Hii ndio picha bora ya wiki nchini Tanzania, imepigwa Kigoma

Hii ndio picha bora ya wiki nchini Tanzania, imepigwa Kigoma

19 May2023
Kibondo, Tanzania

UBAGUZI WA ELIMU HAUKUBALIKI, ENZI ZA CCM YA NYERERE KULIKUWA HAKUNA MATABAKA YA SHULE



Mwenyekiti wa chama cha Democrasia n a Maendeleo (CHADEMA) Freeman mbowe amesema ikiwa chama hicho kitashika dola ya kuongoza nchi, Miongoni mwa mambo muhimu watakayofanya ni pamoja na kuruhusu demokrasia.

Ni katika mwendelezo wa Operation +255 katiba mpya unaoendelea huko kibondo Mkoani Kigoma nchini Tanzania, na akiwa ameshikilia hoja ya Elimu hasa kwa wananchi wa kigoma, mbowe alihoji ikiwa wananchi hao wanaendelea kukitetea chama hicho na huku chma hakitambui mchango wao ..

Mwenyekiti Freeman Mbowe anakumbuka enzi za Mwl. Nyerere watoto wa Nyerere, mawaziri wao, watoto wa Mzee Aikaeli Mbowe, watoto wa wafugaji, watoto wa wapishi n.k wote walikwenda kusoma katika shule moja bila ubaguzi tofauti na sasa ambapo kuna shule za vigogo na shule za kata zilizotelekezwa kwa ajili ya watoto wa walalahoi ....

CHADEMA ikishika dola itajikita katika maendeleo ya watu kwa wote ili bila kujali uwezo wa familia itahakikisha elimu inatolewa bila ubaguzi kutokana na wazazi kutokuwa na uwezo tofauti na CCM ya sasa inayopendelea elimu na shule bora kwa watoto wa vigogo...

CHADEMA ikiondoa ubaguzi huu wa elimu, ni kuwa chini uongozi makini wa CHADEMA, hata familia za raia wenye uwezo mdogo wa kipatowatoto wao watapata elimu isiyo bagua ... na kupata fursa ya maendeleo kama ya familia za vigogo ...
asante sana

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Hii ni Tz mpya ya Samia mpenda Suluhu 👇🏻

Screenshot_20230520-233652.png
 
ITV habari za chadema wanaziweka mwishoni kabisa katika taarifa yao ya habari. Hahah
 
Njombe, Tanzania

KAZI YA KIONGOZI NI KUSHUGHULIKA NA MATATZO YA WATU - Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa Mh. Peter Msigwa



Katika hotuba yake Mchg. Peter Msigwa alaumu serikali kupuuza maendeleo ya watu katika maeneo nyeti huku vigogo wa serikali wakitumbua kodi za wananchi kwa matumizi ya anasa mfano magari ya kifahari ya gharama za kufa mtu kama VX8 huku kinamama wajawazito wanalazimika kulipia Tshs. 300,000 wanapokwenda kujifungua pia hakuna huduma za maji katika maeneo ya makaazi ....
 
21 May 2023
Njombe, Tanzania

Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa ya CHADEMA Mh. Peter Msigwa azindua mradi wa maji Njombe



CHADEMA wamewaunga mkono wanachi wa wilaya ya Njombe mradi wao wa maji baada ya uongozi mzima wa CCM kuanzia serikali ya mtaa, kijiji, kata, wilaya, mkoa na taifa wizara ya maji kushindwa kuwaletea maji wananchi wa wilaya ya Njombe

CHADEMA YAPEWA HESHIMA NA WANANCHI KUZIDUA MRADI WA MAJI KIJIJI CHA ULIWA NJOMBE TANZANIA
8.JPG


Njombe, Tanzania

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimezindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliwa halmashauri ya mji wa Njombe uliojengwa kwa nguvu za wananchi uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 12 za kiTanzania unaonufaisha kaya 150 za vitongoji vya Itowa na Canada vilivyopo Njombe Tanzania .

Awali mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Njombe Rose Mayemba amesema wananchi wa kijiji hicho cha Uliwa waliamua kutengeneza mradi wao ili kufikisha maji kwenye makazi kutokana na kukosa huduma hiyo licha ya kuwa na vyanzo vya maji karibu ambapo mpaka sasa kaya 405 bado hazijafikiwa na mradi.

Akizindua mradi huo mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa Peter Msigwa aliyeongozana na viongozi mbali mbali wa kanda ametoa pongezi kwa wananchi bila kujali itiakdi za vyama kwa kufanikisha mradi huo uliopaswa kutekelezwa na serikali.

