Hii ndio orodha ya Miji na Wilaya za Tanzania zenye watu wenye kipato cha Uhakika

Taarifa ndio hiyo kwenye pdf kama ilovyowekwa na Serikali

Kuna Halmashauri zingine zina Eneo kubwa na vimiji au vijiji vilivyochangamka kibiashara kwa hiyo vinakuwa na fursa nyingi kimapato kigen their population.

Pili kuna Halmashauri zina Mazao ya kilimo ya biashara na chakula ambayo yanauzwa sehemu nyingi za nchi na Dunia kwa mfano Mbozi(kahawa),Njombe(Miti,chai,parachichi), Mjinga (kahawa)Tunduru (Korosho),Kilwa (Mazao ya samaki nk)Muleba (Kahawa)

Halmashauri za ukanda wa Iringa hadi Tunduma ni mambo ya kilimo cha Mazao ya biashara,kilimo,viwanda vidogo na biashara maana ziko kwenye ukanda wa njia kuu ya kwenda nchi za Kusini mwa Afrika.

Mikoa ya Nyanda za Juu shughuli kubwa ni kilimo biashara cha Mazao ya chakula na biashara,miti,viwanda vidogo na biashara.

Ni mpaka uingie Tamisemi uchambue Halmashauri moja baada ya nyingine ndio utapata picha kamili shughuli za kiuchumi zilizoko Eneo husika
 
Ndugu zangu wa Singida wanazembea somewhere. Wangetumia fursa ya uadimu wa mafua kulima alizeti, wangetoka. Wizara ya kilimo ikapige kambi Singida ku boost kilimo cha alizeti.
Kweli mkuu maana inashangaza hadi Singida Manispaa ni hamna kitu
 
Dodoma Imeingiaje?
Waulize Tamisemi but hiyo Dodoma usiichukulie simpo kuna uwekezaji mkubwa unaendelea kule,juzi tuu nimeona kampuni kubwa ya Burundi wanawekeza kiwanda cha kutengeneza mbolea zaidi ya dola mil.400 hapo unazungumzia trioni moja,usisahau kiwanda cha kusafisha dhahabu na miradi mingi inayoendelea pale

Tena hayo mapato ya Dom yameshuka walipouza viwanja walifikosha bil.73
 
Iringa ipo vizuri mno,ukijumlisha Hizo sehemu zake ukiachana njombe nadhani ilitakiwa kuwa ya 3 katika hiyo orodha ,hongereni sana wana wa iringa,kazi iendeleeeeee
Mkuu ya tatu kivipi mimi nimetoa vigezo vya Mji/Halmashauri sio kimkoa,hata hivyo pdf hapo chini imetoa summary ya kimkoa
 
Sasa mkuu umeweka halmashauri yangu akati nikijicheki mfukoni kuna masalia ya maganda ya karanga tu?[emoji16] halmashauri nyingi znabebwa na uwepo wa natajiri wakubwa tu, unaweza kukuta hiyo kodi ni ya watu wachache sana.
Hiyo ni personal issue iko nje ya uwezo wangu,hizo pesa wamelipa watu ko na wewe fanya wanachofanya utapata pesa
 
Muleba imeizid bukoba mjini yenye bandari na viwanda na viwanja vya ndege naomba nielimishwe kidogo.

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Unaweza kuta mengi ya mapato ya Bukoba ni yale ambayo TRA wanakusanya ,tafuta regional statistics za TRA unaweza kuta Kagera iko vizuri

Lakini kwa mapato ya mtu mmja mmja na vyanzo ambavyo Tamisemi inasimamia basi huo ndio ukweli kwamba mna pesa kiduchu hapo Manispaa uchwara ya Bukoba,TRA hiyo hapo check kama mpo
 

Attachments

Nimekupata mkuu

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Lakini Makambako tunakosaje hapo?
Njombe wameigawa hovyo hovyo kieneo Halmashauri za Wilaya ya Njombe Vijijini,wangin'gombe na Makambako zina eneo dogo sana Kama Makambako wangekuwa na Njombe Vijijjini wangeingia.

Hata hao Njombe TC wameingia kwa kuwa wana eneo kubwa sana la kiutawala ambalo ni zaidi ya KM 100 kutoka mjini.

By the way Mkoa wenu wa Njombe bado unaongoza kwa kipato cha MTU Moja moja kwa Tanzania ukitoa Mkoa wa Dar es Salaam na Kilimanjaro.
 
Uzi wa maana sana kwa wenye kujua ya maana. Kudos mkuu.

Wenye kutu ya SIASA vichwani mwao huu uzi hautakuwa na msaada kwao...sana sana wataishia kuuharibu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…