Hii ndio orodha ya Miji na Wilaya za Tanzania zenye watu wenye kipato cha Uhakika

Mapato ya halmashauri hayadecide purchasing power ya eneo husika..

Mapato ya TRA ndiyo yanadecide..
Huo ndio uongo sasa,Mengi ya mapato ya Halmashauri ni shughuli za uchumi za moja kwa moja za wananchi unlike kwenye TRA ambako asilimia kubwa ni kodi ya biashara kubwa na corporate

Sasa kwa mantiki hiyo ni wazi nature ya mapato ya Halmashauri yanatoa picha halisi ya uchumi wa mtu mmja mmja na purchasing power ya watu.

Hata hivyo ukija pia kwenye makusanyo ya TRA still hizo Halmashauri zita feature kwenye list kama kawaida
 
Mufindi kuko vizuri sana mkuu, sema tu marehemu alivuruga mambo mengi sana. Miti saa hizi imeshuka bei hivyo wajanja hawavuni wanasubiri bei ipande juu tena.
Sio tuu Mufindi bali Iringa na Njombe kwa ujumla wake hususani wilaya za Mufindi,Kilolo na Njombe.

Hao wanalima miti na Mazao ya miti,chai,pareto,matunda anuai na Mazao ya chakula kama viazi mviringo.

Njombe na Kilolo ni game changer unlike Mufindi imekuwa hivyo miaka mingi.Mathalani kwenye Takwimu za mapato mwaka 2020/21 hadi february Njombe TC ilishaweka kibindoni 5 bln ikiwa na miezi 4 bado so by 30 June watafikisha mark ya zaidi ya bil.6 au saba,come next year nitakuja na data husika.

Ni swala la Muda tuu Njombe na Kilolo kuizidi Mufindi maana tatizo lilikuwa miundombinu hasa Kilolo ni moja ya wilaya fertile Sana na sehemu kubwa ya Eneo ni virgin

Serikali ingekuwa sikivu ingefungua barabara kwa lami kutoka Iringa Kilolo hadi Ifakara,ile barabara ni muhimu sana kiuchumi
 
Muleba imeizid bukoba mjini yenye bandari na viwanda na viwanja vya ndege naomba nielimishwe kidogo.

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Nafikiri Muleba ina eneo kubwa Kama wilaya na hivyo kuwa na vyanzo vingi. Asilimia kubwa ya visiwa vya ziwa Victoria vilivyopo mkoa kagera viko ndani ya Muleba hivyo pesa kutokana na uvuvi ni kubwa, kilimo hasa kahawa, ndizi, vanilla, n.k
 
Sasa nimeelewa why Magufuli alivunja iliyokuwa halmashauri ya jiji.Maana nimeona Ilala MC,Temeke MC,Kinondoni MC halafu tena DSM CC.Sasa sijui Hilo eneo la Dar lipo wapi
 
Kwahiyo watu wa Tanga City wana maisha mazuri kuliko wa Moshi MC au Iringa MC??

Unataka kusema Tandahimba wanaishi au wana maisha mazuri kuliko Hai, Masasi, Songea, Njombe??
 
Iweke hapa tuone mkuu
Magufuli alipiga marufuku kutoa takwimu za mikoa baada ya kuona watu tunarefer tunachokichangia kwenye pato la taifa then haturudishiwi chochote..

Kwa kifupi tu ukiangalia data za TRA wakati wanaweka collections za mikoa, ya Kwanza ni Dar, Arusha inafata Kilimanjaro ndio Mwanza. Yaani Mwanza ilikuwa inazidiwa mpaka na Kilimanjaro. Last time walikuwa wakiweka hivyo ni 2018 au 2017 sina kumbukumbu nzuri..

Ngoja nikatafute then nirudi hapa kama bado zitakuwapo..
 
Sio lazima Korosho mkuu pia huko kuna madini na hardwood timbers na Mazao mengine
Unaongea na mtu ambaye huko kote nacheza.. Tena huwa siishii mjini tu, napita mpaka vijijini kwahiyo hali halisi naijua..

Huwezi kuiweka Tunduru mbele ya Masasi au Nachingwea kwa hali yeyote ile..
 
Kula milo mitatu kwa siku ni Food Abuse
 
Sio lazima Korosho mkuu pia huko kuna madini na hardwood timbers na Mazao mengine
Pitia hizi data za TRA mwaka 2019..

Kilimanjaro iko nyuma ya Arusha na Dar peke yake kwenye almost kila collection
 

Attachments

Sasa nimeelewa why Magufuli alivunja iliyokuwa halmashauri ya jiji.Maana nimeona Ilala MC,Temeke MC,Kinondoni MC halafu tena DSM CC.Sasa sijui Hilo eneo la Dar lipo wapi
Alivunja mwaka huu kwa hiyo mwakani hutaiona hiyo dsm cc
 
Pitia hizi data za TRA mwaka 2019..

Kilimanjaro iko nyuma ya Arusha na Dar peke yake kwenye almost kila collection
Hao nao wawe Wana update data yaani tuko 2020/21 bado wanaleta Takwimu za 2018/19 tena zinaishia kota ya tatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…