Hii ndio "Status" ya Jeshi la Polisi kwa sasa

Hii ndio "Status" ya Jeshi la Polisi kwa sasa

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Na mimi naomba nianze na Mods; Dear Mods hiki ninachoandika ni facts based na sio sio maneno ya kuokoteza, nikipata picha tutatupia pia, naomba muivumilie tu.

Ndugu zangu yafuatayo ni matukio mbali mbali yanayoipa Jeshi letu la Polisi Mtazamo hasi kwenye Jamii yetu, matukio haya hayazingatii wakati (chronological) kikubwa ni tukio lenyewe.

  1. Ni Jeshi la Wala Rushwa Wakubwa: Nenda kituo chochote kile cha Polisi sasa hivi, report tukio lolote lile lakini liwe linakuhusu wewe, ni lazima utaambiwa utoe kitu kidogo. Kama hutaambiwa direct basi utajengewa mazingira ya kuwapa kitu chochote (hii inajumuisha vitengo vyote unavyovijua vya Polisi) Kwa mfano; kujiunga Na jeshi hilo lazima utoe kidogo, hapa na mimi yalinikuta nilipotaka kujiunga na Polisi mwaka 2000 kupitia Mkoa wa Tanga, nikakosa pesa ya kutoa na nikakosa nafasi, Trafiki Barabarani ndio usiseme, last time nimesafiri ilibidi niwape maparachichi, ni omba omba. Rushwa kubwa inawahusu wakubwa wa jeshi hili na matukio yapo wazi kwa leo tuyaache kwanza Ona mfano huu
    Juzi juzi nili kwenda kuomba kuaptiwa hati ya tabia njema ili nisafiri kwenda shule ughaibuni. Nilipofika makao makuu ya jeshi la polisi nili kwenda mapokezi nikaeleza shida yangu. Nilielekezwa kwenda kitengo cha finger print identification (IB). Kwanza kumwona afsa wa kunipatia maelezo ilikuwa mbinde chenga kibao....baadaye nikaambiwa kulipia. Nilipo lipia nikaombwa pesa nyingine 20000/= kwa ajili ya kuchukuliwa alama za vidole. Baadaye jamaa akaniuliza nina kwenda wapi, nikamwambia nakwenda kusoma SA kwa muda wa mwaka mmoja, then lini unasafiri nika mwambia tarehe ya safari kwa nia njema tu...Baadaye akasema njoo uchukuwe barua baada ya wiki tatu, mbele zaidi ya tarehe ya safari akidai kuwa maombi ni mengi mno....Lakini ukitoa ushirikiano hata kesho una pata tu. Ushirikiano ni 50000/=....Nilipotoa hiyo nikaambiwa kakae nje kidogo..baada ya masaa mawili nilichukuwa barua....WANAKULA RUSHWA HATA MAKAO MAKUU YA JESHI SI MCHEZO
  2. Jeshi la Wauwaji: Refer matukio mengi yanayoteka hivi karibuni currently yule mtoto aliepigwa risasi ya kisogoni na askari, askari kujipiga risasi, Mwangosi, wafanyabiashara wa madini. Majambazi siku hizi hawakamatwi wakiwa HAI bali ni risasi tu ndio zinatembea, sijuikama wanafundishwa kulinda au kuua. Nina hakika wasingewaua wangeweza kudhibiti source za haya mambo.
    Malele ana siri nzito juu ya mtandao mpana wa mauaji ndani ya jeshi la polisi unaohusisha watumishi wengine kutoka vyombo vya ulinzi na usalama, wafanya biashara na wanasiasa. Mtandao huo unatajwa na malele ambaye ni mkazi wa kijiji cha Igoma, kwimba mwanza, kuwa ndio uliohusika na mauaji ya kamanda Barlow usiku wa kuamkia octoba 13 mwaka jana ktk eneo la Kitangiri jijini mwanza, alipokuwa anamrejesha mwalimu anayetajwa kwa jina la Doroth Moses, aliyekuwa naye ktk kikao cha Arusi
  3. Jeshi la Dhuluma: Refer mali za watu hapa zinazoporwa na Polisi (matukio ya Mtwara ni udhihirisho) Kamanda mmoja wa Polisi alikutwa anatumia gari lililokuwa la Wafanyabiashara wa Madini ambao waliuwawa. Ongeza
  4. Jeshi la Kulinda Wachache: Refer mikutano ya siasa inavyozuiliwa bila sababu za kimantiki ili tu kulinda maslahi ya watu wachache, refer mauwaji ya wananchi kwenye Migodi, mamia wanapoteza maisha; Soma japo kwa ufupi sehemu hii
    Mkurugenzi wetu Mketo alipojulishwa jambo hilo aliomba akutane na mama huyo. Baada ya kikao, Mketo na viongozi waandamizi wa wilaya akiwamo mhe. Kulaga ambaye ni katibu wetu wa wilaya walianza safari ya kuelekea Msimbati ambako mama huyo amejisitiri baada ya kubakwa na kunyimwa msaada na vyombo vilivyopaswa kumsaidia.
    Kwa taarifa zenye ushahidi, hadi sasa askari jeshi hao wameshawakamata na kuwapeleka makambini zaidi ya wananchi 100 ambapo wote hao wameteswa kinyama kwa kuvuliwa nguo zote, kumwagiwa maji mwili mzima, kupakwa chumvi mwilini na kuanza kutandikwa viboko vya miti maalum na kisha wakimaliza kuteswa huachiwa na kurudishwa uraiani kuuguza vidonda vinavyotokana na vipigo. Hakuna utawala wa sheria Mtwara, ni ubabe, ukatili na dhuluma.
    J. Mtatiro,
    Naibu Katibu Mkuu,
    Chama Cha Wananchi CUF,
    Tanzania Bara.
    +255717536759.
  5. Jeshi la Madawa ya Kulevya: Refer madawa yaliyokamatwa Mbeya baadae jamaa wakaweka unga madawa wakauza, huku mtaani kwangu jamaa wanasema kabisa Polisi wanawadai pesa ili wasiwakamate na wakija kwako wakikamata madawa basi wanawauzia wengine ili wakauze. Jamaa anasema unaweza pigiwa simu na Polisi ukifika wanakwambia mzigo huu hapa panda dau.....Refer pia magunia ya Bangi 18 tena yalikamatwa kwenye Gari la Polisi - Kilimanjaro tena Refer askari waliopata ajali Arusha wakisafirisha bangi asubuhi asubuhi kwenye gari ndogo
  6. Bw. Elli naunga mkono hoja yako na kuongeza lingine linaloniuzi zaidi
Jeshi la Polisi ni Watesaji na Wasiozingatia Haki za Binadamu,
- angalia pale mtuhumiwa anapokamatwa, hawakuambii kosa lako wanakunyanyua juu juu na makofi na mateke. Mwambiemtu kosa lake kwanza alaf mwambie anahitajika kituoni sio lazima kumpiga. ninachukia sana nikiona raia anapigwa na polisi, hawajui una tatizo la kiafya wala hawajali watoto wako wanakuangalia unavyopokea mkong'oto. namna hii sidhani kama watapata ushirikiano wa raia.

