Hii ndio inaitwa kuupiga mwingi, gharama za bando zimepanda tena

Hakuna kitu hakijapanda bei. Wakulima wamepandisha bei ya mazao yao

Wakulima wamepandisha bei ya bidhaa zao

Wafanyakazi mishahara imepanda.

Ngoma droo. Sasa kelele za nn?
Mie saluni nanyoa kwa bei Ile ile
 
kaka huku kwangu Tsh 10000 = MB 3072 (YAANI SAWASAWA NA GB 3, AMBAZO NILIKUWA NANUNUA KWA 5000)

AISEE
 
Kifurushi cha wiki kinaisha ndani ya nusu saa, TCRA na FCC wamenyamaza tu.
Hawa wapo kama ukimsema vibaya mwenye mamlaka husika, au kuwachana ukweli ndo wanafanya kazi haswa.

Kesi ya kkfurushi na ushahidi upo unakulazimisha ufuatilie miezi na miezi
 

Tumia jimixie bundle unaipata kwa *149*01# kisha unachagua number 2 kisha jimixie unachagua unachotaka mimi natumia hivyo toka March.
 
Wale wazee wa kusifia waendelee kusifia siku tukiacha kusifia tayari kila mtu atakuwa ametoka nundu na ndio tutajua li nchi hili limekosa uongozi thabiti usiojali watu maskini,na walishiba kamwe hawawezi kuwathamini wenye njaa iwe ni kanisani au msikitini kote huko wako kimya sio mapadri,wachungaji mashehe na maaskofu wote hatusikii wakisema chochote ila watanzania kiujumla tunateseka sana maisha yamepanda isivyo kawaida Uholela umekithiri kila mtu ni mtaalamu wa kupandisha bei za bidhaa ndani ya Tanzania Taasisi husika zimebaki ni picha tu black and white.hakuna kitu.
 
Kuna kipindi bei ya unga wa ugali ilipanda balaa..sio sahihi kusema vitu havikupanda bei.

Hawakumbuki kipindi cha 8MB aka MB nane, au wameanza kutumia internet juzi. Bei huwa zina badilika na kuna kampuni nyingi ukiona hii haikufai hamia nyingine
 
Nipo Malawi waliniuzia 8GB kwa 4000Mk haifiki hata 8000 tsh haifiki na data zisimi naangalia mechi nyingi live naona ntavuka na data za kumwaga hawa jamaa airtel yao mtandao upo faster na gharama sio kama za majambazi ya bongo muda wote watu wanazima data hapa nikitaka kuwatafuta watu wengi inabidi umpigie ambae uba uhakika hazimi data ndio ampigie huyo mzalendo uongee nae hayo makampuni yanatuibia mno mno...data nayo ni hatari kama mafuta tuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…