Mbowe kidume....Angalau kazi yao sasa inaonekana. Polisi ni rafiki wa Raia mwema na adui kwa mhalifu.
Safi sanaNjombe, Tanzania
KAZI YA KIONGOZI NI KUSHUGHULIKA NA MATATZO YA WATU - Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa Mh. Peter Msigwa
Katika hotuba yake Mchg. Peter Msigwa alaumu serikali kupuuza maendeleo ya watu katika maeneo nyeti huku vigogo wa serikali wakitumbua kodi za wananchi kwa matumizi ya anasa mfano magari ya kifahari ya gharama za kufa mtu kama VX8 huku kinamama wajawazito wanalazimika kulipia Tshs. 300,000 wanapokwenda kujifungua pia hakuna huduma za maji katika maeneo ya makaazi ....
HaswaaaMbowe kidume....
Asnte san BagamoyoCHADEMA KIJIJINI MNANILA BUHIGWE KIGOMA OPERESHENI 255
Wananchi mamia wa kijiji cha Mnanila washika vifua vyao na kusema Mbowe we love You, we missed You kwa kipindi cha miaka 6 ....
Operesheni hiyo kali ya kisiasa ya siku 4 mkoani Kigoma leo imepita Kasulu Mjini
, Muyama kwenda hadi Munzese na kuishia Mungonya ambapo CHADEMA inaongea na wananchi wa majimbo ya mkoa wa Kigoma kutoa elimu ya uraia na kuimarisha chama.
Mwenyekiti Freeman Mbowe awaelezea wananchi wa Kasulu na Kigoma kuwa chama cha siasa kikiwa hakijengi mazingira ya kuwepo Maendeleo ya Watu katika biashara, ukulima, ufugaji n.k wakiache na kuchagua CHADEMA ili wawe huru kukihoji inapokengeuka kwani chama dola kongwe CCM hakiamini katika uhuru huo...
HIi 255 imezaa matunda sanaCHADEMA - KIINGEREZA NA TEKNOLOJIA NI LAZIMA KWA SHULE ZOTE ZA SERIKALI ILI VIJANA WAPATE UFUNGUO WA MAISHA
CHADEMA leo tarehe 21 May 2023 wamehitimisha ziara yao ndefu ya kila jimbo ndani ya mkoa wa Kigoma katika Operesheni 255 iliyo ingia mpaka ngazi ya vijiji pia tarafa kupitia mikutano ya hadhara kutoa elimu ya uraia kuhusu Haki, Uhuru, Demokrasia na Maendeleo ya Watu.
Ziara hii ya mafanikio makubwa sasa itahamia mkoa mwingine Tanzania bara.
Muhila kabisa apoKasulu, Kigoma
Tanzania
MKUTANO WA CHADEMA WA OPERASHENI 255, KTK KATA YA KITANGA KASULU VIJIJINI
Mamia ya wananchi wa kata ya Kitanga wajitokeza kwa wingi kumsikiliza Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Mh. Freeman Mbowe
Kitanga ni kata ya Wilaya ya Kasulu Vijijini katika Mkoa wa Kigoma nchini Tanzania. Wenyeji wa kata hiyo shughuli yao kubwa za kiuchumi zimejikita katika sekta ya Kilimo na Ufugaji .
Changamoto nyingine mbali ya ktk kilimo na ufugaji , ni miundo mbinu ya barabara kutoka vijiji vya Makere, Kitanga, Asante Nyerere, Kigabye, Kalela, Kwaga, Rusesa, Muzye, Bugaga na Kagerankanda n.k kwenda Kibondo ni barabara ambayo inasimamiwa na TANROADS, Mkoa wa Kigoma. Kuna changamoto katika Daraja hili la Mto Malagarasi, eneo hili ndiyo wananchi wa Kitanga wanapata shida kuvuka kwenda Kibondo.
Kabla mwenyekiti wa CHADEMA hajahutubia, wananchi walipewa fursa ya wazi kutoa dukuduku lao kuhusu mambo mbalimbali mbele ya umma uliofurika katika Ziara ya kikazi ya Operesheni 255 ya CHADEMA nchini kote .