Hii ndio Sababu ya Mungu Kutoonekana

Hii ndio Sababu ya Mungu Kutoonekana

Mawazo yangu kuwa Tofauti na Yako haimaanishi wewe usitumie Akili timamu Kujua Ukweli au Uongo.

Sijataka Uamini nimetaka wewe utumie Akili Timamu kujua Mambo kuamini na Kutoamini si Jukumu langu hilo ni Lako mwenyewe. Hata Hizo dini mlizoletewa Ziliwakuta Mna Imani Zenu ila Mkazipuuza Mkaamini Hizo na Mpaka leo mnazitetea bila Kujua Ukweli

I believe in God, nimemuona in so many ways, even kwenye situations nilizoona kwa akili yangu sitoboi nikamuomba yeye akanijibu tena kwa upesi

Naamini katika universe and it’s nature pia na napeta tu[emoji4][emoji4][emoji4]
 
I believe in God,nimemuona in so many ways, even kwenye situations nilizoona kwa akili yangu sitoboi nikamuomba yeye akanijibu tena kwa upesi

Unaweza Kusema Ni jinsi Gani Akili yako ilishindwa Kutatua Ila Mungu ndio akakutatulia Swala lako! Yaani wewe ulikaa pembeni ila Mungu akaja akakufanyia Jambo lako.

Ndugu yangu Mungu amekupatia Akili Timamu Ukiitumia vizuri inatatua tatizo lolote lile. Na kumbuka Binadamu tumeumbwa kusaidiana Sisi kwa Sisi. Mfano Riziki zinatoka kwetu sisi Binadamu Mana Ukimuomba Binadamu mwenzako pesa/maji/chakula n.k atakupatia mana Mungu ametuumba Tusaidiane sisi kwa Sisi

Sasa Isije ikatokea umefanya kazi ukalipwa mshahara mnono ukasema Mungu Amenipa Riziki. Wakati Usingefanya hiyo kazi Mungu Asingekupa Mshahara kumbuka Aliyekupa Mshahara ni Binadamu mwenzako na Anaweza Kukunyima Pia




Naamini katika universe and it’s nature pia na napeta tu[emoji4][emoji4][emoji4]

Uumbaji wa Mungu umemuumba Binadamu kuishi na Baadae azeeke afe. Hata Washenzi wanapeta Kuliko Wewe. Waovu na Wabaya wanapeta kuliko wewe maana Mungu keshaumba Hivyo

Tunatofautiana Kumtiii Mungu tu. Kwingineko wote tunamtegemea Mungu. Wabaya na Wazuri na Wacha Mungu wote tunamtegemea Mungu
 
Amevaa mavazi meupeee anapendeza kwelikweli
Kama Anaweza Vaa Vazi Jeupe anatofauti gani na Wewe mwanadamu. Kwahiyo Mungu wako ana Mwili unaoweza Kuvaa Vazi jeupe! Ndugu yangu

Halafu mnaimba Hakuna Wa Kufanana naye[emoji445][emoji445]

Halafu katika vitabu unavyoamini imeandikwa hakuna Aliyemuona Mungu akaishi. Sasa Inakuwaje wewe umemuona na Mavazi meupe amevaa bado upo JF ndugu yangu mbona Hatutumii akili timamu Tu
 
Huenda hivyo vitu ndio wanaamini ni mungu mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Maana Ni Viumbe wasivyovijua Na Ndivyo vinavyowatawala. Wakinena kwa Lugha wanahisi ni Roho Mtakatifu. Sasa Inakuwaje Wanaongea vitu ambavyo hata wao ukiwauliza hawajui wanachosema

Na anayesikia (wewe au mimi ) hatuelewi wanachoongea nini maana ya Kunena sasa kama Huwezi Elewa
 
Mungu ni roho sio mwili.. Ulipo yupo..Mungu ni nishati hai haionekani Lakini IPO..! Na inafanya kazi.. Bila yeye huwezi kunyanyua hata kope yako
 
Mwenye Enzi Mungu haonekani kwa Sababu yeye hayupo pamoja na Viumbe wake. Yeye yupo alipo na Viumbe wake wapo walipo hana Upendeleo na Kiumbe Yeyote yule bali ana Enzi na Viumbe wake

Yeye hausiani na Viumbe wake na Wala hakai na Viumbe wake aliwaumba na Kuwaweka Katika Sayari zake na Kila Kiumbe akamjalia akili za Kuishi kwake

Habari za kwamba Mwenye Enzi Mungu Anaongea na Viumbe wake kupitia Malaika au Mwenyewe alikuwepo Duniani si Habari Sahihi. Na kama Ingekuwa hivyo mpaka leo hii basi Angekuwa anakuja Na Kuongea na Viumbe wake

Maana Kulingana na Vitabu Mwanzo alikuwa Anaongea na Kutembea bustanini na Kuongea na Viumbe wake ila Baadae akaacha na Kuanza kutuma malaika. Ila leo hii Hata hao Malaika Hawaonekani tena, Dhana hii Haiingii akilini Kwa Mtu anayetumia akili Timamu. Kitu kinachopelekea kwamba watu wengi wamepotoshwa kumhusu Mungu na Viumbe waovu.

Mwenye Enzi Mungu hakuwahi kufanya hayo yote hajawahi kaa na Viumbe wake wala kutuma Viumbe waende kwa Viumbe wengine kumuelezea yeye alivyo.

Hawa wanaoleta Ujumbe na Kusema Ni Ujumbe wa Mungu hawajatumwa Na Mungu mwenye Vyote bali ni Viumbe waharibifu waliokuja Duniani kimagendo. Na kuwaingia watu na Kusema Kupitia Vinywa vya Watu. Kama Vile Jini anavyoingia Kwa Mtu na kusema atakavyo.

Mungu Haonekani kwa Sababu hakai na wewe hapa Duniani na Hawezi onekana a maana Hayupo pamoja na Viumbe wake. Yeye yupo alipo na Wewe upo alipotaka uwepo

ASANTENI
Sijaona sababu kwanini Mungu haonekani kwenye bandiko lako.
Ulichokielezea hapa ni ufahamu wako tu,sio absolute truth,ni porojo tu.kila mtu ana porojo zake,huwezi kuthibitisha Mungu anaongea na watu au la.
 
Sijaona sababu kwanini Mungu haonekani kwenye bandiko lako.
Ulichokielezea hapa ni ufahamu wako tu,sio absolute truth,ni porojo tu.kila mtu ana porojo zake,huwezi kuthibitisha Mungu anaongea na watu au la.
Wewe unaamini nini ndugu yangu. Maana zangu ni Porojo je wewe Unaamini nini

Maana Absolute Truth unao. Hebu niambie wewe Mungu anaonekanaje
 
Wenzako wenye akili timamu kama Kiranga hawaamini kama MUNGU yupo so ayo mambo ya kuamini habari za MUNGU aliyefanyika mwanadamu (KRISTO YESU);tuachieni sisi wajinga tumuamini aliye ufufuo na uzima💯❤🙏✍
 
Wenzako wenye akili timamu kama Kiranga hawaamini kama MUNGU yupo so ayo mambo ya kuamini habari za MUNGU aliyefanyika mwanadamu (KRISTO YESU);tuachieni sisi wajinga tumuamini aliye ufufuo na uzima[emoji817][emoji173][emoji120][emoji871]
Usipojua Huna Hatia.

Unaamini alikufa kwa Dhambi zako pale msalabani. Je hizi dhambi unazofanya Sasa Hivi ni za Nani!
 
Back
Top Bottom