Hii ndiyo Gharama ya Kufunga Mfumo wa VAR, Tanzania bado sana hatuwezi

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
VAR SYSTEM

1. Gharama zake ni kiasi gani?
Kusimika mtambo wa VAR inagharimu £4.6M sawa na 14.5B Tsh.

2. Inaendeshwa chini ya chombo gani?
VAR Huendeshwa chini ya IFAB International Football Association Board) (Bodi ya kimataifa ya shirikisho la soka)

3. Mtu Yeyote anaweza Oparate?
*Hapana, VAR ni mali ya IFAB, ina maana ukihitaji kusimika VAR nchini mwako utalazimika kuipata toka kwao tu.

4. Gharama za waendeshaji zikoje na nani analipia?
Gharama za uendeshaji zipo juu sana hulipiwa na vilabu viwili husika vitakavyokuwa vinacheza siku hiyo, kwa mfano kuna mchezo wa FA cup kati ya Rochdale na Oxford United walijikuta wana bill ya £9251 (29M Tsh) pamoja VAT. Kwa kifupi hiyo bili hugawanywa kwa vilabu vyote viwili.Kwa ligi kama yetu kama utahitaji kulipia michezo yote 240 itabidi vilabu vikohoe chini kidogo ya 7B Tsh kwa msimu

5. Kunahitajika nini ili kufanikisha uwepo wa VAR.

VAR huhitaji mazingira tulivu, kufanya kazi bila mihemko au mashinikizo ili iweze kutoa majibu yasiyo na shaka na yaliyo wazi.

Huwa haiharakishwi kutoa majibu, lakini hupendeza kutoa majibu haraka ili kuwafanya wachezaji, makocha na mashabiki kutoingiwa na mihemko wakisubiri majibu.

MAELEZO YA ZIADA
VAR system huweza kutumia camera 33 zilizo simikwa kwenye viwanja tofauti kwa mchezo mmoja, kwa baadhi ya viwanja England hutumia camera 38 na zote ni 5K zenye ubora wa picha wa hali ya juu kabisa kwa sasa duniani.

Katika hizo, camera 8 ni za (Super slow motion) mwendo wa pole.

Na 4 ni za ultra slow motion) mwendo wa pole wa ziada.
_Hii yote ni kumpa mwamuzi wa VAR wigo mpana wa kuona pande zote za tukio kabla ya kutoa maamuzi.

Ligi tajiri Afrika kama PSL
(South African Soccer
League) imeshindwa kuwa na VAR SYSTEM na sababu kubwa inayotolewa ni gharama kubwa za uendeshaji wake.
 
Watumie camera za Azam, kung'amua makosa yenye utata maana mechi zote zinarushwa live
 
Ingependeza kama gharama ikawa kubwa zaidi ya hapa ili washindwe hadi watakapong'amua kuwa sheria number one ya soka ni Kiwanja, na wakaanza Kudial na viwanja kwanza na siyo VAR.

Hapo wataweza hii gharama hata kwa mkopo.
 
Tuwekeze katika viwanja ili tupate kuona mechi bora.

Kwa kuanza na var wanaweza funga tv ya azam uwanjani ikasaidia kufanya mrejeo iyo itatosha kuanzia
 
VAR yanini watu wanachezea kwemye Mitope
Waache Ushabiki Maandazi kisa Litimu lako lime droo basi Uamue Kufanya jambo Tena kwa Pesa si Zako
 
Kwani c lzm tukatumia hz za kwao wkt ni waz kuwa ili kupata marejeo ya mechi wanatazama video za Azam tu hkn kipya Azam waweke video uwanjani kukitokea shida refa ajiridhishe
 
VAR SYSTEM

1. Gharama zake ni kiasi gani?
Kusimika mtambo wa VAR inagharimu £4.6M sawa na 14.5B Tsh.

2. Inaendeshwa chini ya chombo gani?
VAR Huendeshwa chini ya IFAB International Football Association Board) (Bodi ya kimataifa ya shirikisho la soka)

3. Mtu Yeyote anaweza Oparate?
*Hapana, VAR ni mali ya IFAB, ina maana ukihitaji kusimika VAR nchini mwako utalazimika kuipata toka kwao tu.

4. Gharama za waendeshaji zikoje na nani analipia?
Gharama za uendeshaji zipo juu sana hulipiwa na vilabu viwili husika vitakavyokuwa vinacheza siku hiyo, kwa mfano kuna mchezo wa FA cup kati ya Rochdale na Oxford United walijikuta wana bill ya £9251 (29M Tsh) pamoja VAT. Kwa kifupi hiyo bili hugawanywa kwa vilabu vyote viwili.Kwa ligi kama yetu kama utahitaji kulipia michezo yote 240 itabidi vilabu vikohoe chini kidogo ya 7B Tsh kwa msimu

5. Kunahitajika nini ili kufanikisha uwepo wa VAR.

VAR huhitaji mazingira tulivu, kufanya kazi bila mihemko au mashinikizo ili iweze kutoa majibu yasiyo na shaka na yaliyo wazi.

Huwa haiharakishwi kutoa majibu, lakini hupendeza kutoa majibu haraka ili kuwafanya wachezaji, makocha na mashabiki kutoingiwa na mihemko wakisubiri majibu.

MAELEZO YA ZIADA
VAR system huweza kutumia camera 33 zilizo simikwa kwenye viwanja tofauti kwa mchezo mmoja, kwa baadhi ya viwanja England hutumia camera 38 na zote ni 5K zenye ubora wa picha wa hali ya juu kabisa kwa sasa duniani.

Katika hizo, camera 8 ni za (Super slow motion) mwendo wa pole.

Na 4 ni za ultra slow motion) mwendo wa pole wa ziada.
_Hii yote ni kumpa mwamuzi wa VAR wigo mpana wa kuona pande zote za tukio kabla ya kutoa maamuzi.

Ligi tajiri Afrika kama PSL
(South African Soccer
League) imeshindwa kuwa na VAR SYSTEM na sababu kubwa inayotolewa ni gharama kubwa za uendeshaji wake.
Sisi titabakia kuelezea mitambo ya wenzetu hamna jingine, viwanja tu vya mipira vya kisasa kila mkoa ni shida sembuse hiya VAR.....
 
Gharama za uendeshaji mnawalipa watz ambao wapo control room. Posho zao ni kwa standard za bongo. Haifiki 29M. Kama siko sahihi unisahihishe
Bahati mbaya lazima muingie mkubaliano na wenye makumpuni yaliyopitishwa na FIFA
 
Back
Top Bottom