HII NDIO KANUNI BORA YA KIJASUSI YA KUISHI NA MNAFIKI YOYOTE DUNIANI 😊

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
HII NDIO KANUNI BORA YA KIJASUSI YA KUISHI NA MNAFIKI YOYOTE DUNIANI 😊

Kijasusi jitahidi uwafahamu watu kabla ya wao kukufahamu, na hapo ndipo utagundua WANAFIKI NA WASIO WANAFIKI.

DALILI ZA MNAFIKI

1.Kwanza atajifanya mwema sana kwako
2 Atajifanya kuumia sana dhidi ya wanaokusema mabaya kumbe moyoni anafurahia
3 Atakuweka kwenye mazingira ukosee kisha akupe pole kumbe anafurahia na kukutangaza
4 Muda mwingi akiwa nawe anakupa habari za watu wengine.


FANYA HAYA UKISHAMJUA KUWA NI MNAFIKI.

1.Usimwambie kwanza kuwa umeshamjua.
2 .Hakikisha humpi habari zako ambazo zikifahamika kwingine italeta shida
3 Mtumie kama barua ya taarifa kujua watu wengine
4 Ukimaliza kumtumia kama chanzo cha taarifa anza kumkwepa taratibu.
5 .Hakikisha unafiki wake unakunufaisha kwanza ndio uonyeshe dalili za kumkwepa

#Instagram@ fikia ndoto zako
 
Namba 4 ndo Kila kitu

Kila akikaa na wewe ni kupondea watu wengine utafikiri yeye Hana mabaya
 
Wanafki ni kuchinjia baharini mazima
Fukuzilia mbali, unavyoendelea kumlea ndio kifo chako unavyozidi kukisogeza.!
Mimi nikijua mtu mnafiki namkimbiza silei wanafiki hawana tofauti na wauaji
 
Mtu kashakuwa mnafiki unampa nafasi nyingine ya nini?
Kikubwa kwanza kumtambua halafu kumtumia,,shida ni kama hujamtambua na akawa anakutumia wewe,, haya mambo ni timing,,,,hawa wazuri sana kupata taarifa za mahasimu flani ila hakikisha tu zako zile za kukumaliza humpatii maana ataenda kukukaanga kwa wengine akijua ulikua unamtumia
 
Fukuzilia mbali, unavyoendelea kumlea ndio kifo chako unavyozidi kukisogeza.!
Mimi nikijua mtu mnafiki namkimbiza silei wanafiki hawana tofauti na wauaji
We mtu muda wote anafanya kazi kuwapondea wengine

Unaanza kuwaza sa kama anawapondea wengine wakiwa hawapo vipi na mimi nikiwa sipo

Nipo salama kweli!?
 
Ukimjua mnafiki usimpe nafasi ya kumsikiliza atakuangamiza
 
Mhhh,kumbe. Ngoja nijaribu kuzifuata hizo kanuni
 
Kutaka kufahamu mambo ya wengine kupitia mnafiki ni umbea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…