Possible Causes
  1. Maslahi duni sana ya Askari wetu ukilinganisha na nature ya kazi yao
  2. Kulifanya jeshi la Polisi la watu waliofeli na kufoji vyeti
  3. Askari wachache kulazimishwa kulinda maslahi ya wakubwa wachache
  4. Kukosa nidhamu ya kazi kutokana na mfumo wenyewe wa jeshi kukosa udhobiti na kugeukia kwenye siasa

What is the Way Forward
  1. IGP iwe ni taaluma ya kuomba, kusailiwa na kuchaguliwa
  2. Askari wapate haki zao stahili kwa wakati ikiwepo matibabu na makazi
  3. Overtime ziwe zenye maslahi
  4. entry point za polisi ipimwe kutokana na uelewa na sio vyeti wala kuangalia urefu au ufupi wa mtu
  5. Various training courses zifanywe both psychological and physical sio kushika bunduki tu

Haya ni machache tu lakini NJIA RAHISI ya kutoka hapa tulipo ni hii; Jeshi letu lijitambue kuwa ni la Raia kwa faida ya raia wote wakubwa na wadogo, ni wajibu wao kutulinda. Nipo tayari kuwanadaalia Training Manual ya kisasa na curriculum ili kuokoa jeshi letu.

nawasilisha
 
Mkuu watu wanajiunga na jeshi kwa vimemo. Yote uliyosema ni kweli Madale tuliporwa hadi leo hatujarudishiwa mali zetu pamoja na kuwatambua polisi waliopora.

