Hii ndiyo Dubai bwana

Kaka na wewe upo ustaadhi nikusalimie!l kiarabu Aslaam aleykuum🤣🤣🤣Au nikusalimie kibantu🤣🤣🤣!!!!!
 
Huyo jamaa namshangaa sanaa yaan sijui ana tatizo sema ndio unaamua kukausha tu humu kuna watu Wana matatizo ya akili na inatakiwa twende nao taratibu tu
Hii jamii forums inaruhusu kila aina ya mtu kuwemo Kwa hio tuwavumilie kidogo
 
Tunalipa kodi ,hao walio pewa dhamana ya kufanya hayo wanakuwa wapi hadi linakuwa korongo,ndo ujue weusi ni mabwege[emoji2]
 
Mkuu,

Huwezi kulinganisha uchumi wa mafuta na uchumi wa katani.
Ona jinsi ulivyo na uwezo mdogo wa kufikiri,

Angalia hiyo Dubai,imejengeka kwa hiyo natural resource ya mafuta uliyoitaja,angalia nchi nyingi za Africa,zina almost kila aina ya natural resources,kuanzia madini,mito,ardhi nzuri yenye rutuba,mbuga za wanyama...

Halafu jipige kichwani ili kureset uwezo wako wakufikiri ili siku nyingine usilete pumba zako hapa.
 
Kweli mkuu uwezi kulinganisha.lakini hata tungekuwa na mafuta kama hayo ya Dubai tungetoboa mzee baba?,Check Nigeria,Niger,drc n,k
Sisi tatizo letu ni akili, si rasilimali.

Na hili ni tatizo la msingi zaidi, maana unaweza kukosa rasilimali, ukatumia akili kufanikiwa.

Ukikosa akili, hata ukiwa na rasilimali zitapotea bure tu.

Ingawa hatuna uchumi wa mafuta, hata uchumi wetu wa sasa haulingani na rasilimali zetu.

Tulipotea njia tangu tulipoamua kugawana umasikini kwenye ujamaa.
 
Sisi tatizo letu ni akili, si rasilimali.

Ingawa hatuna uchumi wa mafuta, hata uchumi wetu wa sasa haulingani na rasilimali zetu.

Tulipotea njia tangu tulipoamua kugawana umasikini kwenye ujamaa.
basi nikwambie kitu mkuu tungekua na matumizi mazuri ya akili hata kwa huo uchumi wa mkonge na rasilimali zingine tulizonazo tungetoboa,au nasema uongo chif?
 
Hizi swimming polles za Dubai ni kwa ajili ya wageni tu maana wao havui nguo hadharani, kuna haja gani ya kuwa na mali halafu huimjoi?
 
basi nikwambie kitu mkuu tungekua na matumizi mazuri ya akili hata kwa huo uchumi wa mkonge na rasilimali zingine tulizonazo tungetoboa,au nasema uongo chif?
Ulichoandika ndicho nilichoongezea kwenye bandiko langu uliloninukuu baada ya wewe kunukuu na kabla sijasoma maandishi yako.

Tumefikiria kitu kimoja.
 
Ulichoandika ndicho nilichoongezea kwenye bandiko langu uliloninukuu baada ya wewe kunukuu na kabla sijasoma maandishi yako.

Tumefikiria kitu kimoja.
tuko pamoja mkuu,ila kama ntakua sijakosea kuna reply moja ulisema atuwezi kulinganisha uchumi wa mafuta na mkonge,,baada ya mimi kuuliza miaka ya 60's tulikua uchumi sawa na Dubai?,
ila wewe ukaleta jibu moja la msingi ambalo nimeelielewa,kwamba sisi atuna matumizi mazuri ya akili.hapo tuko sawa kabisa wala atujatofautiana mkuu.
 
Hata Dar ingeweza kuwa hivi endapo Watanzania wangeamua kuwajaribisha wengine zaidi ya wale wale wa kila siku!.
P

Tunahitaji mabadiliko mapya ya ki fikra, yaani hata kuweka taa za Barabarani na ktk mitaa tu zimetushinda achia mbali mashimo na ufinyu wa barabara zetu na uchafu ulio zagaa kila maeneo hasa ktk miji mikubwa

Na mbaya kuna wenzetu wanasafiri kila mara ktk nchi hizo zilizoendelea lkn hawana hamu hata shauku tu ya kubadili hali zetu hata kwa kuiga yale madogo ambayo yapo ndani ya uwezo wetu
 
Kwa ambao hamjawahi fika Dubai mnatakiwa kujua ule mji umegawanyika sehemu mbili. Kuna Dubai hii mpya inayoendelea kujengwa ambako ndo kuna lile jengo refu na majengo mengine mazuri ya kisasa. Zile hotel zenye Dolphins ziko upande huo. Dubai Mall pia iko huko. Picha za mleta uzi hiyo ni Dubai mpya. Matajiri kama Shilole na Kajala mdo hufikia huko.

Pia kuna Dubai ya kizamani huko Deira na Sharjah. Pale Deira ndo sisi choka mbaya huwa tunafikia. Hoteli hata kwa Tsh 70k unapata. Na kuna apartments zilizokodishwa na wabongo ambazo nao wanatulaza sisi kama vile wanafunzi kwenye madeka. Ni bei nafuu sana. Wanachaji kama Dirham 150 kwa wiki. Kimsingi huu upande wa swekeni maisha ni marahisi. Ili twende sawa na watoto wa kishua huwa tunaenda kule Dubai mpya na kupiga picha za kutosha kwa ajili. Pamoja na Deira kuwa sweken bado ni pa moto mno... pasafi hatari hakuna vumbi kabisa. Soko la vito vya dhahabu ndo liko huko Deira (Gold souk). Hata maduka ya simu mengi ya bei rahisi unayakuta Deira. Kimsingi hili ni eneo la wafanyabiashara waliofuata mizigo. Ukitaka bata panda taxi nenda mitaa ya Burj Khalifa.

Sehemu ambayo utaona uchafu na kujihisi upo bongo ni Sharjah maeneo wanapouza computer used. Mnaotaka kwenda Dubai msiogopeshwe. Ukiwa na milioni zako 3 unaenda na kurudi kwa raha zako. Milioni 3 inakava nauli, malazi na msosi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…