Hii ndio sheria itakayo waumbua Simba sc Fifa

Barua ya tff inasema fakhi hakuwa na kadi tatu za njano..
 
Mkuu kwa Udaku umefuzu
 
Kwa mujibu wa simba fakhi alipata kadi zote tatu katika mechi za ligi kuu,, so tff ndo watakaotoa ushahd ambao FIFA watautumia kutoa maamuzi.

Bahati nzuri FIFA haiamini kamwe katika kutoa points mezani. Sana sana itakuwa fines tu kwa wote waliohusika ila ubingwa ndo hivyo tena kwani matokeo ya uwanjani kati ya Simba vs Kagera Sugar yatabaki kama yalivyo.
 
Kuwa mkubwa kiumri haimaanishi kuwa wewe ni muelewa kunizidi.nilichokiona kwako ni ushabiki wa kutaka wenzio wamatopeni uwaliwaze.Yanga haina haja na suluhu yoyote toka kwa simba kwakuwa simba haikuambulia chichote kaitaba
Hata Akilimali ni kikongwe
 
Kwa mujibu wa simba fakhi alipata kadi zote tatu katika mechi za ligi kuu,, so tff ndo watakaotoa ushahd ambao FIFA watautumia kutoa maamuzi.
Nakuunga mkono,,na nduo madai ya simba, kitu cha kujiuliza, kwanini wasingeweza kutumia recorded matcha kati ya simba vs African lion kuona iwapo kweli kulikuwa,na kadi 3 za njano kabla ya mechi kati ya Sumba na kagera sugar?
 
Kamati ya SAA 72 haikupaswa kushugulikia hiyo rufaa kwasababu haikuwahusu, ilikatwa nje ya mda na haikulipiwa walichopaswa ni kuacha kamati ya nidhamu ilishughulikie sasa kitendo cha kusikiliza rufaa yenye ukakasi ni kinyume cha taratibu na ni viashiria vya rushwa , lakin pia ukumbuke kamati ya SAA 72 ilikaa Mara 2 kutoa maauzi ambapo pia walimwita muamuzi wa mchezo kutoa ushaidi sasa jambo la kujiuliza kwanini aitwe muamuzi? Inamaana data hazikuwepo? Kama zilikuwepo sabab zip zilifanya wakae zaid y mar mbili kutoa maauzi? Kwakuzingatia maelezo hayo tyari utaona kunaviashiria vya rushwa.
 
Pole,inaonekana ni mfatiliaji mzuri wa mamho ya soka hususan Simba.Pole kwa sababu unatuamisha ujinga ambao sisi wengine hatujauzoea.
Hivi kwa nn Simba walikubali kufungwa na Kagera 2-1 ambapo walijui kuwa ile gemu ni muhimu sana kwa mustakabali wa Ubingwa.
Kwa taarifa yako simba walikuwa hapaswi kukata rufaa na baadala yake ni kuwapa taarifa tu TFF juu ya kile ambacho walihisi si sahihi.
 
Post kama hii ndiyo inaweza kutufanya Wana Simba SC tusitake suluhu nanyi na tukakinukishe huko FIFA muaibike zaidi.
Suluhu na Yanga? Nyie issue yenu ni TFF na Kagera sugar. Yanga alichofanya kushinda mechi zake kihalali uwanjani. Hayo ya mezani hayawahusu mkitaka ubingwa wa kupewa nendeni tu FIFA. Ila ni vema mkajikita kutafuta matokeo uwanjani wakati mwingine.
 
Tatzo walotoa maamuzi c wenye mamlaka, kuna viashiria vya rushwa kwa maana muda wao ulipta na maamuzi yalitakiwa yatolewe na kamati ya nidham
 
Wanajisumbua fifa hakuna rufaa yoyote mpaka sasa simba kapgwa mimba na swalaa
 
Kesi ishawashnda fifa watashangaa tuu hakuna kesi mmeliwa smba mlikuwa mnaongeaa sn tulien nyie n watumwa wa YANGA sasa
 
MAAJABU YA VIONGOZI WA SIMBA SC NA FIFA SAGA!

Na. Fredy Masolwa.

Jana baada ya msimu wa Ligi kuu Tanzania bara 2016/2017 kumalizika kwenye viwanja vinane, kumeibuka na sintofahamu nyingi sana kwenye mitandao ya kijamii.

Sintofahamu hizo zilianza baada ya Yanga kupigwa na timu ya Mbao FC goli 1, kwenye mchezo wao wa kumaliza msimu huu uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Nakuzifanya Simba na Yanga kuhitimisha kwa pointi sawa 83, lakini Yanga akatangazwa Bingwa kwa wingi wa magoli, akichukua mara 27 na kwa mfululizo miaka 3.

BAADA YA MECHI 08!

Baada mechi kuisha sehemu mbalimbali na Yanga kutangazwa bingwa huku Toto, African Lyon na JKT Ruvu kushuka daraja, kulitokea na nakala ya risiti ya DHL kwa Simba kwenye mitandao ya kijamii, ikionesha kutumwa kwa kipeto chao kwenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), kwa kuishitaki Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwa kuwanyima pointi tatu za "Kagera na Simba Saga"

CAS NI NINI?

Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS - Court of Arbitration for Sport), imeanzishwa mwaka 1984 ikiwa chini ya Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki na ICAS, kwa kuhudumia rufaa na malalamiko yote ya michezo mbalimbali ikiwemo na mpira wa miguu, na kutoa suluhisho la sintofahamu mbalimbali.

MAAJABU YA SIMBA

Moja, Simba analalamika kukata rufaa FIFA kabla ya kupitia CAF, cha ajabu wamenda FIFA moja kwa moja wakishitaka TFF, baada ya kupeleka rufaa yao CAF na ndio waeleke CAS au waende CAS moja kwa moja.

Pili, wanasema wamenda FIFA - Strasie 20, 8044 Zürich nchini Uswizi, wakati CAS ipo Cheteuu de bethusy, CH 1012, Lausanne nchini Uswizi, ni ajabu la mwaka.

Tatu, ukisoma kanuni kuu za CAS, zinawataka kutuma shauri lao ndani ya siku 21 kabla ya shida kutokea na litasikilizwa ndani ya miezi sita mpaka kumi na mbili, lakini viongozi wa Simba wametuma FIFA na sio CAS kama ibara ya 49 (muda wa kutuma rufaa au malalamiko ya mlalamikaji sio mlalamikiwa au taasisi yake) inavyosema.

Nne, Kanuni kuu cha CAS zinasema, ibara ya 31 inasema sio lazima kutuma malalamiko kwa njia kama DHL n.k, lakini unaweza tumia njia ya haraka na wepesi kwa barua pepee procedures@tas-cas.org, tazama viongozi wa simba walichofanya.

Tano, ibara ya 49, 64.1 na 65.2 inaeleza juu ya malalamiko au rufaa kwa CAS, sio FIFA yanalipiwa Swiss franc 1000, lakini Simba hawajaonesha kama wamelipia hicho kiasi.

UCHAGUZI WA SIMBA

Nimemtambua Katibu wa Simba kupitia mgogolo huu, Bwana Hamis Kisiwa, lakini aliyetuma barua ya kilo 1.5 ni Kamanda wa Vita, Geofrey Nyange.

Ukitazama kwa jicho la kimafuriko ya maji yaliyofunguliwa bwawa la Kihansi, kisha kuaribu mipunga ya wakulima wengine huko Morogoro, Chita.

Viongozi wa Simba wanatafuta agenda ya mkutano mkuu wao utakaofanyika mwaka huu, ukiwa na agenda moja wapo ya uchaguzi mkuu wa viongozi hao.

Wanatazama ahadi zao wakati wakiomba ridha ya kuongoza Simba sasa, hawajatimiza mpaka sasa kwa asilimia kubwa, kama ubingwa hawajapata VPL, uwanja wao bado changamoto na mambo mengi nichangamoto.

Wakifanikiwa la kuwadanga hili la CAS, huku wao wakisema na kuhubiri FIFA, basi tutegeme Rais wa sasa kurudi tena kuongoza Simba na watu wake.

Kama wakishindwa kuwadanganya basi namuona Mc. Adam Raga wa Tabora akirudi tena kuongoza Simba, baada ya kuwadanganya kwenda FIFA badala ya CAS.

FIFA wana Bodi ya Sheria, ina Kamati ya Nidhamu (Disciplines Committee) hapa ndio uanzakuamua mambo mbalimbali, ukishindwa kutambua maamuzi yao basi unakata rufaa, Kamati ya Rufaa (Appeal Committee) kwa maamuzi tofauti na matarajio yako, kwakuangalia kanuni za maadili ya kimaamuzi "FIFA Disciplinary Code Decisions", pia maamuzi ya CAS uzingatiwa kama utaanzia huko kabla ya kamati.

Sasa Simba watuambie wamenda wapi FIFA kwa kanuni zipi, ofisi ipi au kamati ipi? Au wamenda CAS kwa taratibu zipi?

Dar es Salaam Young Africans (Yanga) endeleni kushangilia ushindi wenu ni halali, kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu za TFF, CECAFA, CUF na FIFA.

Simba Hoyeeeeee!

Mwisho!

0715011406
 
Reactions: Ftc
Pilipili usiyoila...........
.
 
Bahati nzuri FIFA haiamini kamwe katika kutoa points mezani. Sana sana itakuwa fines tu kwa wote waliohusika ila ubingwa ndo hivyo tena kwani matokeo ya uwanjani kati ya Simba vs Kagera Sugar yatabaki kama yalivyo.
Malinzi na wahaya wenzie ndo wamewadanganya hivo??
 
We jamaa muongo sana kweli simba haitaki ubingwa inafanya mazungumzo na wakati jana yule tapeli wenu kawaonyesha waandishi wa habari kielelezo kuwa barua au rufaa yao imepokelewa au unataka tuamini maneno ya RAGE kuwa Simba ni mbumbumbu?!!
 
unawafaham lakini? au huwa unawasikia tu
Mkuu,
Najaribu kujipa utulivu wa kifkra ili nione watafanya nn.. Lakini wewe tayari usha set conclusion ya maamuzi yao. Too biased,

Huoni kama kweli kuna tatizo hio itakuwa mechanism ya ku regulate na kufanya check and Balance ya soka kupitia shirikisho letu, ambalo limekuwa kama samaki aliyeoza kwa muda mrefu? Na pengine kipelekea kuinua soka letu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…