Mzee wa Usafi
JF-Expert Member
- Apr 16, 2008
- 644
- 292
Juzi juzi nili kwenda kuomba kuaptiwa hati ya tabia njema ili nisafiri kwenda shule ughaibuni. Nilipofika makao makuu ya jeshi la polisi nili kwenda mapokezi nikaeleza shida yangu. Nilielekezwa kwenda kitengo cha finger print identification (IB). Kwanza kumwona afsa wa kunipatia maelezo ilikuwa mbinde chenga kibao....baadaye nikaambiwa kulipia. Nilipo lipia nikaombwa pesa nyingine 20000/= kwa ajili ya kuchukuliwa alama za vidole. Baadaye jamaa akaniuliza nina kwenda wapi, nikamwambia nakwenda kusoma SA kwa muda wa mwaka mmoja, then lini unasafiri nika mwambia tarehe ya safari kwa nia njema tu...Baadaye akasema njoo uchukuwe barua baada ya wiki tatu, mbele zaidi ya tarehe ya safari akidai kuwa maombi ni mengi mno....Lakini ukitoa ushirikiano hata kesho una pata tu. Ushirikiano ni 50000/=....Nilipotoa hiyo nikaambiwa kakae nje kidogo..baada ya masaa mawili nilichukuwa barua....WANAKULA RUSHWA HATA MAKAO MAKUU YA JESHI SI MCHEZO