Hii ndio orodha ya Miji na Wilaya za Tanzania zenye watu wenye kipato cha Uhakika

Hii ndio orodha ya Miji na Wilaya za Tanzania zenye watu wenye kipato cha Uhakika

Unaongea na mtu ambaye huko kote nacheza.. Tena huwa siishii mjini tu, napita mpaka vijijini kwahiyo hali halisi naijua..

Huwezi kuiweka Tunduru mbele ya Masasi au Nachingwea kwa hali yeyote ile..
Tupe basi mkuu vyanzo vya mapato vinatoka wapi huko Tunduru?

Pengine na ukubwa wa Wilaya unachangia lakini pia mapato ya hifadhi
 
Tupe basi mkuu vyanzo vya mapato vinatoka wapi huko Tunduru?

Pengine na ukubwa wa Wilaya unachangia lakini pia mapato ya hifadhi
Gemstones na mazao ya biashara kama Ufuta na Korosho kiasi..

Kwenye madini wengi ni wageni, wenyeji hujishughilisha na kilimo..

Ila hapo kwenye list yako sijaiona Tunduru ngoja nikaiangalie

(Okay nimeona wako 27, wana madini ya vito, labda ndio yanawabeba sana)
 
Kwahiyo watu wa Tanga City wana maisha mazuri kuliko wa Moshi MC au Iringa MC??

Unataka kusema Tandahimba wanaishi au wana maisha mazuri kuliko Hai, Masasi, Songea, Njombe??
Pengine hali zinabadilika maana kwa miaka iliyopita hizo wilaya hazikuwemo kwenye Halmashauri zenye mapato mengi but kadiri mda unavyoenda mabadiliko yanatokea

Na hakika kwamba kwa sasa maisha ni better off kuliko hapo zamani na kuifikia Wilaya za Moshi itachukua mda but with new economic muscles watafika ni suala la mda sio la overnight.

Kumbuka hayo mapato wanakusanya na kutumia wenyewe tofauti na huko kwingine ambako wanategemea zaidi Ruzuku ya serikali kuu.

Nikupe mfano ukiingia kwenye bajeti za Halmashauri utakuta wanaopata pesa nyingi wameweka miradi mingi zaidi on top ya ile ya kutoka serikali kuu,eg.Kahama MC wanajenga hospital ya Wilaya kwa pesa za ndani,Dom CC wanajenga hoteli kwa pesa za ndani ,na trend iko hivyo kwenye Halmashauri zingine zenye uwezo wa makusanyo ni ishu ya vipaombele tuu.

Pia Manispaa nyingi za Dar zinajenga barabara zao kwa kupeleka pesa Tarura nje ya bajeti ya kawaida kutoka serikali kuu.Kwa hiyo boss mda utaleta majibu mazuri
 
Gemstones na mazao ya biashara kama Ufuta na Korosho kiasi..

Kwenye madini wengi ni wageni, wenyeji hujishughilisha na kilimo..

Ila hapo kwenye list yako sijaiona Tunduru ngoja nikaiangalie

(Okay nimeona wako 27, wana madini ya vito, labda ndio yanawabeba sana)
Okay kwenye germstones huwa naona wafanyabiashara wanaenda Sana huko

Mkuu uwe unasoma kabla ya kuchangia, Tunduru DC ipo no.27
 
Muleba imeizid bukoba mjini yenye bandari na viwanda na viwanja vya ndege naomba nielimishwe kidogo.

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Uvuvi
Mimi mwenyew nashangaa.
Hadi wilaya ya misenyi yenye viwanda kama kagera sugar,kilimo cha vanilla,mpaka wa mutukula na Ranchi kibao inazidiwa na wilaya ya muleba iliyojaa migomba na kahawa
Uvuvi wa visiwan ndo unaibeba sn Muleba
 
Nataka za current hizo nimeziona ndo maana nikauliza kwa nini wasiweke hadi za mwaka wa fedha 2020/21? Historia sio dili kwa sasa tunataka tuone matokeo ya jasho letu.
Ndio sasa tuombe ziwekwe..

Na kutowekwa lazima ni maelekezo kutoka juu au data zilikuwa zikipikwa..
 
Ngoja bandari ijengwe.
Pesa itakuwepo Huku.
Utalii wenyewe Corona imezingua
Bagamoyo bado sanaa
Bagamoyo imekuwaje tena? Hakuna mkwanja kivipi yaani?
1. Utalii
2. Uvuvi/Samaki
3. Kilimo
4. Viwanda
5. Ukaribu na Dar es salaam
6. Hoteli
7. Heritage site(s) - UNICEF

What is not happening???
 
