Hii ndio sababu Vijana wengi Tunakufa mapema, hauwezi kutoboa kwa mtindo huu wa maisha

Hii ndio sababu Vijana wengi Tunakufa mapema, hauwezi kutoboa kwa mtindo huu wa maisha

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Hebu fikiria unaamka tu unakutana na hili balaa...

MDOGO WAKO:Kaka naomba 600,000/= Kwa ajili ya ada . Walisema nisipolipa hawatanipokea kabisa .

BABA MWENYE NYUMBA:Missed Calls 83 na Ujumbe: Leo nakupatia Nafasi ya Mwisho

BINTI WA JIRANI: Nafikiri Nina Ujauzito wako .

RAFIKI YAKO: Kaka ,fedha yangu lini unanipa? Ni mwisho wa mwezi Sasa ulioniahidi mara ya Mwisho.

WAZAZI: Tunakufa Kwa Njaa kijana wetu .
Hatuna chochote , Tusaidie .

MCHUMBA: Sawa tu,naona umeanza kunionyesha dharau kabla hata hatujaoana. Endelea tu na Hao Malaya wako. Usinitafute mimi. Pepo wewe!

EX: Ulinitumia tu ,Mbwa wewe. Utakufa Kifo kibaya sana.

M PESA:Unakumbushwa kulipa Mkopo wako wa SONGESHA kiasi Cha Tsh. 63200/=

TALA: Tunajua unapoishi , Wewe ni Mdaiwa sugu Sasa na tutakukamata tu.

MSHAHARA :Kiasi Cha Tsh. 87,000 kimewekwa kwenye akaunti Yako inayoishia 3214.

SONGESHA: kiasi Cha Tsh. 63200 kimekatwa kwenye akaunti yako ili kulipa mkopo wako. Salio lako ni Tsh. 23,800

GETINI: "Wapangaji ambao hawajalipa Hela ya ulinzi shirikishi na Takataka mnapewa siku 3, vinginevyo mtaitwa Ofisi za Serikali za Mtaa."
==================

Vaa hivi Viatu,
Mwanaume ,Utakuwaje Kawaida Hapa?

Bado kitaa nao wanakuzingua
 
Matatizo kadhaa hapo ni mtu kajitafutia...
TALA..ukute ulitumia kuhonga ama kusambaza bia kwa washkaji.
Binti wa jirani..nyege mshindo akati una mchumba.
Ex....huna msimamo, kwann uachane nae baadae uje umkule
FEDHA inahitaji discipline. Huwezi kufanya kila kitu hapa duniani. Kuwa na vipaumbele.

Unajijua choka mbaya, unagonga maex na mabinti wa jirani na unakopa voda na tala, unategemea baba mwenye nyumba akuchekee au akuonee huruma..afu ndo una mchumba. Umeyatafuta mwenyewe.
 
Uliyo andika hapo ndo maisha ya kila siku

Lete sasa kinachotuua mapema
 
Mambo yote haya uliyoorodhesha ni MAJANGA YA KUJITAKIA KWA HIYARI. Hakuna hata janga moja kati ya hayo uliyotaja yanaweza kusababishwa kwa kudra za Mungu.
Je, umeshawahi kuishi katika nchi yoyote ile ya Kibepari au nchi ya Mabeberu??? Endapo kama umewahi, utakubaliana na Mimi kwamba huko hakuna Upuuzi kama huu. Mambo kama hayo yapo katika nchi za watu wasiostaarabika tu, kama hizi za kwetu barani Afrika.
 
Back
Top Bottom