Litaondoka na CCM hata kama ni miaka mingi inayokuja.
 
kikubwa mkuu ni maslahi duni hawa jamaa wanapanga nyumba uswahilini na pesa zao zakuungaunga hata hizo overtime zao za uonezi mkubwa!
 
kikubwa mkuu ni maslahi duni hawa jamaa wanapanga nyumba uswahilini na pesa zao zakuungaunga hata hizo overtime zao za uonezi mkubwa!

Yeah yeah asante kwa kunielewa, wanamaisha magumu ajabu ya Mungu....thanks
 
Asante Mpwa wangu kwa kukubaliana na mimi ila mimi nataka tuwaangalie Polisi kwa Jicho La Pili, tutafute Mbinu Mbadala ya kuwafanya wawe upande wa sisi wanyonge
Mkuu watu wanajiunga na jeshi kwa vimemo. Yote uliyosema ni kweli Madale tuliporwa hadi leo hatujarudishiwa mali zetu pamoja na kuwatambua polisi waliopora.

Litaondoka na CCM hata kama ni miaka mingi inayokuja.
 
Pia kupewa vyeo kwa undugu na kujuana. Huambatana na kulipa fadhira
 
Asante Mpwa wangu kwa kukubaliana na mimi ila mimi nataka tuwaangalie Polisi kwa Jicho La Pili, tutafute Mbinu Mbadala ya kuwafanya wawe upande wa sisi wanyonge
Sawa, ila mfumo hauruhusu. CCM wamefanikiwa kwa kuwa na tawi la chama ndani ya majeshi. We raia ni mahali pa kuvunia tu wala polisi hawatambui kuwa wewe ndiye mwajiri. Sababu ni kuwa watawala pia hawatambui kuwa raia (wapiga kura) ndio waajiri
 
Mpwa hata mimi nilikua nawachukia sana but nimefikiria kuwa ni vyema tutafute mbinu mbadala wa kuwapaenda; mimi ni victim mkubwa sana wa Hawa watu ambao walishanisweka Rumande pale Urafiki tarehe 30/09/2010 kisa chenyewe ni cha kipuuzi sana, wakadai niwape 50,000/= pale Urafiki. ilikua ni uonevu wa hali ya juu sana na niliumia sana sana na namba ya yule askari alienileta pale Ninayo hadi leo na jina ninalo bado nafikiria jinsi ya kumuonyesha kuwa alichokifanya it was not fair
mimi sipendi hata kuwaona nikiwaona tu kichefuchefu serious nawachukia ppolisi sana,
 
Eti ilibidi uwape maparachichi, ha ha haaaaa hii nayo kali!
 
Polisi iwe chini ya JWTZ,nidhamu na utendaji utakua wa ufanisi
 
No No ni kweli na ni wale pale Maili Kumi baada ya kupita Korogwe......niliwaonea huruma ilikua ni mwezi wa nne natoka kijijini, wakanikagua wakakuta kila kitu kiko okay, ndipo yule kijana akaniambia Mzee njaa bhana, nikamwambia sina kitu natoka kijijini ila nina matunda hapa, ndio akaniomba nikampatia ila kwa CONDITION kuwa yawe yameiva ili wale pale pale....ni rahisi sana kuwa poisoned kwa njia hii
Eti ilibidi uwape maparachichi, ha ha haaaaa hii nayo kali!
 
Na mimi naomba nianze na Mods; Dear Mods hiki ninachoandika ni facts based na sio sio maneno ya kuokoteza, nikipata picha tutatupia pia, naomba muivumilie tu.

Ndugu zangu yafuatayo ni matukio mbali mbali yanayoipa Jeshi letu la Polisi Mtazamo hasi kwenye Jamii yetu, matukio haya hayazingatii wakati (chronological) kikubwa ni tukio lenyewe.

