Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wanaJF wenzangu,
Wakuu mimi sio mwanasiasa, na wala sijawahi kujishughulisha na mambo yoyote ya kisiasa. Ila nimekuwa mfuatiliaji na msomaji wa mambo ya kisiasa kupitia vyombo vya habari, mitandao, mikutano mbali mbali ya wanasiasa.
Na kiukweli katika kusoma na kufuatilia mambo hayo ya kisiasa, nimefahamu jambo moja au mawili yanayomfanya Rais Samia apendwe upande mmoja, na achukiwe upande mungine. Kwa leo ningependa nizungumzie jambo moja ambalo lina A mpaka D. Nalo ni 👇
1. Kwa vile Rais Samia alizaliwa na kukulia katika familia ya kawaida.
a) Hivyo na yeye amekuwa akijichukulia kama vile mtu wa kawaida,
b) Asiependa kujitukuza,
c) Asietamani kutumia mamlaka yake kuwaumiza wengine,
d) Lakini pia amekuwa akiyaelewa zaidi matatizo ya watu wa chini ambayo yeye binafsi ameyaishi na kupelekea kuwasaidia watu hao kupitia njia mbali mbali za kilimo, biashara na misaada ya hapo kwa hapo.
Hilo hapo juu ni jambo la kwanza linalosababisha Rais Samia apendwe na mamilioni ya Watanzania ambao wanaona, na kuelewa ni jinsi gani Rais Samia amekuwa akionesha mshikamano na kusimama upande wao kila wakati ili kuwapa muelekeo bora wa kesho yao.
Hii ni tofauti na wale waigizaji wanaokusanya michango ya hao hao wanyonge, na kuitumia kukatia ticket ya kuendea Ulaya kula bata na familia zao, zingine kulipia bills za shule za watoto wao na kuishi maisha ya anasa, alaf uchaguzi ukifika ndio waigizaji hao wanajifanya kurudi kuwahadaa baadhi ya wadanganyika kwa kujifanya kupanda bajaj, boda boda, mwendokasi nk, ili wapigiwe kura.
Tabia ya kujiweka karibu na watu wa aina zote haswa wa hali ya chini, limemfanya achukiwe na watu wachache (wapinzani) ambao wanaona wema huo wa Rais Samia kwa wananchi wa hali ya chini, unaweza kumpa ushindi wa kishindo katika uchaguzi wowote ule, hivyo kupelekea wapinzani hao kuangukia kidevu na kushindwa kuchukua madaraka kama wanavyojaribu kuwadanganya washikiwa akili wao mitandaoni.
So mpaka sasa nimeshaziona sababu ambazo zinamfanya apendwe na kuchukiwa. Ila nje ya mitandao wanaopenda na wengi kuliko wanaomchukia.