Hii ndio sababu Magenius hawawezi kuwa matapeli

Hii ndio sababu Magenius hawawezi kuwa matapeli

Ndio nikitu unachoweza kutengeneza mapema tokea mimba kuzaliwa malezi na makuzi, kila mtu amezaliwa akiwa na akili ziro lakini hukua na kuongezeka nakupanuka na kuzidi kiwango kutokana na mazingira ya makuzi na malezi. So kwa kua mimi mazingira hayakuruhusu ndio maana sikufikia kiwango cha akili nyingi, ila ninao uwezo nia na sababu kwa mwanangu kua hivyo.
Kama wewe mumeo na koo zenu ni normal hata ule nini au ulee vipi hauwezi toa genius. Unatakiwa uzaliwe hivyo kwanza urithi kwa genetics kisha makuzi na mazingira ni kuendeleza kama ambavyo mtu hukuza kipaji alichozaliwa nacho.La hatuzaliwi hatuna akili Bali ni kuwa 'tunazaaliwa na akili Ila hatuzaliwi na uelewa' uelewa unakuja kwa kujifunza na makuzi na mazingira sasa ukijumlisha ndo yanachangia uelewa anaokuwa nao MTU.na pia uelewa wako unaamuliwa na akili yako ya kuzaliwa nayo. Yaani kiwango chako cha uelewa kinaamuliwa na kiwango chako cha akili ulizozaliwa Nazo, ni kama kusema kwa kiingereza kuwa " you're ability to be smart is determined by you're intelligence level" hivyo ni kuwa " we were born intelligent but not smart" smartness is acquired through learning but intelligence is something you're born with (IQ) and it can be below average,average, above average or upper(genius).
 
Huu uzi umefikirisha sana. Nina mwanangu ana miaka mitano na ninahisi ana dalili zote ulizoziandika za kundi la kwanza. Sijui nifanyeje?
 
Kuna dogo moja wayback Alikuwa gumzo tangu utotoni (elimu ya awali mpaka O level, Ila Kazingua o level....mtaa Anajulikana kama genius......Nlipata bahati ya kupiga nae stori akasema Mikwaruzano ya kifamilia ndo ilimharibia , (ilimfelisha) imagine alikuwa haandiki notes ila Top 3 humkosi, , , ngeli anagonga balaa bio na agr Kama hayupo class Ticha hafundishi.....alikuwa mkorofi kinoma .....



Malezi yanaplay part gani kwenye intelligence ya mtu?
 
Kuna hawa vijana wawili humu jf ambao ni hatar Sana. Mshana Jr na The Bold je wako kundi gani maana huwa duh hawafai kabsaa thread zao ni noma
Intelligence hao. Cause magenius si rahisi mtu wa kawaida ukawaelewa labda uwe genius au intelligent

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tapeli ni Genius pia!! sema tu ki-Bongo bongo mnawadharau!! ni bonge la mtaji, tena utapeli ni sanaa ni kipaji adimu, think again, nakupa mfano hawa kwa jeshi la Israel ni Mtaji mkubwa sana!!

wanajua lugha za kiarabu km waarabu, wengi wameajiliwa na MOSSAD AL ABEIT! ndani wanaishi na waarabu km waarabu asilia lkn wanaifanyia kazi Israel! wameoa, wamezaa koo! tena mpaka za kifalme!! King Abdulah wa Jordani ni muisrael damu damu, yule! mke wa Yasser Arafat ni yahudi hawa walioa na kuolewa kitapeli! Mohamedi Budia ni tapeli yahudi yule!

Utapeli ni sanaa! ni kipaji adimu! wapelekeni TISS!
 
Duniani tumo binadamu wa aina tatu kiakili na wote tunaishi pamoja in harmony na tumegawanyika katika makundi makuu matatu kiutendaji na utekelezaji wa akili zetu.

Kundi la kwanza ni wale Magenius.. Hawa mabwana wana IQ kubwa kuliko binadamu wa kawaida wana score around (160 - 300) wana uwezo mkubwa sana wa kuchakata taarifa vichwani mwao na kufumbua mafumbo magumu kuliko ila bahati mbaya zaidi hawa asilimia 90% yao ni wagonjwa wa ugonjwa wa usonji( Autism). Ugonjwa wa akili huu, ugonjwa huu wa usonji mara nyingi huwapata wakiwa watoto wa mwaka na nusu na kuendelea. Dalili zao huwa wanapenda kukaa peke yao, hawapendi kelele, wanachelewa kuongea, wana hisia Kali sana za kunusa na kusikia na wako very bright kwenye kitu kimoja pekee. Na pia huwa wanaongea kidogo sana..they only do "small talk" they are not good conversationalist. Sio waongeaji wazuri sana.

