Hii ndio imani pekee kila jamii duniani inaamini

Hii ndio imani pekee kila jamii duniani inaamini

Maghayo

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2014
Posts
20,307
Reaction score
47,210
Mzuka wanajamvi!

Kila jamii duniani inaamini vitu flani hasi ama chanya.

Kwa mfano hapa Tanzania kuna watu ukiwapa pesa kwa mkono wa kushoto hawakubali, kujitawadha kwa mkono wa kulia siyo sahihi, kwenda dukani usiku kununua chumvi unatakiwa kuita dawa ya mboga, kufagia usiku siyo sahihi unafukuza baraka, kuwashwa washwa na kiganja hela inakutembelea n.k.

Lakini hii hapa ndo imani inayoaminiwa na kila jamiii duniani kwa anzia Argentina south America hadi north pole green land. Toka Misri hadi South Africa. Ulaya yote Asia yote, uarabuni kote, Australia hadi visiwa vya Pacific marekani kote.

NI KUPIGA MLUZI USIKU. Kila jamii duniani wanaamini kupiga mluzi usiku haitakiwi.
 
Yote ya yote kuwashwa kiganja cha mkono asilimia mia moja unapata hela.
 
Ukipiga inakuaje kwani?
Unaiita Demons. Calling demons. Nilikuwa na demu flani wa Estonia nikawa napiga mluzi usiku akamaind. Nikashangaa nikamuuliza kumbe hata nyie mnaamini hivyo?

Ikabidi niingie chimbo kufanya utafiti. Nikamuuliza Bangladeshi akasema hivyo hivyo siyo sahihi, nikawauliza wasomali, Senegalese, chechens, waethiopia, Egyptian, Filipino, thais, Syrians, iraqis, Iranians majibu ya kawa hivyo hivyo. Hawa ni jamii tunachanyikana mara kwa mara.

Nikashangaa hadi wateule wanaamini hivyo.

Ila nilivyokuwa natafiti kwa kusoma wateule na majirani zao waarabu wametofautiana hii imani bundi ni muovu. Wateule wanawapenda bundi kwasababu wanaua jamii ya panya rodents mashambani wakati wa mavuno nafaka na hii ni karne na karne.

Hawaamini bundi ni muovu. Lakini hawa bundi wakiruka kwa upande wa waarabu Syria, Lebanon, misri na palestina wanauliwa sana. Lakini kwa wateule hawauwawi karne na karne.

Wateule na jamii chache duniani wanaamini bundi siyo muovu.
 
Yote ya yote kuwashwa kiganja cha mkono asilimia mia moja unapata hela.
Hii siamini. Nilisoma sehemu nilicheka nusura nife. Kuna jamaa dokta India amsema hamna kitu kama hicho. Anadai ukiwa na kisukari ama presha viganja, nyayo na toes zina washa washa kwasababu blood circulation inachukua muda kufika hizo sehemu.

Kwa iyo akawahasa wahindi waache hizo imani eti hela itakutembelea wakati ni nerve damage.

Nilicheka sana.
 
Kuna mganga anakuchanja chale, akianza kupaka dawa kabla ya kuanza manuizi anapiga mruzi, hapo ni usiku.

yule mzee ana manuizi makali sana. " Yeyote atakayejaribu kumrushia uchawi wa aina yoyote huyu....umrudie na afe kifo cha kutokwa damu mdomoni, masikioni na mkunduni"

hapo familia yote inasikia na anakuwa anarudia rudia mara kadha hiyo sentensi
 
Back
Top Bottom