Hii ndio sababu Magenius hawawezi kuwa matapeli

Duh hata hii sentensi inasound kitapeli sana dah
 
Hizo za kwanza kuna mtoto wa baba mdogo wangu yupo std 2 anazo mpaka wanamuogopa wanatamani hata kumpeleka kwa wataalamu maana

Haongei na watu hata wazazi wake
Anajifungia ndani watoto wenzake wakija kwao
Performance yake ipo low sana (Na hapa ndio wazazi wake wanachanganyikiwa)
 
Singependa kutofautiana na wewe kwa yote ulioandika au kusema kwa maana upo sahihi kwa kiwango kikubwa sana. Ila naweka nyongeza inawezekana kwa kutumia lugha na mtazamo mwingine ambao ukiangalia kwa kina utakuta tunaongea jambo moja ambalo linaweza kuonakena tofauti kwa wanaowaza kidogo. IQ kirefu ni Intelligence Quotient ni uwezo wa kujifunza na kufikiri kwa kina(critical thiking) na uwezo wa kufikiri kimantiki( logical thinking) ni utafiti uliofanywa zadi ya miaka 100 iliyopita na mtu kama Francis Gatton na kuanza kufanyiwa majaribio baadaye na mtu kama Alfred Binet sio watu pekee walioendelea kufanya utafiti au majaribio ya kujua uwezo wa akili ni wengi sana na bado wanaendelea. Umeongelea IQ kwa mapana yake na kugawa kiwango cha binadamu katika matumizi ya akili zao katika makundi matatu singependa kurudia ulichoongea kwa urefu maana nipo kuunganisha ulichoongea na ungunduzi mpya zaidi ambao bado wengi pia wanaendelea kuufanyia kazi kwa maana ya matumizi. Kuna ungunduzi mpya wa EQ kirefu chake ni Emotion Intelligence ni uwezo wa kujitambua ambao unasemekana ni bora kuliko IQ. Binadamu ni kiumbe ambacho hakitofautiani sana na wanyama wengine kwa maana ya kuzaliwa na akili ila binadamu amekuwa tofauti na wanyama katika kutumia akili kujifanyia maisha bora zaidi kwa kutatua changamoto zinazojitokeza katika maisha wanyama wamekuwa na uwezo mdogo sana wa kupatia majibu changamoto zinazojitokeza ndio maana Wazungu au ngozi nyeupe zinawafananisha waafrika na wanyama sio kwa ajili ya rangi ya ngozi ila katika uwezo mdogo wa kupatia majibu changamoto tukiwa tumezungukwa na mazingira rafiki kwa maana ya hali ya hewa na rasilimali. EQ ni utafiti takiribani miaka 30 tu iliyopita na Wayne Paynes na kama miaka Ishirini iliyopita watu kama Daniel Goleman ndio waliogundua kuwa EQ ni bora kuliko IQ. Dunia haijalala kila siku kuna mabadiliko ya mazingira kwa maana ya maumbile kutokana na mambo mengi ambayo mengine ni asili lakini mengine yanatokana na maendeleo ya binadamu kutaka maisha bora ambayo yanaongeza athari za kimazingira ni jambo pana sana naweza kuandika kitabu kikubwa sana lakini sio lengo, nataka kueleza kwa kifupi jinsi ugunduzi,utafiti na ubunifu ambao unaendelea kila siku unavyoleta mabadiliko na kuzalisha matajiri na wenye kufikri vizuri kwa maana ya kusaidia wengene kufikri. Kwakua maendeleo ya binadamu yanatokana na uwezo wake wa matumizi ya akili yake kama tulivyoona katika tafiti za IQ na EQ kwa maana ya binadamu kugundua akili ndio kila kitu sasa wanafanya utafiti kujua jinsi akili inavyofanya kazi. Kwa sasa dunia inatengeneza matajiri wengi sana kila siku kutokana na ufahamu wa matumizi ya akili kuongezeka baada ya watu wengi kujua kutumia akili zao kwa kuzipa maarifa kwa maana ya taarifa sahihi kila siku na sasa pia kupata taarifa imekuwa rahisi kuliko kipindi chochote cha nyuma kugundulika kwa EQ kutawezesha dunia kuwa na maendeleo ya ajabu sana miaka Ishirini ijayo maana idadi kubwa zaidi ya wanadamu wenye kujitambua itaongezeka. Kwa leo naomba kuishia hapo ila nafahamu nachoelezea inawezekana sijakuwa na mpangalio mzuri inaweza kusababisha kutumia nguvu nyingi kuelewa ninachomanisha lakini tupo tutaendelea kuhabarishana...............
 
Mkuu uwe una tag mim ila u mwaka post zako zimepungua uku ukileta chakula ya ubongo nitafrai kupata habari mapema🕵🏽
 
We utakuwa Ni tapeli pia, Maana hayo maana hili andiko ladhibitisha ya kuwa ww ni intelligent, na intelligents wengi wao ni matapeli kama ulivodadavua.

Mi nishajijua nipo kundi gani
 
Humble african where are you brother you are missed aisee [emoji28]
 
mi nimepewa mtoto ana autism. ni kweli usemayo. yuko vizur mno ila anaish dunia yake. naumia sana nikimuona. na ninampenda mpaka naumwa.
 
Aisee Usonji ni mtindio wa ubongo bhana na sio autism. Autism ni kama Aspergers syndrome. Mi najua wenye usonji ni wale mataila wa kutoa udenda. Labda autism ina jina jingine la kiswahili
 
Mtu ambae ni highly intelligent(genius) na aliye chini ya normal( mental defect-upungufu wa akili, ulemavu wa akili) Mara nyingi tabia zao zinashabihiana hasa kwenye suala la ukimya na kukwepa watu hivyo wachunguze yupo kundi lipi maana kuna namna ya kuwatofautisha
 
Naweza sema huyo wa mazingira magumu IQ yake ilidrop kutokana kwamba hakujifunza aliyokuwa akiyajua mwenzake. Ila kama akijifunza anauwezo wa kuwa na IQ sawa na mwenzake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…