Ifuatayo ni orodha ya Miji na Halmashauri 41 pekee kati ya Halmashauri 165 Tanzania ambazo watu wake Wana kipato cha Uhakika na kuwa na purchasing power inayotoa fursa ya uhakika wa biashara kwa Tanzania.
Orodha imehusisha Halmashauri zenye mapato yanayoanzia shilingi za Tanzania bilioni 3.5 kwenda juu.

Orodha hii imetokana na makusanyo ya ndani ya kila Halmashauri kiutoka kwenye vyanzo vya mapato vya Halmashauri ambavyo ni shughuli za kawaida za wananchi kutoka Tamisemi kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Mapato hayo ni nje ya vyanzo vinavyokusanywa na TRA na wakala zingine za.serikali.

Kama wewe ni mfanyabiashara hii itakuwa picha halisi ya uchaguzi wa sehemu ya kuwekeza.

1.Ilala MC=58.6bln

2.Dodoma CC=53.2bln

3.Kinondoni MC=44.5bln

4.Temeke MC=34.4bln

5.Arusha City=19.2bln

6.Ubungo MC=17.9bln

7.Mbeya City=13.0bln

8.Tanga City=12.8bln

9.Mwanza CC=12.2bln

10.DSM CC=11.4bln

11.Ilemela MC=10.2bln

12.Geita TC=9.2bln.

13.Morogoro MC=7.5bln

14.Kahama MC=7.12bln

15.Chalinze DC=7.1bln

16.Mkuranga DC=6.6bln

17.Kigamboni MC=6.4bln

18.Mufindi DC=6.1bln

19.Moshi MC=5.7bln

20.Iringa MC=5.62bln

21.Njombe TC=5.6bln

22.Tunduma TC=5.4bln

23.Tarime DC=5.2bln

24.Kilolo DC=5.0bln

25.Mtwara MC=4.8bln

26.Mafinga TC=4.7bln

27.Tunduru DC=4.7bln

28.Muleba DC=4.61bln

29.Kilwa DC=4.6bln

30.Geita DC=4.5bln

31.Arusha DC=4.01bln.

32.Mlimba DC=4.0bln

33.Mbozi DC=3.97bln

34.Tandahimba DC=3.92bln

35.Mbarali DC=3.9bln

36.Rungwe DC=3.89bln

37.Kilosa DC=3.8bln

37.Mbeya DC=3.8bln

38.Mbinga DC=3.65bln

39.Chato DC=3.64bln

40.Kibaha TC.3.62bln

41.Chunya DC=3.5bln

My take kuna Mikoa/Miji ni ya kuonea huruma mfano Tabora,Singida,Rukwa,Katavi,Kigoma,Simiyu na Manyara.Hii mikoa haina hata Halmashauri moja yenye mapato kwa kiwango cha kuanzia bilioni 3.5 au zaidi

Kiufupi inatoa picha ya hali mbaya ya umaskini wa kipato kwa wananchi wake.Hali kadharika Mikoa ya Dar, Mbeya,Geita na Iringa ina hali nzuri ya kimapato kwa watu wake.

Pdf ya Tamisemi hii hapa [emoji116][emoji116] unaweza kujionea mwenyewe

View attachment 1764113
Kweli kuna mikoa hali zao ni mbaya sana
 
Mkoa wa Iringa inaonekana kuna hela sana, hasa Wilaya ya Mufindi.
Huku twina mapesa wuhulo kiba na hatuzitumii tumezitunza tu MUCOBA nakata nguzo za mlingoti nauza zinachipua baada ya miezi 24 nakata tena zinachipua tuna migodi isihokauka huku labda muache kujenga ndo tutakuwa masikini. WanaMufindi hoiyee
 
AISEEH KUMBE RUNGWE TUPO

xema hii haishagazwi sana coZ kuna vitu vingi vinaingza mapato kwenye wilaya hii mfano viwanda vya Chai. Viwanda vya maziwa (ASAS). Viwanda vya parachichi .....pia mazao ya kahawa n.k
 
Wachaga wengi wameenda shule ila nashindwa kuelewa ule ujinga wanaofanya wa kupoteza rasilimali nyingi kujenga majumba vijijini kwa ajili ya 'pride' ambayo muda mwingi wanaishi popo ukiacha zile week mbili za mwisho wa mwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hebu ficha upumbavu wako mkuu.
Kujenga nyumbani sio ufahari ni kukumbuka, kuenzi na kurudisha fadhila mahali ulipozaliwa na kukulia.
Pia inaepusha zile aibu hasa panapo tokea msiba au sherehe itakayo fanyikia nyumbani na kuhusisha ndugu, jamaa na marafiki kutoka mjini halafu wakute nyumbani pako hovyohovyo hali ya kuwa huku mjini uko vyema.
 
Back
Top Bottom