Hivi mambo kama haya nayo huwekwa kwenye mipango ya maendeleo ya nchi na kupewa muda maalum wa kuyatekleza?

Nakuunga mkono. Lushoto imekaa vizuri sana kwa utalii, na ndiyo maana kule wazungu hawakomi kwenda huko.

Makamba? siyo mtu sahihi wa kuyafanya hayo. Unakumbuka alivyowachomea utambi watangulizi wake?
 
Ni wakati wenu Chadema kuchukua jimbo muweke lami!
 
Yule ni mbunge na waziri,

Unaamini anajielewa Kweli na kutimiza ipasavyo majukumu yake?
Mkuu kwanza ungeainisha kwenye bajeti ni kiasi gani kilitengwa kwa ajili ya jimbo lake, then tuone kama alishindwa kwa capacity yake kuisimamia.

Na pia maendeleo ya jimbo hayapimwi kwa kutumia ujenzi wa barabara tu, maendeleo ni muungano wa aspect nyingi Mkuu.
 
Makamba akili hana kabisa, Yeye ni kutegemea uchawi tu, Sasahivi eti nae anataka urais wakati Jimbo tu linamshinda wakati kawa waziri miaka kibao,Sijui watanganyika ninani aliyeturoga?Majitu kama haya hata kwenye mikutano yao upaswi kwenda, lakini utakuta uchaguzi ukikaribia anaanda machawa kibao wa kumnadi kutoka humo kwenye matope.
 
😆😆😆😆
 
Mkuu hapo ni uelewa wa wananchi kuhusu majukumu ya mbunge, kwa kufahamu hilo wabunge wengi wanatumia hilo kuhadaa wananchi.

Mkuu yawezekana wananchi wakawa na uelewa ila wakawa ni waoga wa kuhoji pale wanapoona mbunge anadanganya.
 
Achana na budget,

Ni mbunge Kwa muda Gani?

Upi Hasa ushiriki binafsi wa mbunge kama kiongozi kuhakikisha barabara inakuwa katika Hali nzuri?

Miaka alitokaa bungeni inatosha, apumzishwe aje mwingine.
 
Ukisema watanzania ni wajinga utaambiwa umetukana. Sasa miundombinu unayozungumzia ni kazi ya mbunge kuijenga? Kazi ya mbunge ni kuwasemea wananchi. Je, mlimpa mbunge mawazo/kero/mahitaji yenu akaacha kuyafikisha bungeni? Sasa serikali isipopeleka pesa kutokana na ufinyu wa bajeti au kwa maamuzi ya kibaguzi (kama jiwe lilivyosema ukichagua mpinzani sahau maendeleo), mbunge analaumiwa vipi?
 
Ujinga sio tusi wala upumbavu pia (pitia kamusi ya kiswahili),nimekuelewa na sasa utakubaliana Nami kuwa mbunge mtarajiwa anapoahidi kuwa atajenga ile pass ya mombo to mlalo ikiwa atapewa kura kuwa huu ni uongo?,na ubunge wake unaweza kuwa batili maana ametumia mbinu za uongo kupata kura,mkuu bottom line Lushoto kupo super,Mola kawapa kila kitu ILA wamekosa viongozi wenye uchungu na wilaya yao
 
Nilipita huko km miaka 3 iliopita maeneo hayo mawasiliano yalikata toka njia panda mpk Lushoto mjini njia zilizibwa na maporomoko,tukaenda huko vijijini kulichotusaidia ni kua na toyota cruiser kule kupanda ndio shida kipindi hiki ilakushuka matope yanakupa lift ila mwenyewe ukimkuta mjini hata nia ya kujenga zege gumu hana analiga kasia mchi kwa nchi
 
Hayo ma bila kupingwa yao ni mamilungula inafahamika.

Safari hii lazima apitishwe kwenye tanuri la moto.

Lakini hawa wana mbinu chafu nyingi, wanafukuza watia nia kwa dau kubwa na mizengwe mingine ovu, hadi anahakikisha kabakia peke yake.

Halafu siku ya kura, mnampigia yeye na kivuli.

Na siku hiyo unakuta kapandikiza vidomo kaya mamluki yake vituoni, utasikia.. 'Hiri rikijana rinakubarika sana si unaona harina wa kuripinga' ni chaguo la mungu...
 
Je January alipeleka kero za wananchi Bungeni ? ukisoma pale juu kabisa aliitisha wananchi watoe kero
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…