Hii ndiyo Gharama ya Kufunga Mfumo wa VAR, Tanzania bado sana hatuwezi

Hii ndiyo Gharama ya Kufunga Mfumo wa VAR, Tanzania bado sana hatuwezi

Mashabiki wa makolo fc wanapambana sana kuipinga VAR.
Jitahidini mshinde kihalali
Nchi yenyewe ni kama kiota cha ndege, watu wake wananuka shida kila kona ya miili yao, kwenye michezo team zinacheza kwenye mabwawa badal ya kutengeneza viwanja eti mafukara nao mnawaza VAR[emoji28].
 
VAR SYSTEM

1. Gharama zake ni kiasi gani?
Kusimika mtambo wa VAR inagharimu £4.6M sawa na 14.5B Tsh.

2. Inaendeshwa chini ya chombo gani?
VAR Huendeshwa chini ya IFAB International Football Association Board) (Bodi ya kimataifa ya shirikisho la soka)

3. Mtu Yeyote anaweza Oparate?
*Hapana, VAR ni mali ya IFAB, ina maana ukihitaji kusimika VAR nchini mwako utalazimika kuipata toka kwao tu.

4. Gharama za waendeshaji zikoje na nani analipia?
Gharama za uendeshaji zipo juu sana hulipiwa na vilabu viwili husika vitakavyokuwa vinacheza siku hiyo, kwa mfano kuna mchezo wa FA cup kati ya Rochdale na Oxford United walijikuta wana bill ya £9251 (29M Tsh) pamoja VAT. Kwa kifupi hiyo bili hugawanywa kwa vilabu vyote viwili.Kwa ligi kama yetu kama utahitaji kulipia michezo yote 240 itabidi vilabu vikohoe chini kidogo ya 7B Tsh kwa msimu

5. Kunahitajika nini ili kufanikisha uwepo wa VAR.

VAR huhitaji mazingira tulivu, kufanya kazi bila mihemko au mashinikizo ili iweze kutoa majibu yasiyo na shaka na yaliyo wazi.

Huwa haiharakishwi kutoa majibu, lakini hupendeza kutoa majibu haraka ili kuwafanya wachezaji, makocha na mashabiki kutoingiwa na mihemko wakisubiri majibu.

MAELEZO YA ZIADA
VAR system huweza kutumia camera 33 zilizo simikwa kwenye viwanja tofauti kwa mchezo mmoja, kwa baadhi ya viwanja England hutumia camera 38 na zote ni 5K zenye ubora wa picha wa hali ya juu kabisa kwa sasa duniani.

Katika hizo, camera 8 ni za (Super slow motion) mwendo wa pole.

Na 4 ni za ultra slow motion) mwendo wa pole wa ziada.
_Hii yote ni kumpa mwamuzi wa VAR wigo mpana wa kuona pande zote za tukio kabla ya kutoa maamuzi.

Ligi tajiri Afrika kama PSL
(South African Soccer
League) imeshindwa kuwa na VAR SYSTEM na sababu kubwa inayotolewa ni gharama kubwa za uendeshaji wake.
Tuboreshe viwanja kwa kutandika nyasi bandia. mambo ya VAR ni siasa tu
 
GSM anaweza kujitolea kufunga VAR kwenye viwanja vya nchi nzima, si ana hela nyingi🐒
 
Hiyo billion 14 inatosha kabisa kuweka kapet na taaa za viwanja vyote vya ccm
 
Hizo fedha zitumike kufundisha waamuzi wenye viwango qu hata ikiwezekana wazitumie kuleta waamuzi wenye viwango kutoka nje kusaidiana na wale wanaofanya vizuri ndani ya nchi
 
Kombe la Dunia napo nchi washiriki huwa wanalipia hizi gharama kwa kila mechi? kama ilivyo kwenye Vilabu
 
Kwani c lzm tukatumia hz za kwao wkt ni waz kuwa ili kupata marejeo ya mechi wanatazama video za Azam tu hkn kipya Azam waweke video uwanjani kukitokea shida refa ajiridhishe

Hizo fedha zitumike kufundisha waamuzi wenye viwango qu hata ikiwezekana wazitumie kuleta waamuzi wenye viwango kutoka nje kusaidiana na wale wanaofanya vizuri ndani ya nchi
Hao waamuzi wa nje wenyewe wanatumia VAR
 
Mashabiki wa Yanga wanakomaa kweli isiwekwe...
 
Back
Top Bottom