Nilifuatilia zaidi na kuyajua mengi juu ya Autism baada ya mpwa wangu kugundulika ana ugonjwa huu wa usonji akiwa na miaka 3..huyu dogo ana miaka 10 tu kwa sasa mnaweza kuwa mmekaa nje akawambia mtoto analia na kweli after a second dogo analia ndani...then mmekaa nje anakwambia maharage yanaungua..na kweli mnasikia harufu ya maharahe kuungua jikoni punde baada ya yeye kusema. Wako very sensitive. Ni wakimya na pia very loner..wanapenda kukaa wenyewe tu na huwa wanaconcetrates na kitu kimoja tu mawazoni mwao huyu dogo shuleni ni mtupu but he is very artistic genius and creative, unaweza ukatembea nae mjini then mkirudi home anadrawing kit yake ya kuchorea tu anachora mji mzima mlimopita kwa usahihi bila kurejea popote pale hadi huwa navurugwa ufahamu ukizingatia Mimi hata kuchora kagari tu siwezi. Nikagundua dogo is genius sababu ya ugonjwa wake wa usonji.

Nikarejea historia ya Michelangelo na Vincent Von Gosh hawa wote walikuwa artistic genius..huyu Van Gosh alikuwa anaweza kuuchora hadi upepo unaovuma..hakyamungu! This is insanely genius..ukingalia kwenye picha zake za starry starry night utaona kazi zake but alikuwa mwehu na michoro hii aliichora akiwa kwenye chumba cha vichaa alipojipiga risasi na kufariki akiwa mpweke sana. Michaelangelo huyu ni balaa yeye hata simzungumzii maana anahitaji Uzi wake kabisa ili tumtendee haki. Tukipata muda tutamjadili.

Albert Einstein Mwanamahesabu na mwanafikizia ambae amebadilisha maisha ya binadamu anaaminika kuwa the most influential scientist of the 20th century, amechangia mengi kwenye aerospace engineering, astrophysics, mathematic, spirituality e.t.c alifanya kazi kubwa ya sisi kuishi hivi Leo kwa theory yake of relativity ya E=MC sqaure ndio theory iliofagia njia ya kutengeneza mabomu ya nyuklia Leo hii. Akiwa na miaka 10 usonji ukiwa umemuandama hakuweza kuongea vizuri wala kuwa na marafiki akiwa na IQ kubwa kabisa aliweza kufaulu somo moja tu la hisabati tu shuleni yaliyobaki alifeli vibaya sana. Alipofikisha miaka 16 alikuwa anaitwa chuoni kusolve complex mathematics equations zilizowashinda maproffesor na akiwa na miaka 25 hakukubaliwa na vyuo vingi maana kwenye mtihani wa kujiunga na chuo alifaulu somo moja pekee mathematics kwa asilimia 100. Watu hawa huwa wanakuwa na ugonjwa wa Usonji unaowafanya kufikiri kitu kimoja tu deeply kutokana na nerve circuit zao zilivyoundwa kwenye brain. Magenius maarufu Waliothibitika kuwa na Autism ni Albert Einstein, Charles Darwin, Sir Issac Newton, Michelangelo, Aristotle, Tesla e.t.c Wengi wao wana muandiko mbaya sana maana mikono yao haiwawezi kuendana na kasi ya ubongo unavyofikiri, hivyo wanajikuta wanaandika fasta na rough ili kukimbizana na kasi ya ubongo wao unachokifikiria.

Tunahitimisha kwa kukubaliana na mwanafalsa maarufu wa ugiriki ya kale kwamba any genius is accompanied with some sense of madness.. Magenius wengi ni vichaa na hii inapigiliwa msumari na kauli hii "too much of anything is harmful " akili ikizidi kipimo muhusika anakuwa hayuko normal na hivyo anakuwa psychiatric Case hivyo ni ngumu sana kichaa kukutapeli maana ni mgonjwa wa akili maana ana complex things kichwani ambazo hata yeye hawezi na hana lugha ya kuzielezea kwa watu wakamwelewa kirahisi atawezaje kukushawishi uingie mkenge!? Jibu ni hawezi kukutapeli maana hata hawana good socializing ability kama wengine. lakini hapa sasa ndipo linapoibuka kundi la watu wengine wanaitwa "intelligent people" watu hatari sana hawa.

Hawa intelligent people bongo zao ziko katikakati kiakili wana uwezo wa kupata maneno sahihi ya kuelezea zile complex ides za genius..hawa uandika hata zile manual zinavoelezea namna ya kutumia vitu mbalimbali vilivyoundwa na magenius kwa lugha rahisi na nyepesi maana wanayo maneno sahihi na ya kueleweka kirahisi, hawa wanaandika kimkakati hoja zao na kuweza kushawishi watu kirahisi sana kama alivyosema Fid Q msanii wa hip hop kwamba "neno zuri huwa halina ukweli na neno baya ndio lenye ukweli " hawa intelligents siku zote Daima dumu wana maneno sahihi na matamu ya kukufanya uuone ukweli au usiuone.. Aina ya watu hawa ni Adolph Hitler, Barack Obama, Hemingway, e.t.c na Kwenye hili kundi wanakaa matapeli pia Kariba ya brother wa Forex n.k sijawahi kuona katika maisha yangu tapeli asie jua kupachika maneno sahihi na matamu kwenye maandishi au maneno yake. Sijawahi kumuona! Mtaji wao ni maneno yake matamu.

