Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,034
- 6,913
- Thread starter
- #21
Taarifa ndio hiyo kwenye pdf kama ilovyowekwa na SerikaliNaomba taarifa hii nzima kama unayo. Taarifa hii inaweza kutoa direction ya fursa ya uwekezaji.
Ukiacha mkoa wa DSM na majiji ambao vyanzo vyao vinatokana na uchumi wenye mjumuiko wa vitu vingi mikoa mingine ina kitu ambacho data hizo hazijakiweka wazi.
Nimeona Iringa na Njombe, halmashauri zao zinafanya vizuri sana. Na line ya Wilaya zote kutoka Iringa hadi Tunduma zinafanya vizuri sana. Nini kipo nyuma ya mapato hayo?
Nimeangalia baadhi ya sehemu Halmashauri za Wilaya zimefanya vizuri kuliko Manispaa husika. Natamani kujua chanzo cha mapato hayo, mfano Muleba DC imefanya vizuri kuliko Bukoba MC, Kilwa DC kuliko Lindi MC, etc.
Zipo baadhi ya sehemu kama Kahama, Geita TC, Tarime DC sababu ni madini. Halmashauri za Pwani kuna viwanda, hao wengine nini kimewabeba?
Kama ni kilimo tujue ni kilimo kipi kusaidia wananchi wajue walime nini. Pili kama ni kwa sababu ya structure ya kodi/tozo/ushuru kwenye mazao fulani ni vema liwe wazi pia.
Kuna Halmashauri zingine zina Eneo kubwa na vimiji au vijiji vilivyochangamka kibiashara kwa hiyo vinakuwa na fursa nyingi kimapato kigen their population.
Pili kuna Halmashauri zina Mazao ya kilimo ya biashara na chakula ambayo yanauzwa sehemu nyingi za nchi na Dunia kwa mfano Mbozi(kahawa),Njombe(Miti,chai,parachichi), Mjinga (kahawa)Tunduru (Korosho),Kilwa (Mazao ya samaki nk)Muleba (Kahawa)
Halmashauri za ukanda wa Iringa hadi Tunduma ni mambo ya kilimo cha Mazao ya biashara,kilimo,viwanda vidogo na biashara maana ziko kwenye ukanda wa njia kuu ya kwenda nchi za Kusini mwa Afrika.
Mikoa ya Nyanda za Juu shughuli kubwa ni kilimo biashara cha Mazao ya chakula na biashara,miti,viwanda vidogo na biashara.
Ni mpaka uingie Tamisemi uchambue Halmashauri moja baada ya nyingine ndio utapata picha kamili shughuli za kiuchumi zilizoko Eneo husika