Mpwa wangu Mentor, kuna vitu ambavyo vinahitaji utulivu tu na maamuzi ya busara, tunaweza au ninaweza kuli-shape taratibu na kimya kimya hadi siku moja kila mtu akalifurahia, sio uchawi. Ni kuamua tu siku moja kuwafumbia macho na masikio hao wakubwa. Kwa mfano tukisema na tukaamua kuwa IGP iwe ni post ya kutangazwa na kusailiwa huoni tutakua na mwanzo mzuri, then tunashuka hadi kwa ma-RPC kuwa wawe promoted si kwa vigezo vya undugu, urafiki, udini, ukanda au ukabila, kunakuwa na Kamati huru yenye kuyafanya haya, huoni tutakua na mwanzo mzuri na kuwa na jeshi la mfano?
Au Askari wetu mmoja amekosea, basi awe punished openly na instantly kusiwe na kusita wala kuyumbisha, Yes We can