  1. Ni Jeshi la Wala Rushwa Wakubwa: Nenda kituo chochote kile cha Polisi sasa hivi, report tukio lolote lile lakini liwe linakuhusu wewe, ni lazima utaambiwa utoe kitu kidogo. Kama hutaambiwa direct basi utajengewa mazingira ya kuwapa kitu chochote (hii inajumuisha vitengo vyote unavyovijua vya Polisi) Kwa mfano; kujiunga Na jeshi hilo lazima utoe kidogo, hapa na mimi yalinikuta nilipotaka kujiunga na Polisi mwaka 2000 kupitia Mkoa wa Tanga, nikakosa pesa ya kutoa na nikakosa nafasi, Trafiki Barabarani ndio usiseme, last time nimesafiri ilibidi niwape maparachichi, ni omba omba. Rushwa kubwa inawahusu wakubwa wa jeshi hili na matukio yapo wazi kwa leo tuyaache kwanza
  2. Jeshi la Wauwaji: Refer matukio mengi yanayoteka hivi karibuni currently yule mtoto aliepigwa risasi ya kisogoni na askari, askari kujipiga risasi, Mwangosi, wafanyabiashara wa madini. Majambazi siku hizi hawakamatwi wakiwa HAI bali ni risasi tu ndio zinatembea, sijuikama wanafundishwa kulinda au kuua. Nina hakika wasingewaua wangeweza kudhibiti source za haya mambo.
  3. Jeshi la Dhuluma: Refer mali za watu hapa zinazoporwa na Polisi (matukio ya Mtwara ni udhihirisho) Kamanda mmoja wa Polisi alikutwa anatumia gari lililokuwa la Wafanyabiashara wa Madini ambao waliuwawa. Ongeza
  4. Jeshi la Kulinda Wachache: Refer mikutano ya siasa inavyozuiliwa bila sababu za kimantiki ili tu kulinda maslahi ya watu wachache, refer mauwaji ya wananchi kwenye Migodi, mamia wanapoteza maisha

Possible Causes
  1. Maslahi duni sana ya Askari wetu ukilinganisha na nature ya kazi yao
  2. Kulifanya jeshi la Polisi la watu waliofeli na kufoji vyeti
  3. Askari wachache kulazimishwa kulinda maslahi ya wakubwa wachache
  4. Kukosa nidhamu ya kazi kutokana na mfumo wenyewe wa jeshi kukosa udhobiti na kugeukia kwenye siasa

What is the Way Forward
  1. IGP iwe ni taaluma ya kuomba, kusailiwa na kuchaguliwa
  2. Askari wapate haki zao stahili kwa wakati ikiwepo matibabu na makazi
  3. Overtime ziwe zenye maslahi
  4. entry point za polisi ipimwe kutokana na uelewa na sio vyeti wala kuangalia urefu au ufupi wa mtu
  5. Various training courses zifanywe both psychological and physical sio kushika bunduki tu

Haya ni machache tu lakini NJIA RAHISI ya kutoka hapa tulipo ni hii; Jeshi letu lijitambue kuwa ni la Raia kwa faida ya raia wote wakubwa na wadogo, ni wajibu wao kutulinda. Nipo tayari kuwanadaalia Training Manual ya kisasa na curriculum ili kuokoa jeshi letu.

nawasilisha

Polisi wengi wamelaaniwa,laana hiyo unaweza kuiona vizuri wanapo staff kazi.nasikushauri ujiunge na jeshi hilo la polisi,ni bora uwe mwanajeshi ulinde mipaka ya nchi yetu.
 
Polisi wengi wamelaaniwa,laana hiyo unaweza kuiona vizuri wanapo staff kazi.nasikushauri ujiunge na jeshi hilo la polisi,ni bora uwe mwanajeshi ulinde mipaka ya nchi yetu.
Mpwa wangu kumbuka polisi hawa ni ndugu zetu, ni baba na mama zetu, uncles na Aunt zetu tutafute namna nzuri ya kuwafanya tuwapende bhana nao wajiskie amani na kuona kuwa wanachokifanya ni wajibu wao kwa ajili yetu sote.
 
Kamwe huwezi kuliofanya jeshi la Polisi liwe la RAIA eti kwa kuanzisha dhana ya Ulinzi shirikishi.....
 
Mpwa chuki hii haitajenga bali itabomoa mimi nataka tujenge Jeshi hili liwe la kwetu na sio la kwako peke yao
ukweli toka moyoni mwangu...i hate this watu called police....hata awe katika haligani siwezi mpa msaada wowote....
 
Asante Mpwa wangu kwa kukubaliana na mimi ila mimi nataka tuwaangalie Polisi kwa Jicho La Pili, tutafute Mbinu Mbadala ya kuwafanya wawe upande wa sisi wanyonge

You're wasting your time buddy. Diplomatic solutions wiii never end corruption and other kind of evils done by the current police force in tz. What we need now is total demolition of the current police unit. Put all the cops out of of action for 6 month suspend everybody out there! Jwtz can take charge of police activities during those 6 months. Recruit some fresh blood of educated youths and train them to be the proper police of the people!a
 
Back
Top Bottom