Kasulu, Kigoma
Tanzania
MKUTANO WA CHADEMA WA OPERASHENI 255, KTK KATA YA KITANGA KASULU VIJIJINI
Mamia ya wananchi wa kata ya Kitanga wajitokeza kwa wingi kumsikiliza Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Mh. Freeman Mbowe
Kitanga ni kata ya Wilaya ya Kasulu Vijijini katika Mkoa wa Kigoma nchini Tanzania. Wenyeji wa kata hiyo shughuli yao kubwa za kiuchumi zimejikita katika sekta ya Kilimo na Ufugaji .
Changamoto nyingine mbali ya ktk kilimo na ufugaji , ni miundo mbinu ya barabara kutoka vijiji vya Makere, Kitanga, Asante Nyerere, Kigabye, Kalela, Kwaga, Rusesa, Muzye, Bugaga na Kagerankanda n.k kwenda Kibondo ni barabara ambayo inasimamiwa na TANROADS, Mkoa wa Kigoma. Kuna changamoto katika Daraja hili la Mto Malagarasi, eneo hili ndiyo wananchi wa Kitanga wanapata shida kuvuka kwenda Kibondo.
Kabla mwenyekiti wa CHADEMA hajahutubia, wananchi walipewa fursa ya wazi kutoa dukuduku lao kuhusu mambo mbalimbali mbele ya umma uliofurika katika Ziara ya kikazi ya Operesheni 255 ya CHADEMA nchini kote .