"Mmefanya kazi ya serikali kwa hiyo viongozi wenu wasikie kwamba mmefanya majukumu ambayo serikali ilipaswa kuyafanya,nyumba 150 sio haba na kwa hili tunaiambia serikali uwezekano wa kupata maji safi na salama inawezekana" amesema Mchg. Peter Msigwa

Emmanuel Mgulo kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Uliwa Njombe Tanzania amesema mradi huo umetekelezwa kwa takribani mwaka mmoja ambapo ulianza Desember 26, 2022 na kukamilika February 5, 2023 kutokana na fedha zilizopatikana kutoka kwa wananchi kwa njia ya uchangishaji.

Historia ya kukosa maji jimbo la Halmashauri ya Njombe mjini ilifika hadi Dodoma kupitia Edward F. Mwalongo aliyekuwa mbunge kupitia CCM 2015-2020 katika bajeti ya 2019/2020 akiwa bungeni , aliomba bila mafanikio kwa Mheshimiwa Waziri mtusaidie wananchi wa Lugenge wapate maji. Miundombinu ya usambazaji na matenki ya Vijiji vya Lugenge, Kiyaula, Kisilo, Ihalula na Otalingolo yalishakamilika lakini miundombinu ya kuleta maji kutoka kwenye chanzo mpaka leo haijakamilika.
 
Kitanga ni kata ya Wilaya ya Kasulu Vijijini katika Mkoa wa Kigoma nchini Tanzania. Wenyeji wa kata hiyo shughuli yao kubwa za kiuchumi zimejikita katika sekta ya Kilimo na Ufugaji .
Basanza, Uvinza
Kigoma

KATIBU MKUU WA CHADEMA MH. JOHN JOHN MNYIKA AKIWA BASANZA UVINZA KIGOMA



Katibu mkuu wa CHADEMA Mh. J.J Mnyika atangaza kuwa milango kuelekea uchaguzi wa kata Basanza na jimbo la Uvinza wajitokeze kuanzia sasa kwa kutia nia ili wapimwe na kupikwa ili baadaye kura za maoni ndani ya chama kuwa na wagombea wenye ushawishi mkubwa kuweza kushindana katika uchaguzi mkuu wa nchi na ule wa serikali za mitaa na vitongoji.

Mchakato huo wa kupata wagombea waliopikwa vizuri CHADEMA umeanza huku pia mazungumzo ya katiba mpya ili uchaguzi huru na haki ufanyike 2024 na 2025 chini ya Tume Huru ya Uchaguzi ambayo haitashirikisha wakurugenzi wa halmashauri.

Wananchi wa kata ya Basanza waliafiki mchakato huo wa kuwepo na katiba mpya na pia tume huru ya uchaguzi usiyohusisha wakurugenzi wa halmashauri ili uchaguzi uwe wa kweli, huru na haki 2025

RAMANI YA MKOA WA KIGOMA
1684635950982.png
 
View attachment 2626701

Kiukweli baada ya operesheni 255 , Matumaini ya Watanzania wengi yameongezeka mno !

Cha kufurahisha ni kwamba Hata wenzetu wana Usalama nao wameanza Kutabasamu .

Ama kwa hakika Tanzania mpya inanukia .
Mungu Ibariki Tanzania .

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Hawa ni polisi walewale wasemao wamesikia kuna hatari ya ugaidi au wameletwa wengine
 
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimezindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliwa halmashauri ya mji wa Njombe uliojengwa kwa nguvu za wananchi uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 12 za kiTanzania unaonufaisha kaya 150 za vitongoji vya Itowa na Canada vilivyopo Njombe Tanzania .

Awali mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Njombe Rose Mayemba amesema wananchi wa kijiji hicho cha Uliwa waliamua kutengeneza mradi wao ili kufikisha maji kwenye makazi kutokana na kukosa huduma hiyo licha ya kuwa na vyanzo vya maji karibu ambapo mpaka sasa kaya 405 bado hazijafikiwa na mradi.

Akizindua mradi huo mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa Peter Msigwa aliyeongozana na viongozi mbali mbali wa kanda ametoa pongezi kwa wananchi bila kujali itiakdi za vyama kwa kufanikisha mradi huo uliopaswa kutekelezwa na serikali.
Chama kimechangia ngapi kuwa boost wananchi hao
 
we are all at the same race and the same end why should one see oneself better than another we are all Tanzanians #NAIPENDATANZANIAYASASA
 
Asante kwa taarifa.