Then group la mwisho ni "normal people" au tunafahamika zaidi kama watapeliwa Ahahaha. Sisi tunafit Kwenye social world maana tunaenda clockwise na jamii yetu na bongo zetu hazijisumbui kuchakata taarifa zaidi wala kuconcertrates na kitu kimoja we are carefree hatuna tofauti na simu za Motorola za zamani mwanga ukizima zinazima moja kwa moja hadi ndani tofauti na intelligents ambao wao ni simu janja(smartphone) zenyewe screen ikizima na kuwa nyeusi ujue imezima kinafiki internal background inaprocess more informations kifupi hazilali bongo zao tofauti na normal people sisi ambao ni kundi kubwa akili zetu ni za kawaida sana na ndio akili za binadamu wenye afya na wazima kiakili maana hatuoverload brain zetu na sisi sio wagonjwa wa akili kama hao wawili hapo juu wanaosumbukiwa na Autism na Bipolar disorder.

Tujitahidi tujue mechanism za matapeli na tuwaepuke mapema before its too late.

Na je unadhani wewe unafit group gani hapo juu? Kwanini unahisi group ulilochagua linakufaa? Tupe sababu?
Usonji au Autism huujui mkuu, fanya home work yako vizuri.Autism unaletwa na chanjo mkuu kwa vile zina Mercury, Aluminium na Lead.Hizi zina haribu ubongo na kufanya mtoto kuwa degenerate.Sasa ukiniambia mtoto mwenye Autism ana IQ kubwa sikuelewi.Most likely huyo atakuwa na kitu kingine, na most likely ni demonic forces.
 
Jamaa is simply a genius,wewe lete mada yoyote,iwe ya kisiasa-rais wa nchi yoyote duniani,historia zao,historia ya nchi zao,nk,sayansi-viumbe vya baharini,nchi kavu,sayansi,uchumi,michezo-soka,boxing,rugby,wrestling,movie-sema movie yoyote anaweza kukutajia wahusika majina yaohalisi,asili yao wanakotoka,historia zao,kila kitu atakupa reference ya hicho kitu kwa kukot kwenye kitabu au source yoyote mwaka,eneo,wahusika,neno kwa neno.Yaani ukibishana nae unaumbuka..Incredible memories!!Yaan hata alivyofeli kila mtu aliendelea kumheshimu genius.Unaweza kuta anatembea anacheka mwenyewe kwa material yanavyotiririka kichwani.Acha kabisa
kuna mwamba mmoja na sie tulikuwa tunamuita google...na yeye alizingua darasani lakini yuko informed kupita maelezo
 
Usonji au Autism huujui mkuu, fanya home work yako vizuri.Autism unaletwa na chanjo mkuu kwa vile zina Mercury, Aluminium na Lead.Hizi zina haribu ubongo na kufanya mtoto kuwa degenerate.Sasa ukiniambia mtoto mwenye Autism ana IQ kubwa sikuelewi.Most likely huyo atakuwa na kitu kingine, na most likely ni demonic forces.
jamaa alichoandika yupo sahihi 100%. ila kuna sehem hajaweka sawa. autisim ziko mara mbili. kuna hyo anayosema mtu kuwa na akili moja mkimya nk. halafu kuna ile ya mazezeta kabisa. mi ninae mtoto ana hilo tatizo la autisim. akiwa mwaka na nusu anajua kusoma na kuandika kwa kuangalia Tv hakuna mtu alikuwa anajua. mpaka cku tunamkuta amejiandikia mwenyewe. aliongea vizur akiwa na miaka 6. ila darasan ni wakwanza mpaka leo. yupo darasa la 7. mkimya haongei na ana mambo yake mara nyingi. nilipata shida sana kumwelewa. nilijua ni Autism baada ya kumpeleka shule flan ya wazungu ndio wakaniambia. mi wa kwangu ni mdadis sana. aliwah kunivunjia tv akitafuta wanaoongea humo ndan. kwa ushaur wa wale wazungu nimefanikiwa kumlea kwa kujua namna ya kudance accodingly. sasa hv ukimuona hutajua kama ana hlo tatizo. anapenda sana hesabu na kiingereza. na moja ya vitu muhm walichoniambia wale walim wakizungu nikuwa. wana akili moja tu so mnunulie gitaa piano na laptop. na awe anaogelea. so kwenye masomo yake akichamganya somo la gitaa piano laptop na swiming utamgundua anachopendelea so ukimjua tu mpeleke huko huko. na ndicho kilichotokea kwa mwanangu. kitu kimoja muhm watu wanatakiwa kujua ni kuwa. kumlelea mtoto mmoja mwenye autism ni sawa na kulelea watoto wanne wazima. namshukuru Mungu amenisaidia jamaa kwa sasa yuko vizur mno.
 
Back
Top Bottom