LGE2024 Hii ndio Sababu ya Watendaji kukimbia Ofisi ili kuihujumu Chadema, Hata hivyo watashindwa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
SIJUI HATA MNAHANGAIKA NA NINI WAKATI MNAJUA KABISA HAMTASHINDA YAANI HAPO KAMA MNAFANYA MAIGIZO TU
 
Reactions: Tui
Kwa mfano Mtiti huu wa Chadema Jimbo la Mbarali Haukutarajiwa na wengi, Kwa vile ilidhaniwa kwamba Utekaji na Mauaji waliyofanyiwa viongozi wa Chadema labda ungewaogopesha Wanachama wake kuchukua fomu
Ishara nzuri hii, kama maeneo mengi nchini mwamko huu upo. Lakini tusisahau, hii ni ngwe ya kwanza tu, na huko kupotea kwa wenye ofisi ni hatua ndogo tu. Bado kuna pesa za Abdul zitamwagika kila mahali kuwanunua hao hao wanaorudisha fomu leo!
Na bado pikipiki kila kata hazijaanza kazi!
Hakika "Hii ni Vita".
 
Kumbe Abdul ana hela za kununua kila Mtanganyika! Astaghafillulah!
 
Hakuna kitu
Kwenye geti la chuo kikuu Cha Cape Town nchini Africa kusini kuna maandish yasemayo"
"Ukitaka kuangamiza taifa lolote duniani huhitaji kutumia silaha za nyuklia wala mabomu ya atomic. Njia nzuri ya kuangamiza taifa ni kuharibu mfumo wa elimu. "Ruhusu mbumbumbu waonekane wamefaulu na wasonge mbele.

Matokeo yake yatajionesha baada ya muda, "mbumbumbu" hao wakisha hitimu.
Wagonjwa watafia mikononi mwa madaktari, majengo yataanguka mikononi mwa wahandisi, pesa zitapotelea mikononi mwa wachumi, utu utapotea mikononi mwa viongozi wa dini, na haki itapotea mikononi mwa mahakimu.

#Kuchezea Elimu Ni Kuangamiza Taifa. ......✍️
 
Kumbe Abdul ana hela za kununua kila Mtanganyika! Astaghafillulah!
Usifanye masihara mkuu 'Erythro'. Hapa watu kufikia kutoa roho za watu na kudai 'kifo ni kifo tu", usifikiri kuna utani hapo!

Hawa pesa siyo tatizo kwao hata kidogo, kwa sababu wana wafadhili wenye mikoba mizito sana ambao wapo tayari kutununua sisi sote kwa maslahi yao.
Tutakao baki tunapiga kelele, hilo siyo tatizo kwao, mradi tu wapo wengi tu miongoni mwetu walio tayari kuuza utu wetu sote.

Ki-nchi, kama UAE na ukwasi wote ule kitashindwa vipi kulinunua li-nchi kubwa kama Tanganyika ambalo watu wake vichwani mwao kuna upungufu mkubwa!
 
Ndiyo maana na sisi tunaongozwa na failure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…