Ila ninatamani sana kama chadema kingekuwa na kitengo imara cha habari kutuhabarisha na kutupa nondo za hiyo mikutano.
Molemo where r u??
Kwahiyo huridhiki na erythromycin basi mm Clindamycin na wengine akina argument in wako
 
Live : Tarafa Muyama jimbo la Buhigwe Kigoma CHADEMA OPARESHENI 255


Elia Michael afisa tarafa wa Muyama anayesimamia vijiji saba vikiwemo Nyanga, Mugera, Kirungu, Katundu, Munyegera hadi Nsagara ampokea mwenyekiti wa CHADEMA taifa akiongozana na viongozi wa kitaifa makao makuu na viongozi wa CHADEMA Mkoa wa Kigoma.

Elia Michael afisa tarafa aliyepitia mikononi mwa Mwenyekiti Freeman Mbowe kisiasa alipopanda jukwaani kijijini Nyanga katika mkutano wa CHADEMA wa operesheni 255 asifia hali mpya ya kisiasa nchini Tanzania na kusema mtumishi wa serikali anaruhusiwa kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa.

Tarafa ya Muyama ndipo anapotokea makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Philip Isdor Mpango .

Kiongozi wa CHADEMA Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mh. Salum Mwalimu asikitika kuona hali ngumu ya wananchi wa Buhigwe tarafa ya Muyama. Lakini hatarajii Makamu wa Rais Dr. Philip Isdor Mpango kuipendelea tarafa ya Muyama kupita kiasi kama ilivyofanyika kwa Chato kupendelewa kupita kiasi wakati wa utawala wa Rais John Pombe Magufuli.

Mwenyekiti wa CHADEMA taifa alipopewa nafasi ya kuzungumza katika mkutano kijijini Muyama amlaumu Dr. Philip Isdor Mpango aliyehudumu kutoka nafasi za kutunga sera za kiuchumi hadi kuwa rai namba mbili kupitia cheo cha sasa cha Umakamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anahusika moja kwa moja na umasikini uliopo Kigoma, Katavi, Mtwara na kote nchini Tanzania .

Mwenyekiti Freeman Mbowe anasisitiza kuwa kodi duniani kote hutozwa katika kipato tena siyo cha kimasikini lakini serikali ya CCM katika kilo ya sukari kuna kodi ya shs. 1600 huku vocha ya simu kodi ni 30% mfuko wa simenti shs 7,000 kwa mfuko n.k n.k na kodi hizo zinakwenda kutumika katika kuwanunulia magari ya kifahari ya V8, posho nono nono na matumizi makubwa ya misafara ya magari ya viongozi wa serikali kupitia migongo ya wananchi masikini ...

Kuondokana na jaribio la kuiamini CCM kwa miaka 60 ni lazima kuiondoa CCM ili kubadililisha sera, aina ya utawala na mifumo ya kiuongozi ili nchi ipate maendeleo ya watu hatimaye kuondokana na umasikini anasisitiza Mwenyekiti Freeman Mbowe.

Imani za kijamii za CHADEMA ambazo ni Haki itawale popote, Uhuru yaani watu huru kutoa maoni yao, Demokrasia kupata viongozi wa watu kupitia chaguo huru la watu bila kuiba kura viongozi Maendeleo katika Watu Wote.

Wazee wa Kasulu waliuliza kuwa wazee hawafiki millioni moja katika nchi hii ya Tanzania vipi ishindwe kutoa matibabu bure kwa wazee anasema Mwenyekiti Freeman Mbowe

Jawabu la matatizo yote yanayowakabili wananchi wa Tanzania ni kuitoa CCM madarakani kupitia uchaguzi ulio huru na haki.
 
CHADEMA KIJIJINI MNANILA BUHIGWE KIGOMA OPERESHENI 255

Wananchi mamia wa kijiji cha Mnanila washika vifua vyao na kusema Mbowe we love You, we missed You kwa kipindi cha miaka 6 ....


Operesheni hiyo kali ya kisiasa ya siku 4 mkoani Kigoma leo imepita Kasulu Mjini
, Muyama kwenda hadi Munzese na kuishia Mungonya ambapo CHADEMA inaongea na wananchi wa majimbo ya mkoa wa Kigoma kutoa elimu ya uraia na kuimarisha chama.

Mwenyekiti Freeman Mbowe awaelezea wananchi wa Kasulu na Kigoma kuwa chama cha siasa kikiwa hakijengi mazingira ya kuwepo Maendeleo ya Watu katika biashara, ukulima, ufugaji n.k wakiache na kuchagua CHADEMA ili wawe huru kukihoji inapokengeuka kwani chama dola kongwe CCM hakiamini katika uhuru huo...
 
Back
Top Bottom